Tanzania Crypto Community

Tanzania Crypto Community Crypto Education Support From TANZANIA. Tunatoa huduma za elimu ya CRYPTO na BLOCKCHAIN TECHNOLOGY.

HISTORIA YA BITCOIN TOKA MWAKA 2008 MPAKA SASAINAENDELEA..kwa bitcoin alizokuwa nazo elfu kumi ni sawa na kwamba pizza h...
16/07/2023

HISTORIA YA BITCOIN TOKA MWAKA 2008 MPAKA SASA
INAENDELEA..
kwa bitcoin alizokuwa
nazo elfu kumi ni sawa na kwamba pizza hiyo ilifikia thamani ya
dola za Marekani milioni mia moja tisini na saba na nukta nane
tatu ($ 197.83 milioni). Malipo hayo yamebaki historia mpaka
sasa. Anajutiaje? Wengi wanasema aliidharau, je angetunza hizo
bitcoin basi angekuwa sehemu ya matajiri wakubwa duniani.
Tangia wakati huo bitcoin bado haikupata umaarufu wala
kujulikana sana. Mpaka kuanzia miaka ya 2010 hadi 2015 bitcoin
ikawa inatumika katika biashara haramu k**a za madawa ya
kulevya. Mtandao huo wa biashara haramu ulijulikana k**a Silk
Road, ulishamiri sana huko Marekani na ukawa muhimu kwa
sababu malipano yalifanyika kwa siri sana kati ya mtu na mtu na walilipana bila kujuana na ilikuwa sio rahisi kwa serikali kuingilia
na kuwajua wahusika. Bitcoin ilikuwa na uwezo wa kununua kila
kitu na bidhaa yoyote kupitia mtandao huo. Mpaka serikali ya
Marekani ilipokuja kugundua na mtandao huo kuvunjwa rasmi.
Hata hivyo biashara hiyo ilikuwa na matokeo rasmi mawili.
Moja, kwa mtandao huo wa bitcoin kutumika katika biashara
haramu basi ikavuma kwamba bitcoin imezaliwa kuwa pesa ya
kihuni, ya majambazi, ya wahalifu na magaidi. Hasa kwa sababu
mtandao huo wa Silk Road uliweza pia kutumia bitcoin kulipia
magaidi wa kujitoa mhanga na kununua silaha kwa shughuli za
mashambulizi ya kigaidi. Tukio hilo lilisababisha kuyumba sana
kwa bitcoin, na kujengewa picha hasi katika jamii.
Mbili, ikawa faida kwa bitcoin. Kwa sababu ya kuhusianishwa na
matukio ya kihalifu na biashara halamu, basi ikapelekea bitcoin
kutangazwa sana katika vyombo vya habari duniani kote.





Itaendelea follow ukurasa Kwa muendelezo zaidi

HISTORIA YA BITCOIN TOKA MWAKA 2008 MPAKA SASAMwaka 2008 Satoshi Nakamoto aliandika walaka uliyoelezea namna ambavyo pes...
16/07/2023

