Health Insurance

Health Insurance Health Insurance inahusika na utoaji wa Elimu na matibabu ya changamoto mbalimbali za kiafya kwa kutumia Virutubisho Lishe

*MAUMIVU YA KIUNO NA NYONGA*Maumivu ya kiuno na nyonga (Lumbago) ni hali inayotokea mara nyingi na inayohusu misuli na m...
25/11/2022

*MAUMIVU YA KIUNO NA NYONGA*

Maumivu ya kiuno na nyonga (Lumbago) ni hali inayotokea mara nyingi na inayohusu misuli na mifupa ya upande wa chini wa mgongo. Hali hii huathiri takriban 40% ya watu kwa wakati fulani maishani mwao.

*SABABU ZINAZOPELEKEA MAUMIVU YA KIUNO NA NYONGA* (mifupa kwa ujumla)

👉🏻kujichua muda mrefu hupelekea maumivu hayo.
👉🏻Namna ya kulala (style) /godoro linaweza kukusababishia maumivu hayo
👉🏻Kubeba mizigo kwa kuinama na mzigo,
👉🏻mawazo (stress) nyingi
👉🏻kulala kwa muda mrefu na matumizi mabaya ya MTO
👉🏻kuteguka au mkazo wa misuli.
👉🏻Unene wa kupindukia
👉🏻 kuvuta sigara
👉🏻kunenepa wakati wa ujauzito
👉🏻mfadhaiko
👉🏻matatizo ya mwili
👉🏻mkao mbaya na kulala vibaya pia huchangia maumivu ya mgongo.

✍🏻Wanawake wanaweza kuwa na maumivu ya kiuno kutokana na hali zinazoathiri mfumo wa uzazi k**a;
👉🏻Matatizo ya hedhi
👉🏻uvimbe kwenye mayai
👉🏻saratani ya ovari au fibroidi ya uterasi.
👉🏻Matatizo ya kimwili yanaweza kuwa osteoathritisi,
👉🏻 Ugongonjwa wa baridi yabisi (arthritis rheumatoid)
👉🏻kuharibika kwa diski zilizo katikati mwa pingili za uti wa mgongo
👉🏻kuvunjika kwa pingili za uti wa mgongo (k**a vile kufuatia osteoporosisi)
👉🏻maambukizi au tyuma ya uti wa mgongo.

*MADHARA YA MAUMIVU YA NYONGA NA KIUNO*
👉🏻Hupelekea kushindwa kufanya tendo la ndoa
👉🏻Hupelekea kupooza kwa baadhi ya viungo vya mwili
👉🏻Hupelekea kuwahi kufika kileleni mapema wakati wa tendo na kushindwa kurudia
👉🏻Unaweza kushindwa kutembea kabisa /kunyanyuka, utakaa ukiwa umelala.

*ANGALIZO :*

👉🏻Kuna sababu nyingi zinazopelekea maumivu ya nyonga na baadhi ya sababu hizi huashiria magonjwa hatari ni Vyema Ukafahamu Kwanza Chanzo Cha tatizo Kabla ya Matibabu.

✍🏻TATIZO HILI LINATIBIKA KUTOKANA NA CHANZO CHA TATIZO

✍🏻Kupata tiba tuwasiliane

Ahsante
MAWASILIANO
0710705676

Napokea messages nyingi Sanaa kutoka Kwa kina dada kuwa siku hizi kupata mtoto ni Changamoto kwao, lakini hawajui nini C...
27/07/2022

Napokea messages nyingi Sanaa kutoka Kwa kina dada kuwa siku hizi kupata mtoto ni Changamoto kwao, lakini hawajui nini Chanzo Cha wao kuwa katika Hali hiyo inayowaletea utata mkubwa Sanaa katika Ndoa zao.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini mwanamke, Binti au dada huyo hawezi kubeba ujauzito:
🕳️Kuugua baadhi ya magonjwa ya zinaa yanayopelekea kupata vimbe mbali mbali katika mfumo mzima wa Uzazi k**a vile PID, fibroids na zingnezo
🕳️Kukosa uwiano sawa wa homoni za k**e ni mojawapo ya viashalia vya huyu mwanamke kutokuweza kubeba mimba.
🕳️Kukosa Ute wa Uzazi nyakati za hatari au nyakati ambazo yai limekwisha kupevuka linahitaji kurutubishwa, hii hutokana na baadhi ya njia za uzazi wa mpango k**a sindano vidonge Nk
🕳️Kutokuwa na mzunguko unaoeleweka Kwa mwanamke, hii huchangia asilimia kubwa sanaaa maana Kuna siku maalum TU za mimba kuingia katika mzunguko wa mwanamke kwahy k**a mzunguko haueleweki itapelekea kutoshika mimba
🕳️Kuziba Kwa mirija ya uzazi, hii nayo huchangia dada kutokuweza kutimiza lengo lake la kupakata mtoto inaweza kuwa imevimba au imejaa maji na kupelekea mayai kushindwa kufika sehem ya tumbo Ili kurutubishwa na mbegu za kiume
🕳️Wengine chango la uzazi hupelekea wasipate mimba, pamoja na adha nyinginezo chango hufanya mimba kutokutungika
🕳️Zipo sababu zingine k**a vile kutoa mimba mara Kwa mara, kuwa na Msongo wa mawazo, uzito kuwa mkubwa sanaaa nayo ni sababu inachangia kukosa mtoto.

