Lenny Forex Institute

Lenny Forex Institute Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Lenny Forex Institute, Financial service, Nyamagana, Mwanza.

Let's kill market togetherYour warlmy welcome for mentorship services, signal services and account management just hit m...
11/07/2020

Let's kill market together
Your warlmy welcome for mentorship services, signal services and account management just hit me inbox🎼🎧

**IFAHAMU BIASHARA YENYE UTAJIRI MKUBWA DUNIANI,FOREIGN EXCHANGE (FOREX).THE AGE OF FINANCIALREVOLUTION.**Kwa ambao wali...
12/03/2020

**IFAHAMU BIASHARA YENYE UTAJIRI MKUBWA DUNIANI,FOREIGN EXCHANGE (FOREX).
THE AGE OF FINANCIAL
REVOLUTION.**
Kwa ambao walikua
hawafahamu kwamba,
biashara ya fedha za kigeni
(forex trading) ndiyo ndiyo
biashara yenye ujazo mkubwa
wa mapato (turnover) kwa
siku kuliko biashara yoyote
duniani. Inakadiriwa kwamba
kwa wastani wa siku moja
forex trading inafikia
turnover ya zaidi ya trilioni 4
za dola (ambazo kibongo
bongo ni k**a trillion 8000).
Hii ni maradufu hata ya
biashara inayofanyika pale new York stock exchange kwa siku ambayo yenyewe inafika kwenye dola
zaidi ya bilioni 70. Hivo ni dhahiri kabisa soko la fedha za kigeni (forex market) ndilo soko kubwa
zaidi ulimwenguni katika masoko yanayohusisha uwekezaji wa kifedha.
Hivo katika ujazo huo mkubwa wa biashara kwenye fedha za kigeni ni wazi kwamba kila siku kuna
utajiri mkubwa unaotengenezwa na biashara hii. Na ni watu wengi sana wananufaika nayo.
Biashara ya fedha za kigeni ni nini?
Kwa maana rahisi kabisa biashara ya fedha za kigeni ni kununua pesa ya nchi fulani na hapo hapo
kuuza pesa ya nchi nyingine ili kufanya ubashiri wa bei kwa lengo la kujipatia faida.
Mfano tu mimi nnavoenda kariakoo bureau de change pale nnapotoa shilingi 2100 na kununua dola
moja kwa dhumuni la kwamba huenda baada ya mwezi mmoja dola ile moja itapanda na kuuzwa 2350
na hivo ntakua nimepata faida. Hapo tunasema umejihusisha kwenye biashara ya fedha za kigeni.
Sababu kubwa inayovutia watu kuingia kwenye biashara hii nnayoiita ya? ubashiri?; ni kuwa thamani
ya fedha ya nchi fulani inakuwa na tabia ya kupanda au kushuka dhidi ya fedha ya nchi nyingine
kutegemeana na sababu nyinginyingi k**a hali ya uchumi na jiografia ya kiasiasa ambazo ntaziongelea
baadae. Hivo lengo hasa la wanaofanya biashara hii ni kutumia kupanda na kushuka huku kwa fedha
fulani ili kunufaika.
Biashara hii inafanyika vipi ?
Katika biashara ya fedha za kigeni kuna kitu kinaitwa hapa ni unakua unaongelea zile fedha ambazo
unataka kuzitumia katika kufanya ubashiri wako. Pair maarufu katika forex market ni k**a EUR/USD,
GBP/USD, USD/CHF na USD/JPY hizi pair zenye USD zinaitwa major pair.
Kabla ya kwenda moja kwa moja kuelezea fursa za biashara hii ya forex trading kwa Tanzania,
nitagusia kidogo wenzetu walioendelea nchi za ulaya, marekani na mataifa ya Asia namna
wanavoifanya biashara hii.
Kwa watu wa nchi hizo biashara ya FOREX inafanyika online. Yaani katika hayo mataifa huwa kuna
;FOREX brokers?; ambao mtu akishajiunga na broker wake basi anafanya deposit ambayo hiyo