HISTORIA YA BITCOIN TOKA MWAKA 2008 MPAKA SASA

Mwaka 2008 Satoshi Nakamoto aliandika walaka uliyoelezea
namna ambavyo pesa ya digitali (bitcoin) ingeundwa kuwezesha
kulipana kwa kati ya mtu na mtu bila kuingiliwa au kusimamiwa
na chombo chochote. Mwaka mmoja baadaye 2009, bitcoin ya
kwanza ikazaliwa katika mfumo wa kompyuta unaoitwa code.
Hiyo code ikaambatanisha na taarifa katika gazeti lililoandika
kuhusu kuanguka kwa benki kubwa huko Uingereza baada ya
mtikisiko mkubwa wa mfumo wa pesa duniani uliyoanzia
Marekani, k**a ishara ya kushindwa kwa mfumo wa kifedha
uliyopo sasa.
Muamala wa kwanza wa bitcoin ulianza rasmi baada ya Satoshi
Nakamoto kutuma bitcoin kwa Hal Finey mtaalamu mwingine wa
kompyuta raia wa Marekani. Cha kustaajibisha ni kwamba tangu
kuandika kwa walaka uliyoelezea utaalamu wa kutengeneza hii
pesa ya digitali, Satoshi Nakamoto haijulikani duniani kote ni mtu
gani. Kwamba ni mtu mmoja au kikundi cha watu, ni mwanamke au mwanaume na anatokea wapi. Pia kumekuwa na fununu
kwamba ni CIA walitengeneza au serikali ya nchi ya Marekani, au
Freemason isipokuwa hawataki ijulikane wazi. Lakini wengine
wakadai kwamba nguri wa kompyuta Hal Finney ambaye alikuwa
wa kwanza kupokea muamala wa bitcoin ndio mvumbuzi wa
bitcoin na mfumo wa pesa za digitali. Hata hivyo nae alikataa
katakata kabla ya kifo chake mwezi wa 8 mwaka 2014.
Miaka ya mwanzoni tangia 2009, bitcoin iliyonekana k**a
takataka kitu kisicho na maana na wala thamani yoyote. Zaidi
ilikuwa inajulikana miongoni mwa watu wachache sana, kati yao
ni wataalamu wa kompyuta. Na mwezi wa Tano tarehe 22 mwaka
2010 mtu aliyejulikana kwa jina la Laszlo Hanyecz alitoa jumla ya
bitcoin 10,000 kulipia piza, kitu ambacho ni historia ya
kustaajabisha duniani kote mpaka sasa maana kulingana na
thamani ya juu zaidi ya bitcoin iliyofikiwa mwezi Disemba mwaka
2017, ya dola za Marekani elfu kumi na tisa mia saba themanini
na tatu na nukta sufuri sita ($19783. 06)

FAIDA ZA MFUMO MPYA WA PESA BITCOIN AND BLOCKCHAIN Kuwekeza katika miradi mahali popote duniani Ujio wa pesa za digitali...
14/07/2023

FAIDA ZA MFUMO MPYA WA PESA BITCOIN AND BLOCKCHAIN

Kuwekeza katika miradi mahali popote duniani
Ujio wa pesa za digitali umewezesha watu kufanya biashara na
kuwekeza mahali popote duniani. Awali ilikuwa si rahisi kumiliki
hisa za makampuni ya Marekani k**a vile Google au Facebook
ukiwa Tanzania. Kwa mfumo huu mpya kumekuwa na ongezeko
la njia nzuri kwa kutumia bitcoin kununua hisa za makampuni
katika mataifa makubwa duniani. Biashara za hisa zilikuwa
zinahitaji watu wenye kipato kikubwa na uelewa mkubwa lakini
ujio wa intaneti na upatikanaji wa taarifa kwa urahisi inawezesha watu kushiriki katika masoko ambayo ilikuwa vigumu kuyafikia
na kuvuna faida. Mfano app ya Abra inafungua mlango wa mtu
yeyote duniani kupitia jukwaa lake kununua na kumiliki hisa za
makampuni makubwa, pesa za digitali na ETF.
 Kinga dhidi ya mfumko wa bei (infalation)
Mfumko wa bei ni wakati ambapo thamani ya sarafu inashuka, na
bei ya vitu kupanda. Hali hii huwa inapelekea ugumu wa maisha.
Kwa ujio wa teknolojia hii mpya ni salama zaidi kwa sababu pesa
za kigitali zinatabia ya kupanda thamani, hivyo kuwa kinga dhidi
ya kushuka kwa thamani na kukuleteta faida. Ndio maana
haistajabishi kutambua kuwa mwaka ambao bitcoin ilizaliwa 2008
ulikuwa mwaka wa mtikisiko mkubwa wa uchumi duniani.
Ambapo kulitokea mfumko mkubwa wa bei ya vitu na kushuka
kwa thamani ya dola.

ukurasa huu uweze kujifunza zaidi.