Kwa ushauri, maoni na maswali wasiliana nasi Whatsapp no 0710705676
Health Insurance
Office zipo:Moro, dar, Dodoma na Mbeya

MADHARA YA KUTOONDOA SUMU KATIKA MWILI(DETOXIFICATION PROGRAM) Asilimia kubwa ya maradhi yanayowasumbua watu hivi leo ya...
02/07/2022

MADHARA YA KUTOONDOA SUMU KATIKA MWILI

(DETOXIFICATION PROGRAM)



Asilimia kubwa ya maradhi yanayowasumbua watu hivi leo yanatokana na sumu zilizopo katika miili yao. Inawezekana umewahi kusikia mambo mengi kuhusu sumu kwenye mwili, lakini hufahamu chazo halisi cha sumu hizi.



VYANZO VYA SUMU

Miili yetu imekuwa ikipokea sumu na uchafu kila siku kutokana ;

1. Matumizi ya dawa mara kwa mara

2. Matumizi ya pombe (Alcohol) na sigara

3. Mazingira na athari kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia

4. Ukosekanaji wa lishe sahihi na diet nzuri

5.Matumizi ya madawa makali

6.Uzito mkubwa

7.Mitindo ya maisha

8.Njia za uzazi wa mpango za kisasa



DALILI ZA KUWA SUMU NYINGI MWILINI

1.Matatizo ya ngozi kwa mfano chunusi,vipele

2.kuwa na uzito wa kupindukia

3.kutokupata choo au choo kigumu

4.kukosa usingizi Na kujihis kuchokachoka

5.Kiichwa kuuma

6.Kupata miwasho

7.Maumivu ya viungo K**a vile mgongo,goti

8.kuwa na hasira mara kwa mara.

9.Tumbo kujaa gesi







MADHARA YAKE

1.kuondoa hamu ya tendo la ndoa

2.maumbikizi ya figo

3.Maumbikizi ya Ini

4.Hupelekea matatizo ya kutopata watoto (ugumba)

5.hupelekea uvimbe kwa ndani ya kizazi kwa mwanamke

6.Hupelekea matatizo ya pressure

7.Mvurugiko wa homoni



SULUHISHO LA KUDUMU



Kwa watu wenye changamoto hizo kampuni tumewaandalia program ya lishe kamili na virutubisho muhimu. Bidhaa hizi ni vyakula, siyo dawa wala mitishamba.

Faida ya Kutumia kinywaji hiki;



• Huondoa sumu na uchafu katika Mwili .



•Huongeza Kinga ya Mwili kwa asilimia kubwa sana



•Husaidia kubalance presha



•Husaidia kubalance kiwango cha sukari katika Mwili.



•Hudhibiti virusi Na bacteria



•Huondoa uvimbe wa ndani Na nje.



•Husaidia katika kurekebisha mfumo wa mmengenyo wa Chakula.



•Husaidia katika kuondoa matatizo ya upataji choo kigumu au mtu anayekosa choo.



•Husaidia katika kuimarisha mfumo wa mzunguko wa damu na upumuaji katika Mwili.



• Husaidia katika kuimarisha mfumo wa uzazi kwa mwanaume na mwanamke pale atakapoitumia na Bidhaa zetu nyingine.



• Husaidia kuongeza virutubisho na kuupa Mwili afya na kulainisha Ngozi na kuifanya Ngozi kuwa ng'avu na laini.



•Huondoa uchovu Na kuupa nguvu.



Kwa yeyote anayehitaji hii program ya kuboresha na kuimarisha afya yake.