inakuwa ndiyo mtaji wa muhusika. Baada ya hapo akisha ingia online kuna platform kwenye program
ambayo inasimamiwa na broker wake inakuwa inaonesha list ya pair za fedha za kigeni ndipo atakuwa
ananunua ama kuuza fedha zake.
Ila msingi mkubwa unakua ni ule ule mfano: k**a mtu ana mtaji wa $ 10,000 halafu anataka kufanya
ubashiri wa kununua EURO. Akiingia kwenye online platform yake ataona bei ya kununulia EURO ie
EURO/USD = 1.23 ikiwa na maana EURO moja inauzwa kwa dola 1.23. Hivo hiyo dola $ 10,000 kwa
bei ya 1.23 itaweza kununua EURO (10000/1.23)=8130.08
Kwa hiyo imetumika $ 10,000 ambayo imenunua EURO 8,130. Na mwekezaji amefanya hivo
penginepo kwa kubashiri kuwa bei ya EURO dhidi ya dola itapanda. K**a inatokea utabiri wake
unakuwa kweli na bei ya EURO kwa dola inapanda na kufika EURO/USD = 1.37 ina maana sasa akiziuza
tena zle EURO 8,130.08 atapata USD(8,130.08?-1.37)= 11,138.21 wakati pesa aliyokuwa nayo
k**a mtaji ni $ 10,000 lakini kutokana na ubshiri wake ameshatengeneza faida ya $ 1,138.21
ambayo itakuwa inaonekana kwenye system za computer.
Hivo ndo namna biashara hiyo kwa wenzetu inavofanyika. Lakini sababu dunia sasa ni kijiji, bishara
hii unaweza kufanya hata kwenye simu yako hiyo ya smartphone. Nimegusia tu kwa hapo maana lengo
langu ni kuzungumzia biashara hii kwa mazingira ya Tanzania na namna unaweza ukatengeneza utajiri.
Watoto wa mjini wanasema pesa ndefu. Ila kwa wale ambao wanataka pia kupata uzoefu na kuifanya
k**a wenzetu walioendelea basi kuna hawa ma FOREX broker unaweza ukawagoogle: FXCM, eTORO,
DUKASCOPY na XM. Hawa ni mabroker wa kuaminika na wote wana mpaka apps za simu kwa hiyo
ukipenda unaweza ukawaangalia na kujifunza.
Jua yafuatayo kwanza
Kabla ya kufanya biashara hii nnayoiita ya ubashiri; ni vema ukawa na uelewa wa kujua ni kitu gani
kinapelekea thamani ya pesa ya nchi inaporomoka ama kupanda dhidi ya fedha ya nchi nyingine.
Ni k**a biashara ya bidhaa nyingine tu, mfano katika kilimo mkulima anaweza kubashiri bei kubwa ya
mazao yake kwa sababu mvua zilikuwa chache na mavuno ni kidogo hivo ujasi wa bidhaa sokoni ukiwa
ni mdogo na mahitaji hayajabadilika ni dhahiri bei itakuwa ni kubwa kwa mazao yake, hivo atakuwa
sahihi kwa ubashiri wake aliofanya kabla.
Vivo hivyo katika biashara ya fedha za kigeni unaweza kubashiri kushuka au kupanda kwa thamani ya
fedha yako dhidi ya fedha nyingine ili kujua kwa usahihi k**a ni wakati muafaka wa kununua ama
kuuza fedha za kigeni.
K**a mwekezaji unatakiwa kujua sababu jumla za kuporomoka ama kupanda kwa thamani ya fedha ya
nchi dhidi ya fedha ya nchi nyingine. Sababu hizo ni k**a zifuatazo na uhusiano wake katika thamani
ya fedha.
i) Mfumuko wa bei (inflation), inflation ikiwa ndogo inaonesha thamani ya pesa ipo juu kwa sababu
pesa inakua na uwezo mkubwa wa kununua kwa sababu bei zipo chini. kinyume chake ni sahihi kwamba
k**a mfumuko wa bei unakua ni mkubwa dhidi ya nchi tunazofanya nazo biashara iki maanisha wao
inflation inabaki kuwa ndogo ina maana lazima pesa yetu ipoteze thamani dhidi ya pesa yao.
Kwa nchi yetu hapa kwa sababu tunatumia sana dollar inamaana kwamba ki nadharia trading partner