TUKUTANE KATIKA MAKALA YAJAYO TUWEZE KUJIFUNZA HISTORIA YA BITCOIN NA JINSI ILIVYOWEZA KUBADILISHA MAISHA YA WATU WENGI DUNIANI


FAIDA ZA MFUMO WA PESA MPYA BITCOIN AND BLOCKCHAIN.Usawa kwa wote Ni mfumo ambao tajiri sana aliyeko Marekani na Mkulima...
14/07/2023

FAIDA ZA MFUMO WA PESA MPYA BITCOIN AND BLOCKCHAIN.

Usawa kwa wote
Ni mfumo ambao tajiri sana aliyeko Marekani na Mkulima
aliyeko kijijini Kamsamba Mbozi wote wanakuwa na fulsa sawa ya
kunufaika na mfumo huu mpya. Hii inawezekana kutokana na
wimbi la simu za kisasa na upatikanaji wa mtandao kusambaa
karibu kila kona ya dunia.
 Urahisi wa kutuma pesa kwa gharama nafuu
Katika mfumo wa pesa za makaratasi wa sasa ni gharama kubwa
kutuma pesa kati ya nchi na nchi. Kunapokuwa na urahisi wa
kutuma pesa kati ya nchi na nchi hufanya uendeshaji wa biashara
kuwa rahisi pia, hivyo kuleta maendeleo na kukuza uchumi
kuendana na kasi ya utandawazi. Pia kulingana na taarifa za
Mpango wa Maendeleo Endelevu Duniani (SDGs) kumekuwa na
gharama kubwa za kuwezesha utumaji pesa kati ya nchi kwa
mfumo wa pesa wa sasa. Ambapo ada ya kutuma pesa ni asilimia
saba (7%) tofauti na lengo la asilimia tatu (3%). Na gharama ni kubwa zaidi kiasi cha kufikia 8.97% inapohusu nchi za Africa.
Teknolojia hii mpya ya bitcoin na mfumo wa pesa wa digitali
unarahisisha utumaji wa pesa kwa gharama nafuu chini ya 3%, na
kikubwa zaidi pesa hufika kwa wakati.
 Usiri na usalama zaidi
Pesa yako katika mfumo wa digitali inakuwa ni siri. Hakuna
anayeweza kujua unamiliki kiasi kadhaa, isipokuwa wewe
mwenyewe. Mfumo unakuwa unatambua mtu fulani ana pesa
(bitcoin) kiasi fulani lakini jina Lake Halijulikani. Pia pesa katika
mfumo huu ni salama kabisa. Kazi ya mtu anayemiliki pesa hii ni
kutunza tu neno la siri.
 Ni rahisi kutumia
Huitaji kubeba pesa zako kwenye begi au mfuko, ndani ya simu
pekee inatosha na unaweza lipia huduma au bidhaa sehemu
yoyote duniani kwa urahisi zaidi. Kazi pekee ni kutunza neno lako
la siri (nywila). Na hutahitaji kubadilisha shilingi kwenda Yen ya
Japan ili kulipia gari lako toka Japan. Ukiwa na bitcoin inatosha
kutumika mahali pote duniani.

ukurasa huu uweze kujifunza zaidi ITAENDELEA.

TOFAUTI YA BITCOIN NA MFUMO WA PESA WA SASAHauna mtu wa katikati (trustless). Katika mfumo wa teknolojia mpya hakuna mtu...
14/07/2023

