Kikundi Cha Upendo

Kikundi Cha Upendo Kusaidia katika changamoto mbalimbali k**a sherehe misiba lakini pia kukwamuana kwa maswala ya kifedha kwa kukopeshana kwa mashariti nafuu

Mwanakiundi wa kikundi cha upendo group akipatiwa pole na viongozi wanaosimamia maafa ndani ya kikundi kwa kuuguliwa na ...
06/11/2021

Mwanakiundi wa kikundi cha upendo group akipatiwa pole na viongozi wanaosimamia maafa ndani ya kikundi kwa kuuguliwa na mtoto wake aliyekuwa amelazwa katika hospital ya mkoa ya seke toure..... # # # UMOJA NI NGUVU.

SOMA  : Mwanajeshi Commandoo nchini Nigeria ameamua kuwasweka ndani Wazazi wake yaani Baba na Mama baada ya kugundua kuw...
22/10/2021

SOMA : Mwanajeshi Commandoo nchini Nigeria ameamua kuwasweka ndani Wazazi wake yaani Baba na Mama baada ya kugundua kuwa Pesa kibao alizokuwa akiwatumia akiwa masomoni nchini Italy kwa ajili ya ujenzi wa nyumba walizifuja.

Mwanajeshi huyo Capt Brian ambaye alikuwa masomoni nchini Italy kwa miaka sita ameeleza kuwa alikuwa akiwatumia pesa za kujikimu na pia kusomesha wadogo zake lakini jambo la kushangaza Wazazi wake hao walikuwa wakimtumia picha feki kuwa ndiyo nyumba yake hadi alipokuja kugundua utapeli huo majuzi aliporejea kutoka masomoni.

Capt Brian aliamua kuwasweka mahabusu Baba na Mama yake na kuamuru kuwa yeyote ambaye angewawekea dhamana basi angekabiliana naye na kwamba baadae atawafungulia mashtaka ambapo endapo watapatikana na hatia wanaweza kwenda jela miaka kumi kwa utapeli huo.

Je unadhani uamuzi wa Capt Brian ni SAWA?

ili tupate maoni ya wengi

 Dah....Hebu angalia macho ya mtoto na alivyong’ang’ania mwili wa mamaye.Bado anaamini mama atatafuta namna ya kumwokoa,...
21/10/2021



Dah....Hebu angalia macho ya mtoto na alivyong’ang’ania mwili wa mamaye.
Bado anaamini mama atatafuta namna ya kumwokoa, kumbe mama hayupo tena.

Kuning’inia kwenye tumbo la mamaye ndiyo usalama wa hali ya juu anaoujua tangu azaliwe. Mara zote wakati mama anaruka kwenye matawi ya miti mikubwa yeye huwa amejishika tumboni kwa mama. Ana imani sana na sehemu hiyo.Ndiyo maana ameamua kwenda “Down With The Ship.”

Kuna kubwa la kujifunza kwenye hili tukio. Nimewaza mengi wakati natafakari hii picha, hasa kwa vile nina watoto wanaonipenda na kunitegemea.

K**a wazazi tujue kuwa watoto wetu wanatutegemea kwa kiwango ambacho maisha yao yanategemea yetu. Baya lolote kwetu, kifo chetu, kuugua kwetu kunayaathiri maisha yao moja kwa moja.

Leo hii unadharau familia yako na kuwajali ZAIDI rafiki zako wa kazini, kwenye vilabu vya pombe na sehemu nyingine za starehe. Familia yako unaipa muda kidogo sana na wala huoni umuhimu mkubwa wa kuwa na familia yako. Mambo mengi unawaza na kuamua KIBINAFSI SANA. Unataka kujifurahisha wewe kwa starehe za muda zisizo salama bila kujali athari zinazoweza kuipata familia kwa maamuzi yako!

Kumbuka, baya lolote kwako litaathiri wanao moja kwa moja. Rafiki na wengine wana maisha yao nje ya wewe, lakini kwa wanao wewe ndiyo kila kitu, k**a unavyomwona mtoto wa Nyani kwenye hii picha, mama yake ndiyo kila kitu. Watoto wako wanaweza kuendelea kuishi bila wewe ila maisha yao yatakuwa yameharibika kabisa. Wao ndiyo watakaoipata “Down With The Ship.”

Tafadhali, ukishakuwa na familia, weka mbele familia yako. Maslahi yao iwe kipaumbele cha kwanza kwako. Wasije wakazama na wewe kwenye majanga unayovuna kwa kuendekeza UBINAFSI na starehe zisizo salama.

Ni kweli, wakati mwingine mambo mabaya hutokea tu na hayakwepeki, lakini ni wajibu wetu kujilinda na kumwomba Mungu atulinde.

Be careful. Wajibika. Jizuie linda familia yako.

Ubarikiwe sana

20/10/2021
20/10/2021

Hatari sana

20/10/2021

Bangi mbaya sana

Address

Mahina
Mwanza
W

Telephone

+255758890361

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kikundi Cha Upendo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kikundi Cha Upendo:

Share