wetu ni USA ambao wao inflation yao ipo chini ya 2%. Kwa hiyo ni kwamba kwa vyovyote vile k**a
mfumuko wa bei unapanda ina maana tutegemee kuporomoka kwa thamani ya pesa yetu dhidi ya USD.
Kwa kutumia baadhi ya takwimu utaona ni namna gani mfumuko wa bei kwa kiasi fulani japo yaweza
kuwa kidogo namna inahusika na kuporomoka kwa thamani ya fedha yetu.
Mfumuko wa bei.
Monthly weighted Average $ price
Ukiangalia chati hiyo kwa makini ni kwamba mfumuko wa bei una uhusiano wa moja kwa moja (+) na
kupanda kwa bei ya dola. Japo inawezekana kwamba sio inflation imepelekea hivo lakini uhusiano upo
hata k**a ni kidogo.
Kwa mwekezaji wa FOREX taharifa k**a hizi ni za muhimu na lazima uzielewe kwa haraka mfano bureau
of statistics ikitoa makadirio kuhusu inflation basi itakuwezesha at least kupata picha nini kinaweza
kujiri kwa wajati ujao hivo uweze kufanya ubashiri wako vema.
ii) Nakisi katika biashara, hili wengi tunalifahamu kwamba nchi yetu tunaagiza nje (import) zaidi
kuliko tunavyouza nje (export). Hivo kinachotokea shilingi yetu inapata pressure kubwa kwa sababu
utalii tunaoutegemea utuletee dola ulikua umedorora. Na wakati huo huo tuna import zaidi matokeo
yake ni kwamba too many shillings chasing too little dollars? na kupelekea pressure ambayo
ikapandisha bei ya dola sokoni.
Sasa k**a mwekezaji pindi unapopata taarifa za mwanzo kwamba kwa mfano import zinaongezeka au
utalii umedorora. Moja kwa moja ubashiri wako utakuambia kwamba baada ya kipindi fulani bei ya dola
itapanda. Na k**a ulizinunua kabla basi utakuwa umefaidika. Nchi za ulaya na America k**a import
zinaongezeka masoko huwa yanapata shocks. Kwa sababu wawekezaji wanatenda kutokana na taarifa
wanazosikia.
Kwa hiyo ukiwa mbashiri taarifa ni muhimu sana.
iii) Deni la taifa, hili linasikika kila siku kuhusu mzozo wa madeni wa ugiriki na misukosuko inayoipata
sarafu ya EURO kila kukicha.
Ni kwamba nchi ikiwa na madeni makubwa yatapelekea presha ya mfumuko wa bei kwa sababu serikali
itavutiwa kuprint more money ili kulipa madeni. Kitu ambacho kitaongeza ujazo wa fedha kwenye
mzunguko na utapelekea mfumuko mkubwa wa bei na kushuka kwa thamani ya fedha.
Kwa waliosoma Historia k**a mimi, baada ya WWI Germany aliamriwa kulipa War reparations kwenye
Versailles treaty. Kilichotokea wakati huo Germany iliyokuwa inaongozwa na Weimer iliamua kuprint
money ili iweze kulipa madeni ya war reparations lakini matokeo yake ilipelekea inflation kuwahi
kutokea duniani na mwaka 1923 1USD=4,210,500,000,000 Gr.Marks
Hivyo k**a mbashiri waweza kuangalia kwamba kwa Tanzania deni letu la nchi bado ni kubwa sana kwa
hiyo unaweza ukabashiri kuwa shilingi yetu yawezekana ikaendelea kuporomoka huko mbeleni. Hivo
kwa mfano unaweza kutumia ubashiri wako kununua dola nyingi kwa sasa ili baadae uje kuziuza ghali na
kutengeneza faida.
iv) Performance ya uchumi wa nchi, ukuaji mzuri wa uchumi unaenda sambamba na thamani ya pesa
ya nchi. Nchi k**a Botswana au Rwanda pesa zao zipo imara sana kwa sababu chumi zao zipo stable
na zinavutia uwekezaji kutoka nje ambao pia ni chachu ya kuwa pesa iliyo imara.