Kwa maeelezo zaidi au ushauri Zaidi piga simu nitafute inbox

16/01/2022

CHANZO CHA MAGONJWA YA MOYO

✍🏻Magonjwa ya moyo hutokea pale ambapo moyo huathiriwa na kuharibiwa kwa vitenda kazi vyake. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata magonjwa ya moyo nayo ni pamoja na;

👉🏿Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P)
Kuvuta sigala
👉🏿Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
👉🏿Kisukari
Kukaa sehemu kwa mda mrefu bila kuufanyisha kazi mwili
👉🏿Umri
👉🏿Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
👉🏿Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
👉🏿Historia magonjwa yanayoambatana na moyo katika familiaAINA ZA MAGONJWA YA MOYO

✍🏻Zipo aina mbalimbali za magonjwa ya moyo hutofautiana japo yote huathiri moyo, nayo ni;

1️⃣Ugonjwa wa moyo unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu (Coronary artery disease)

Hili ni tatizo linalowakuta watu wengi, mishipa ya damu hupasuka na kuharibika hii hutokana na mishipa ya damu kuwa na uchafu na mafuta mengi na kufanya damu isipite vizuri

2️⃣Mapigo ya moyo kwenda tofauti (Heart Arrhythmias)

Hii hutokea pale mapigo ya moyo kwenda taratibu isivyo kawaida au kwenda haraka isivyo kawaisda, pia mapigo ya moyo kwenda ovyo. Hii ni hatari sana na huua sana

3️⃣Moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure)

Hii ni hali moyo hushindwa kufanya kazi yake k**a kupampu na kusambaza damu, kusambaza oxygen. Hii inaweza kutokea kwa mtu mwenye magonjwa k**a ugonjwa wa moyo wa misipa kuathirika, Shinikizo la damu, na magonjwa mengine

4️⃣Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital heart disease)

Haya ni magonjwa ambayo wengi huzaliwa nayo, yanaweza kuwa ni baadhi ya kasoro katika mwili k**a baadhi ya chemba za moyo kuziba au kupasuka, oxygen kupita kwa shida na vinginevyo.
5️⃣Ugonjwa wa valvu na misuli ya moyo (Heart Valve Disease & Cardiomyopathy (Heart Muscle Disease))

Katika moyo kuna chema nne nazo zinapitisha damu na oxygen kutoka kwenye mapafu, valvu hufunguka na kufunga. Valvu na misuli ikiwa imepasuka na kuharibika husababisha tatizo la moyo.

6️⃣Moyo kutanuka.

Hii hutokea pale damu ikiingia ndani ya moyo harafu mishipa ya kutoa damu ikiwa na tatizo ikashindwa kutoa damu nje ya moyo moyo utaanza kutanuka siku hadi siku. Kutanuka kwa moyo kunatokea usipotibu baadhi ya matatizo k**a shinikizo la damu, moyo kwenda mbio, valvu na misuli ya moyo n.k.

7️⃣Shinikizo la damu (B.P) ni shinikizo la damu yako kwenye kuta za mishipa yako kwani moyo wako unasukuma karibu na mwili wako. Unaweza kuwa na shinikizo la damu (shinikizo la damu) kwa miaka bila dalili yoyote.

8️⃣Mshtuko/ Shambulio la moyo (Heart Attack).

Ni kifo cha sehemu ya misuli ya moyo inayosababishwa na kuzuiwa wa usambazaji wa damu. Amana zilizo na mafuta huunda kwa wakati, na kutengeneza alama katika mishipa ya moyo wakoIkiwa baadhi ya misuli ya moyo inakufa, mtu hupata maumivu ya kifua na kukosekana kwa umeme kwa tishu za misuli ya moyo.

9️⃣Chembe ya Moyo.

Hii ni maumivu ya upande wa moyo maeneo ya kifua hutokea wakati unafanya kazi au hata k**a umekaa k**a ni yenye kukubuhu. Maumivu haya huambatana na kutokwa jasho na kukosa hewa. Hutokana na moyo kukosa damu ya kutosha.

UJUE UGONJWA WA SARATAN YA SHINGO YA KIZAZISaratani ya mlango wa kizazi ni aina ya saratani inayoshambulia seli/chembech...
12/12/2021

UJUE UGONJWA WA SARATAN YA SHINGO YA KIZAZI
Saratani ya mlango wa kizazi ni aina ya saratani inayoshambulia seli/chembechembe zilizomo ndani ya ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi.

