Wana MNH wote ni kitu kimoja katika shida na raha. Wana MNH ni lazima tukuze mfuko wetu wa chama. iii, Vilevile tunaamini kwamba mti mmoja haujengi nyumba na kidole kimoja hakivunji chawa. Wanachama wote ni sawa bila kujali umri,hadhi au uongozi. Fitina,majungu na upendeleo ni mwiko kwetu.
3.0) DHUMUNI/ DIRA
i. Kumfariji mwanachama aliyepatwa na msiba au tatizo lolote. Kuwa sambamba naye kwa
yaliyomsibu,mazishi,kuuguza na kadhalika. Kumsaidia mwanachama,asiteteleke kwa yaliyompata. Kufahamiana na kudumisha undugu. Kusaidiana katika shida na raha. Kubuni mbalimbali za kutunisha mfuko ili tuinuane kiuchumi.
3.1) SHIDA
i. Ugonjwa
iii. Matatizo mengine
3.2) RAHA
i. Harusi (kuoa/kuolewa)
ii.Sherehe ya chama
4.0) SIFA ZA KUJIUNGA NA MNH
i. Awe mkazi/mzaliwa wa Mwanza
ii. Awe amejaza fomu ya kujiunga
iii. Awe ametoa kiingilio cha kujiunga katika umoja huu. Akubali kulipa ada ya kila mwezi. Awe mkweli katika kutoa taarifa za majanga na misiba. Awe msiri kwa shughuli zote za chama. Ajiheshimu na kuheshimu wanachama wenzake. viii. Awe na moyo wa kujitolea katika shughuli za chama. ix.Awe mtumiaji wa mtandao wa facebook. x. Aielewe na kuitetea katiba ya chama.
5.0) KIINGILIO
i. Kiingilio ni Tshs.5000 ( elfu tano tu)
ii. Ada ya kila mwezi ni Tshs. 2000 ( elfu mbili tu)
NB: Mwanachama mpya atalazimika kulipa ada na kiingilio ndipo anapokelewa.
6.0) HUDUMA KWA WANACHAMA
Wanaostahili kupata huduma ni:-
i. Mwanachama
ii. Wazazi/walezi wake
iii. Mke/mme
iv. Watoto
v. Kaka,dada na ndugu walio karibu.
6.1) HUDUMA ZA MWANACHAMA AKIFA:
i. Kulala msibani. Kushiriki kikamilifua kwenye mazishi. Ikitokea anasafirishwa,mwakilishi mmojaa kutoka kwenye chama chetu atasindikiza maiti na mfuko
wa chama utaghalimia nauli. NB: Mwanachama akifiwa na ndugu walioelekezwa kwenye ibara ya 6.0) atachangiwa Tshs.50000 (elfu hamsini)
Akifiwa au kufa taarifa zitolewe kwa viongozi.Wanachama watawajibika kufanya kazi kwa pamoja. Ndugu wawili wakipatwa na msiba,huduma yao itakuwa moja tu.
6.2) UGONJWA:
Huduma ya ugonjwa itatolewa kwa watu wafuatao:-
i. Mke/mme
iii. Watoto
iv. Wazazi/walezi
v. Kaka/dada wa kuzaliwa nae
NB: Mwanachama akuigua au kulazwa hospitali atatakiwa kutoa taarifa kwa viongozi ambao watafika hospitali au nyumbani kumuona.Pia uongozi utafuatilia gharama za matibabu na wanachama watatakiwa kuchangia gharama hizo kwa kiasi walicho nacho. Kumbuka,mgonjwa anayestahili kupata huduma hii ni yule liyelazwa hospitali kwa siku 3 au zaidi.
6.3) MATATIZO:
MATATIZO AMBAYO YATACHANGIWA NI:-
i. Nyumba kuungua au kuezuliwa na kimbunga. Kuvamiwa na majambazi nyumbani kwako na kuibiwa.
6.4) RAHA:
6.4.1) HARUSI:
i. Mwanachama atatoa taarifa miezi miwili kabla. Huduma hii itatolewa mara moja kwa mhusika. Kila mwanachama atatoa mchango wake kulingana na kiwango kilichoamuliwa na wanachama. Nusu ya fedha tutamnunulia zawadi na nusu tutampatia mhusika. NB: Pesa hii itatolewa na wanachama moja kwa moja kama mchango wa kawaida kuanzia siku taarifa inapotolewa.
6.4.2) SHEREHE YA CHAMA:
i. Sherehe ya chama itafanyika kila tarehe 24 march kila mwaka,ambayo ni siku ya kuzaliwa kwa
chama chetu. Kikao cha mwezi wa kwanza kila mwaka kitateua kamati ya sherehe. Kila mwanachama ni lazima kuchangia sherehe ya chama. Kushindwa kufanya hivyo bila sababu ya msingi atalazimika kulipa faini pamoja na mchango
wake. Mwanachama ambaye hakuhudhuria sherehe ya chama wakati amechangia na hana sababu inayokubalika hatawajibishwa kikatiba.
6.5) NYONGEZA:
i. Huduma zilizoainishwa kuanzia ibara ya 6.1 mpaka 6.3 huduma yake itatoka katika mfuko wa
chama. Mhusika amjulishe mara moja mjumbe wa maafa ili apate huduma yake haraka
iwezekanavyo kwa muda muafaka. Huduma itafikishwa kwa mlengwa na watu wawili au zaidi ikiwa ni pamoja na risti ya mtoa pesa
na sahihi yake na yeye kuweka sahihi pia. iv.Watu ambao ni ndugu ndani ya umoja huu wakipatwa na msiba unaowahusu wote pamoja
watapata huduma moja. Pesa zilizotolewa katika mfuko wa chama zitarudishwa na wanachama wakati wa kikao kwa kuchangia kiasi ambacho kimegawanywa kwa wanachama wote.
7.0) PESA:
i. Pesa ni ya wanachama wote hivyo wanayo haki ya kujua mapato na matumizi ya chama
wawapo ndani ya vikao vya chama kwa kipindi husika. Mfuko wa chama utajulishwa kila baada ya miezi mitatu.
7.2) MAPATO YA CHAMA YATATOKANA NA:
i. Kiingilio
ii. Ada ya kila mwezi
iii. Faini
iv. Kununua katiba
7.3) MATUMIZI YAKE:
i. Kukopeshana
iv. Matatizo yaliyoidhinishwa
v.Uchapaji fomu,katiba na vitabu vya risti.
7.4) WAJIBU:
i. Kila kiongozi aliye na pesa anapaswa kutoa tarifa ya pesa kila mwezi. Kila aliyekopeshwa ni lazima kurudisha mkopo kama alivyoahidi. Pesa ya chama haisafiri.
8.0) UKOMO WA UANACHAMA:
i. Akipoteza sifa kama zilivyoainishwa kwenye ibara ya 4.0 na 5.0
ii. Akifariki
iii. Akijitoa mwenyewe
iv. Akishindwa kutimiza masharti ya chama atakuwa amejiengua mwenyewe. mwanachama yeyote ambae atashindwa kutoa ada kwa miezi mitatu mfululizo bila sababu maalum na za msingi atakua amejitoa kwenye chama na kupoteza haki zake zote. mwanachama yeyote atakaeonesha vitendo vya udanganyifu kwa madhumuni ya kutaka kukihujumu chama kwa kutaka kujinufaisha yeye binafsi avuliwe uanachama na kupoteza haki zake zote. Akiandika barua ya kujivua au kujiondoa kwenye chama