K**a mwekezaji kwenye FOREX lazima uwe unajua mwenendo wa uchumi wa nchi unakwendaje. Ili
ufanye ubashiri mzuri huko mbeleni mambo yatakuwaje. Kwa Tanzania hapa itabidi usicheze mbali na
machapisho ya banki kuu ya Tanzania.
v) Amani ya nchi, hili lipo wazi wewe k**a kutakuwa na machafuko ni dhahiri lazima shilingi idorore.
Hivo pia sio mbaya ukabashiri na hali ya nchi kwenye amani itakuwaje. K**a unahisi amani itatoweka
unaweza ukaanza kununua fedha za kigeni nyingi kwa sababu baadae lazima ufaidike.
Sababu hizo hapo juu pamoja na nyingine nyingi ni mambo ambayo k**a unataka kujiingiza kwenye
biashra hii ya FOREX TRADING lazima uyaelewe ili ujue mbeleni mambo yatakuwaje.
Kumbuka biashara hii ni ya kubashiri na kitu cha kubashiri siku zote hatari yake ni kubwa. Hivo k**a
ulikosea kuzisoma alama hizo hapo juu vizuri basi tambua utaangukia katika hasara kubwa.
Kwa ufupi hii pia ni biashara yenye hatari (risk) kubwa mno.
Unatengeneza vipi pesa kupitia FOREX TRADING kwa Tanzania?
Kwa Tanzania na nchi nyingi masikini bado hawajaweza kuwa na mfumo ulio advance kwenye FOREX
TRADING k**a wenzetu wa nchi za magharibi.
Hivo kwa nchi k**a Tanzania FOREX TRADING itakuwa inafanyika physically kwa kutumia Bureau de
change ambazo zipo kwa wingi. Yaani mfano pale unaposoma viashiria vyako ukaona kwa mfano USD,
GBP au EURO zitaenda kupanda, utachofanya ni kwenda kuzinunua na kuzihifadhi. Ukisubiri mda fulani
ufike na zenyewe ziwe zimepanda bei.
Mfano
Katika mfano huu ufuatao nitaonyesha fursa zilizopo kwenye biashara hii kwa kuangalia ni pesa kiasi
gani mtu angetengeneza k**a kwa kutumia viashiria nilivovielezea hapo juu na kufanya ubashiri
angewekeza kununua fedha za kigeni na gold kwa mwaka 2003 na kuziuza kwa mwaka 2013 yaani
baada ya miaka kumi.
Baada ya kuangalia takwimu za kiwango cha kubadilishia fedha kwa miaka kumi iliyopita ambazo
zinatolewa na banki kuu ya Tanzania.
Nilifanya uchambuzi na kugundua tangu mwaka 2002 hadi 2013 kuna bei za feza za kigeni zilipanda
kwa zaidi ya asilimia 100 kwa Tanzania bila kusahau gold ambayo toka mwaka 2003 mpaka 2013
ilipanda bei kwa asilimia 884%.
Kwenye chart ifuatayo nitaorodhesha bei ya kununua kwa mwaka 2002 na bei ya kuuza kwa mwaka
2013 au kwa mwaka2012 kwa fadha za kigeni ambazo ni imara. Nimechagua Japanese YEN, USD,
EURO, GBP, CANADIAN dollar, SWISS FR, south African Rand, New Zealand Kiwi na bila kusahau GOLD
ambayo nayo kwenye FOREX TRADING inahesabika k**a fedha.
Fedha ya kigani
Bei ya kununua unit moja kwa 2002 (TZS)
Bei ya kuuza unit moja kwa mwaka 2013 (TZS)
Ongezeko la bei katika asilimia. %
USD 991.561564.33
57.76
1424.08
2553.62
79.32
EURO
871.28
2073.68
138
YEN JAPAN
7.41
17.16
131.57
SWISS FRANC
595.7[/TD]
1716.41[/TD]
188.13[/TD]
CANADIAN $
622.17
1584.13
154.61
NEW Z. KIWI
434.8
1307.47
200.7
SA RAND
8.67
18.6
114.53
GOLD/OZ
303,317
2,624,440.64
765.24
Ikiangalia hapo kwenye jedwali katika upande wa asilimia hapo ndipo kwenye utajiri. Mfano tu k**a
ulitumia TZS 100,000,000 kwa mwaka 2002 kununua GOLD kwa mwaka 2013 ungekuwa na kiasi cha
(7.65*100,000,000)= TZS 765,000,000 ambayo ni sawa na faida ya TZS 665,000,000 ndani ya