TOFAUTI YA BITCOIN NA MFUMO WA PESA WA SASA

Hauna mtu wa katikati (trustless).
Katika mfumo wa teknolojia mpya hakuna mtu wa kumuamini
asimamie au kuidhinisha matumizi ya pesa yako. Huitaji kutuma
pesa yako benki, au posta au kwa njia ya simu ili imfikie mtu
mwingine kwa ajili ya malipo. Isipokuwa ni mfumo wa moja kwa
moja kati ya mtu na mtu (peer-to-peer). Mimi nina rafiki yangu
Diana, ananiuzia saa. Nakuwa na pesa yangu bitcoin
imehifadhiwa kwenye pochi (simu yangu au kompyuta),
nabonyeza tu batani tayari inaenda kwa Diana. Diana akipokea
hiyo pesa mfumo mzima duniani unathibitisha pesa imetoka kwa
mtu fulani kwenda kwa mwingine, na kutambuliwa kwa anuani
zao za kidigitali bila kujua majina halisi ya mtumaji na mpokeaji.
Ila pesa inaonekana kwenye mfumo kwamba muamala
umefanyika kikamilifu.
 Uwazi (transparency)
K**a nilivyoeleza hapo juu, katika mfumo huu mpya hakuna
pesa ambayo inapita njia za panya, bali inakuwa wazi katika
mfumo mzima, na pesa yoyote inakuwa ndani ya mfumo na
kumbukumbuku zinahifadhiwa kila mahali duniani. Mwingine
anaweza kuona kiasi kadha kimetumwa toka anuani fulani
kwenda nyingine, kwa hiyo hakuna wizi. Fikiria kwa sasa ilivyo
ngumu kujua pesa yako iliyotumwa kwa mfumo wa benki kujua
ipo hatua gani. Zaidi utalazimika kurudi benki kuwauliza wahudumu pesa uliyotuma ipo hatua gani, na pia huchukua muda
mrefu kumfikia mlengwa.
 Kinga dhidi ya udhibiti (censorship-resistance)
Hakuna chombo maalumu au serikali kinachosimamia na
kudhibiti uendeshaji wa pesa katika teknolojia hii mpya. Na kwa
sababu ni mfumo ambao umesambaa duniani kote hakuna
sehemu ya udhaifu ya kuathiri mfumo mzima. Ni mfumo ambao
unahifadhi kumbukumbu zilizothibitishwa na kuhalalishwa
duniani kote, hivyo hakuna mahali unaweza dhibitiwa na
kukwamisha muamala. Ni tofauti na sasa ambapo serikali inaweza
kuingilia umiliki wa pesa za mtu fulani na kuzuilia kibali cha
umiliki au kutaifisha kabisa.

TOFAUTI YA BITCOIN NA MFUMO WA PESA WA SASANi mfumo mtawanyiko (decentralized) Hakuna mwenye mamlaka ya kusimamia pesa z...
14/07/2023

TOFAUTI YA BITCOIN NA MFUMO WA PESA WA SASA

Ni mfumo mtawanyiko (decentralized)
Hakuna mwenye mamlaka ya kusimamia pesa za mtu, kila mmoja
ana haki ya kutunza na kusimamia matumizi ya pesa zake
mwenyewe. Fikiria pesa ile umeweka benki, na inakaa huko
mikononi mwa watu wengine. Huwezi kujua pesa yako inafanyiwa
nini. Wachache watajua wanafanyia nini, lakini tena sio kwa faida
ya mwenye pesa, ni kwa faida yao wenyewe waliyokutunzia.
Pia usalama wa pesa yako kwa mfumo wa sasa unakuwa mdogo,
pale benki ikafilisika ni kwamba pia pesa yako inakuwa imepotea.
Vilevile kwa kuwa hiyo pesa ipo kwa msimamizi mmoja,
kukitokea uharibifu na udhaifu katika mfumo wao wa
kumbukumbu ya pesa ni kwamba pesa yako inakuwa imepotea.
Mfumo wa sasa umetambua udhaifu huo, ambapo pesa yako
haihifadhiwi katika sehemu moja bali katika mtandao wa
kompyuta zote duniani. Kwa mwizi kufanikiwa kuiba pesa yako
katika teknolojia hii mpya ya pesa itamhitaji kuingilia mfumo wa
kompyuta zilizo katika mtandao wa kutunza kumbukumbu kwa
asilimia 51 (51%). Mfano rahisi k**a ni kompyuta 100
zilizotawanyika kote duniani na zinatunza kumbukumbu zako za
pesa basi wezi itabidi waweze kuingilia mfumo wa kompyuta 51
kati ya hizo 100 ndipo waweze kufanikiwa kuiba pesa yako. Kulingana na utafiti wa GoBitcoin.io ili kufanikiwa kudukua
mfumo wa bitcoin kwa 51% itakugharimu $8 bilioni ya vifaa tu.
Kitu ambacho si rahisi, na hivyo kuhakikishia usalama wa mfumo
mzima wa bitcoin daima.

