28/02/2023
ZIARA ya maafisa wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar na wataalam kutoka kwenye miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa ๐ช๐บ๐น๐ฟ kwa ufadhili wa European Union in Tanzania inaendelea kisiwani Pemba kwa siku ya pili.
Katika ziara hiyo inayoongozwa na Afisa mkuu wa Utafiti kutoka Wizara hiyo, Dkt. Suleiman Shehe, leo Februari 28, wametembelea wanufaika mbalimbali wa mradi wa unaotekelezwa na , , ambao ni wakulima na wasindikaji wa mazao ya kilimo na kupata picha halisi ya mwenendo wa utekelezaji wa shughuli za mradi huo katika kufikia lengo la kukuza mnyororo wa thamani kwa mazao ya Viungo, mboga na matunda.
Wakiwa katika ziara hiyo, wanufaika wa miradi iliyo chini ya programu ya ๐ช๐บ๐น๐ฟ wamehimizwa kuzingatia suala la uwekaji kumbukumbu ya shughuli zao ili kujua gharama za uendeshaji na faida zake kwenye shughuli hizo.
https://www.instagram.com/p/CpM2HBKtHuu/?igshid=MWMzM2Q4ZmE=