miaka kumi.
Au k**a ungetumia pesa hiyo kununua New Zealand KIWI kwa mwaka 2013 ungekuwa na kiasi cha
(2.007*100,000,000)= TZS 200,700,000 ambayo ni sawa na faida ya TZS 100,700,000.
Waweza tumia mfano wa kiasi chochote cha pesa kwa kuangalia ongezeko la asilimia na kujua kiasi
ambacho kingepatikana baada ya kipindi cha miaka kumi kupitia jedwali letu.
Nimeamua kutumia mfano wa zamani kabisa nikiwa na sababu ya kuonyesha ni jinsi gani uwezo wa
kubashiri ongezeko la bei litavokunufaisha kwa kiasi kikubwa na kwa faida kubwa ambayo huwezi
kuipata kokote kwenye masoko ya fedha.
Hivo k**a mwekezaji katika fedha za kigeni lazima kwanza uwe na jedwali lako k**a hilo na kwa
kutumia vile viashiria nilivovielezea unaweza kumulika hali ya bei hizo kwa miaka ijayo.
Ukiwa katika biashara hii ni suala la lazima kufatilia habari. Kwa mfano k**a ulifanya ubashiri wa
kununua EURO lakini ukiangalia kwamba nchi ya Ugiriki ina hatari ya kuondoka kwenye sarafu hiyo
inamaana kuna wasiwasi wa bei ya EURO kushuka hivo cha kufanya hapo k**a ulikua umenunua EURO
unatakiwa uziuze ili kuepuka hatari ya hasara huko mbeleni.
Hivo ndivo biashara hii inavofanyika suala la habari na taarifa ni muhimu mno na lazima uwe makini
katika maamuzi ya kuuza au kununua kutegemeana na habari unazopata.
Itoshe tu kusema biashara hii mbali na kuwa na faida kubwa pia ina hatari kubwa sana na inahitaji
umakini.
Kwisha kusema hayo nadhani kuna uelewa fulani fulani umepatikana kunusu biashara hii ya fedha za
kigeni (FOREX TRADING) namna inavofanyika kwa nchi za wenzetu na pia fursa zilizopo kwa nchi k**a
Tanzania.
K**a kuna member atakuwa na maswali zaidi basi k**a kawaida JF ni kuacha comment tu na pia k**a
kuna nyongeza yoyote ile ambayo sikuiweka. Maana nimejaribu ku summarize kidogo sababu biashara
hii ni pana sana.
nakala kwa Lenny.
Ni furaha kwangu kwa wale ambao itakuwa imewasaidia.τ€Œ˜τ€Œ˜τ€Œ˜τ€Œ˜τ€‹”τ€‹”τ€‹”
LennyForex Institute:
Our services:
1.Online mentorship /direct for those who are nearby for100$.
2.Forex basics+setups.
3.Price action strategy.
4.Account management: Minimum $300.
Contacts; 0743209386,0674081012, 0718758720 for WhatsApp only.
Broker:

Anyone interested in forex trading?We provide forex course at affordable price of 100$,We provide mentorship through onl...
12/03/2020

Anyone interested in forex trading?
We provide forex course at affordable price of 100$,
We provide mentorship through online platform like ZOOM and direct course please DM FOR MORE CLARIFICATION.
You can check me through whatsapp at +255718758720 or direct call +255674081012 and +255743209386
Also we provide account management services

Ifahamu biashara ya Forex (ubadilishinaji wa fedha za kigeni) biashara inayotrend sasa karibu tubadilishe maisha yetu pamoja. Karibu katika mafunzo kwa gharama ya Tsh 220000/=
Na pia tunatoa huduma ya Account Management kwa waliotayari.

Address

Nyamagana
Mwanza

Telephone

+255743209386

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lenny Forex Institute posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share