ukurasa huu uweze kujifunza zaidi ITAENDELEA.

TOFAUTI YA BITCOIN NA MFUMO WA PESA WA SASABitcoin na Mfumo Tofauti wa Pesa Tumeangalia kwamba mfumo wa pesa wa dunia ul...
14/07/2023

TOFAUTI YA BITCOIN NA MFUMO WA PESA WA SASA

Bitcoin na Mfumo Tofauti wa Pesa
Tumeangalia kwamba mfumo wa pesa wa dunia uliyopo sasa
umehodhiwa na chombo husika katika kila nchi. Na kadri mtu
anapokuwa karibu na huo mfumo ndipo ananukia utajiri na
kusababisha ukosefu wa usawa katika jamii. Na mtu aliyekalia huo
mfumo wa pesa anakuwa ni mwenye nguvu na kutawala
mwelekeo wa maisha ya wengine.
Sasa imezaliwa njia mbadala ambayo inakuja kutengeneza usawa
na kila mmoja kuwa na nafasi katika kusimamia mfumo wa pesa.
Katika dunia ya sasa wimbi kubwa la kuondoa mfumo huu wa
sasa na kuja mfumo wa pesa ambao uko mikononi mwa kila mtu
unafanikiwa kutokana na ongozeko kubwa la upatikanaji na
umiliki wa simu za kisasa (smart phones), ikiambatana na
kutanuka kwa upatikanaji wa huduma za mtandao (internet) na
kuzaliwa kwa njia za wazi na za usawa katika mfumo wa pesa za
digitali k**a bitcoin.
Mfumo huu mpya ambao unasambaa kwa kasi na kuelekea
kuuondoa mfumo wa sasa umekuja na sifa kuu sita (6) ambazo
ndio nguzo za teknolojia mpya ya pesa duniani.
Hauna kibali wala mipaka(permisionless and borderless)
Katika teknolojia hii mpya kila mmoja duniani anaweza kumiliki
na kufanya miamala ya pesa bila kuingiliwa na chombo chochote
k**a benki au serikali, na bila kujali kiwango cha utajiri, ajira ya
mtu, au umiliki wa akaunti ya benki kwa sababu ni mfumo huru
na wa wazi, na hauna msimamizi (gate keeper).

ukurasa huu uweze kujifunza zaidi ITAENDELEA.

INAENDELEA MFUMO WA PESA WA SASAUchakachuaji wa pesa Chombo husika au serikali inaweza kuchakachua pesa na kusababisha m...
14/07/2023

INAENDELEA MFUMO WA PESA WA SASA

Uchakachuaji wa pesa
Chombo husika au serikali inaweza kuchakachua pesa na
kusababisha mfumko wa bei kwa kuzalisha noti nyingi kinyume
na nguvu ya uchumi, hatimaye kusababisha zaidi ugumu wa
maisha kwa wananchi. Mifano ni katika nchi ya Zimbabwe na
Venezuela. Nchini Venezuela wananchi wanahitaji kusukuma
mkokoteni wa noti za Boliviar ili wakalipie mkate kutokana na
mtikisiko mkubwa wa uchumi uliyoikumba nchi hiyo, ikiwa ni
pamoja na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na Marekani hivyo
kushuka sana kwa thamani ya sarafu yao.

 Kushindwa kwa chombo husika ni kushindwa kwa mfumo
mzima
Unapokuwa na chombo kimoja cha kusimamia pesa, k**a benki
kuu au serikali, inapotokea udhaifu wa hicho chombo basi
unakuwa ni udhaifu wa mfumo mzima katika nchi, na kuathiri
kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi au dunia nzima. Ni mfano wa
mayai yote kuwekwa katika kikapu kimoja, ukidondosha kikapu
hicho basi mayai yote yatapasuka bila kuambulia hata yai moja.

Tukutane katika makala yajayo tuone tofauti ya mfumo wa pesa wa SASA na Bitcoin

INAENDELEA MFUMO WA PESA WA SASA.Pesa ya Tanzania haiwezi kufanya kazi Marekani Biashara ni dunia nzima, na utagundua ku...
14/07/2023

INAENDELEA MFUMO WA PESA WA SASA.

Pesa ya Tanzania haiwezi kufanya kazi Marekani
Biashara ni dunia nzima, na utagundua kuwa kufuatana na
utandawazi basi kumekuwa na urahisi wa kufanya biashara
kirahisi duniani. Wakati hilo limepiga hatua, lakini utandawazi
huu haujaendana na utandawazi wa malipo ya kipesa. Kwanza
kuna gharama ya kubadilisha pesa kutoka sarafu ya nchi moja
kwenda sarafu ya nchi nyingine. Mbili kuna gharama ya kutuma
hiyo pesa ili kumfikia mlengwa, mfano mwepesi unahitaji utume
shilingi milioni 10 Ulaya. Basi utahitaji kubadili hiyo pesa kwenda
Yuro ambayo ni pesa inayotumika Ulaya. Na ukishaibadilisha
unalazimika tena kuongeza kiasi cha juu kulipia gharama za
kuituma hiyo pesa. Mbali na hayo pesa hiyo inabidi iidhinishwe
na chombo husika, k**a vile benki kuu. Hapo tena kuna mawili:
kuidhinishwa au kukataliwa.
 Inahitaji uwe na akaunti ya benki
Mfumo huu wa pesa wa sasa unalazimisha watu kuwa na akaunti
benki ili uweze kukopa au kutunza pesa zako. Lakini kulingana
na masharti ya kufungua akaunti benki na kukosekana kwa
matawi ya benki kumfikia kila mwananchi kumekuwa ni tatizo
kubwa sana. Hata ukitaka kununua kitu kwa njia ya mtandao
kulingana na kasi ya utandawazi unalazimika mpaka uwe na
akaunti ya benki. Na inakadiriwa watu wazima karibia bilioni 1.7
duniani kote hawana akaunti ya benki wala ya mtandao wa simu
kutunza pesa. Pia kumiliki na kuendesha akaunti ya benki ni
gharama, kulipia kila mwisho wa mwezi. Muda mrefu wa kutuma pesa nchi nyingine au kati ya benki
mbili tofauti.
Katika mfumo wa pesa wa sasa inachukua muda mrefu sana
kutuma pesa kwenda nchi nyingine, au kutoa pesa benki moja
kwenda benki nyingine hata ndani ya nchi hiyo hiyo moja. Hivyo
kupunguza ufanisi katika uendeshaji wa malipo na biashara.

Kwa mafunzo zaidi ITAENDELEA

IJUE BITCOIN MLANGO MPYA WA UTAJIRI DUNIANI.Mfumo wa Pesa wa Sasa.  Ni Pesa za makaratasi Ulimwenguni kote zinatumika p...
14/07/2023

IJUE BITCOIN MLANGO MPYA WA UTAJIRI DUNIANI.

Mfumo wa Pesa wa Sasa.
 Ni Pesa za makaratasi
Ulimwenguni kote zinatumika pesa ambazo ni za makaratasi au
sarafu. Mfumo huu ulizaliwa zaidi ya miaka 500 iliyopita kutokana
na wafanya biashara wa wakati huo kuwa na wakati mgumu
kuendesha biashara zao hivyo walihitaji kitu ambacho kinaweza
wakilisha thamani ya bidhaa zao lakini kiwe chepesi kubebeka.
Sio mtu apeleke ng’ombe sokoni halafu arudi na gunia la
mahindi. Basi zikazaliwa pesa za sarafu na makaratasi
tunazotumia sasa kupunguza mzigo.
 Pesa hizi zinasimamiwa na chombo husika katika mfumo
wa kuhodhi (centralization)
Kila nchi duniani ina pesa yake, na husimamiwa na chombo
maalumu. Mfano kwa Tanzania ni Benki Kuu ya Tanzania
(BOT), Marekani ni Federal Reserve na India inaitwa Reserve
Bank of India (RBI). Usimamizi wa pesa zote unawekwa katika
mikono ya watu wachache, kwa kuaminiwa (trusted).
Wachambuzi wa masuala ya pesa duniani na masuala ya haki na
usawa wamedai mfumo huu uliyopo umechangia kutengeneza utajiri mkubwa kwa watu wachache wale waliyoaminiwa kutunza
pesa, na idadi kubwa ya wananchi duniani kubaki maskini. Na
kulingana na tafiti ya Edelman Trust Barometer imeonesha kuwa
taasisi za kusimamia fedha ndio zina kiwango kidogo cha
kuaminiwa na wananchi duniani.
 Ni rahisi kugushi
Mara nyingi tumesikia kuna pesa bandia, mtu amelipwa kwa kazi
ya jasho lake pesa bandia ambazo hazina thamani na uhalali
kabisa. Mtu anajitengenezea pesa feki kwa ajili ya kuwaibia
wengine.
 Zina tabia ya kushuka thamani
Tumeshuhudia jinsi ambavyo pesa zinaondolewa kwenye
mzunguko, mfano ni shilingi moja, shilingi tano, shilingi kumi na
shilingi 20, na zingine nyingi zilikuwemo kwenye mzunguko lakini
kwa kadri ya wakati zimepoteza thamani haziwezi tena kukidhi
malipo ya ununuzi wa bidhaa au huduma.

TUMEANZA KUANGALIA MFUMO WA PESA WA SASA ILI TUWEZE KUONA TOFAUTI ILIYOPO KATIKA BITCOIN NA MFUMO WA PESA WA SASA.

ukarasa huu kwa mafunzo zaidi.

IJUE BITCOIN MLANGO MPYA WA UTAJIRI DUNIANIBitcoin ni nini? Bitcoin ni pesa ya digitali ambayo ilizaliwa mwaka 2009, mpa...
14/07/2023

IJUE BITCOIN MLANGO MPYA WA UTAJIRI DUNIANI

Bitcoin ni nini?
Bitcoin ni pesa ya digitali ambayo ilizaliwa mwaka 2009, mpaka
sasa bitcoin imefikisha miaka 10. Pesa hii imeundwa kwa mfumo
wa kompyuta, na inafanya kazi kwa mtandao wa kompyuta
ambapo kila kompyuta katika huo mtandao inatunza
kumbukumbu ya kila bitcoin, hata ikiwa katika kiwango cha
desimali. Pesa hizi hujulikana kwa Kiingereza k**a
cryptocurrency au digital money. Unaweza jipatia na kumiliki
bitcoin zako kwa njia ya kompyuta au simu.
Lengo kuu la kuzaliwa kwa bitcoin ni kuwezesha njia ya kulipana
pesa kwa urahisi kati ya mtu na mtu bila msuguano (frictionless),
na pia bila mtu wa katikati kusimamia (trustless), na zaidi kwa
lengo la kutokuingiliwa na chombo chochote k**a benki au
serikali (permisionless) duniani. Pia ni pesa ya kutumika dunia
nzima bila mipaka. Huitaji kuibadili k**a ilivyo kwa shilingi ya
Tanzania kwenda dola za Marekani au Yuro ili kuitumia nchi
zingine. Ni pesa ambayo kusudi lake kuu ni kwamba ukiwa nchi
yoyote unaweza kuitumia kununua bidha na kulipia huduma
k**a vile chumba cha hoteli bila kuibadilisha na thamani yake
kubaki ile ile popote ulipo. Pesa hii unakuwa umeitunza kwa
akaunti yako ambayo unaweza ifungua kwa simu au kompyuta na
kutumia vifaa hivyo kumhamishia mwingine wakati wa malipo.
Sehemu nyingi duniani zinaitambua na kupokea malipo katika
bitcoin.

ukurasa huu uweze kujifunza zaidi kuhusu BITCOIN, CRYPTOCURRENCY NA TECHNOLOGY YA BLOCKCHAIN.

ITAENDELEA

FURSA ZINAZOPATIKANA KATIKA CRYPTOCURRENCY1. Nafasi ya Uwekezaji: Cryptocurrency inatoa fursa kubwa ya uwekezaji na kupa...
14/07/2023

FURSA ZINAZOPATIKANA KATIKA CRYPTOCURRENCY
1. Nafasi ya Uwekezaji: Cryptocurrency inatoa fursa kubwa ya uwekezaji na kupata faida kubwa. Baadhi ya sarafu k**a vile Bitcoin, Ethereum, na Litecoin zimepata umaarufu mkubwa na kuongezeka kwa thamani yao kwa miaka iliyopita. Watu wamepata fursa ya kununua na kuuza sarafu hizi kwa matumaini ya kupata mapato ya ziada.

2. Teknolojia ya Blockchain: Cryptocurrency inategemea teknolojia ya blockchain, ambayo ina fursa nyingi zaidi ya kuongeza thamani na ubunifu katika sekta mbalimbali. Teknolojia ya blockchain inaweza kutumika katika usimamizi wa ugavi, udhibiti wa utambulisho, mikataba smart, na hata katika sekta ya afya. Hii inafungua fursa za kazi na ubunifu katika maeneo haya.

3. Malipo ya Kimataifa: Cryptocurrency inatoa fursa ya malipo ya kimataifa haraka na gharama nafuu. Kwa kutumia sarafu za dijitali, watu wanaweza kufanya malipo ya haraka na salama kwa wenzao ulimwenguni kote, bila kuhitaji kampuni za kifedha za kimataifa au ada kubwa za uhamishaji.

4. Uwezeshaji wa Kifedha: Cryptocurrency inatoa fursa ya kuwawezesha watu ambao awali hawakuwa na upatikanaji wa huduma za kifedha. Kwa mfano, katika maeneo ambapo watu hawana akaunti za benki, wanaweza kutumia cryptocurrency kufanya malipo na kuhifadhi thamani yao. Hii inawapa watu fursa ya kushiriki katika uchumi wa dijitali.

5. Uwezeshaji wa Wajasiriamali: Cryptocurrency inatoa fursa kubwa kwa wajasiriamali kuchangia katika uchumi wa dijitali. Wajasiriamali wanaweza kuunda sarafu zao za dijitali (ICO) na kukusanya fedha kwa kupitia njia ya umma. Hii inawapa fursa ya kupata ufadhili na kuendeleza miradi yao.

6. Uaminifu na Usalama: Cryptocurrency inatoa fursa ya kuongeza uaminifu na usalama katika miamala ya kifedha. Teknolojia ya blockchain inahakikisha kuwa miamala yote imehifadhiwa kwa usalama na kudhibitishwa na washiriki wote. Hii inaweza kusaidia kupunguza udanganyifu na kuongeza uaminifu katika mfumo wa kifedha.

LIKE AND SHARE UKURASA HUU KWA MAFUNZO ZAIDI

Address

Www. Bitcoin. Com
Nyegezi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Crypto Community posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category