CHANZO & SABABU ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Wanawake wengi wanaopata ugonjwa huu huwa na kisababishi kimoja au zaidi kinachojulikana ambacho huongeza hatari ya kuupata. Vifuatavyo ni visababishi vikuu:

1.Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 16)
2.Kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja
3.Maambukizo ya virusi vya HPV (Human papilloma virus)
4.Maambukizo ya magonjwa ya zinaa
5.Umri zaidi ya miaka 30
6.Upungufu wa kinga mwilini (VVU/UKIMWI)
7.Uvutaji wa sigara
8.Kupata mimba katika umri mdogo
9.Idadi kubwa ya watoto na kuzaa mara kwa mara
10.Hali duni ya kiuchumi
11.Kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye mkewe alikufa kwa saratani ya shingo ya kizazi
12.Kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye hajatahiriwa
Historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia

DALILI NA VIASHIRIA VYA KUWA NA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.

1.Kutokwa na damu katika tupu ya mwanamke (va**na) ambayo sio ya kawaida. 2.Damu hii inaweza kuwa matone, au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi kabla ya hedhi inayofuata) au damu itokayo kwa mwanamke ambae ameacha kupata hedhi.
3.Kutokwa na damu baada ya kujamiana baada ya tendo la ndoa.
Maumivu wakati wa kujamiana.

Dalili za saratani iliyosambaa ni k**a zifuatavyo

🕳️Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida yenye harufu na maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
🕳️Kupungua kwa hamu ya kula
🕳️Kupungua uzito
🕳️Kuhisi uchovu
🕳️Maumivu ya nyonga
🕳️Maumivu kwenye mgongo
🕳️Maumivu ya mguu
🕳️Mguu mmoja kuvimba
🕳️Kutokwa na damu nyingi kwenye tupu ya mwanamke
🕳️Kuvunjika mifupa (bone fractures)
🕳️Kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye tupu ya mbele ya mwanamke.

MAUMIVU YA NYONGA NI NINI?Kwa ujumla hakuna njia moja inayoweza kuelezea maumivu haya, ni maumivu yanayotokea sehemu kat...
27/11/2021

MAUMIVU YA NYONGA NI NINI?
Kwa ujumla hakuna njia moja inayoweza kuelezea maumivu haya, ni maumivu yanayotokea sehemu katikati ya tumbo na eneo la hips. Baadhi ya watu maumivu yanaweza kuanzia kwenye eneo la chini ya mgongo na kusambaa hadi kwenye eneo la nyonga.

Kwa upande wa mwanamke maumivu yanaweza kutokana na shida kwenye uzazi sababu mfumo wa uzazi wa mwanamke upo kwenye nyonga. Maumivu haya ya nyonga yanaweza kumpata mwanamke, mwanaume na hata watoto pia.

DALILI YA MAUMIVU YA NYONGA
Maumivu ya nyonga siyo ugonjwa bali ni dalili ya uwepo wa tatizo la kiafya. Maumivu haya yanaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu na hutokea kweye nyonga na chini ya tumbo.

Dalili za maumivu ya nyonga hutofautiana kwa wagonjwa. Wengine hupata maumivu mepesi na wengine hupata maumivu makali. Kwa baadhi ya watu maumivu huweza kuwa makali hadi kupelekea kukwamisha shughuli za kimaisha k**a mazoezi, kutembea na tendo la ndoa. Kwa ujumla maumivu ya nyonga huambatana na matatizo mengine k**a kushindwa kufanya tendo la ndoa
NINI KINASABABISHA MAUMIVU YA NYONGA?
Kuna sababu nyingi zinazopelekea maumivu ya nyonga kwa wanawake na wanaume. Inaweza kuwa ni maambukizi, ama athari kwenye viungo vya ndani k**a kibofu cha mkojo, utumbo mpana, kwa wanawake yaweza kuwa ni shida kwenye uzazi. Hapa chini ni maelezo sababu kuu zinazopelekea maumivu ya nyonga.

🕳️Constipation
Kukosa choo ama kupata choo kigumu kwa muda mrefu husababisha maumivu ya nyonga kutokana na presha na kujaa gesi kwa tumbo. Constipation yaweza kusababishwa na lishe mbaya, msongo wa mawazo, matatizo ya homoni, upungufu wa madini ya magnesium, kupungua kwa bakteria wazuri tumboni na kutoshugulisha mwili.

Kwa kutumia package yetu ya digestive care unaweza kupona tatizo lako la constipation na kuimarisha afya ya tumbo.

🕳️Matatizo ya kibofu cha mkojo
Kibofu kinapopata hitilafu hupelekea kuvimba kwa tishu zake na kusababisha maumivu kwenye eneo la nyonga. Ugonjwa wa kibofu uitwao interstitial cystitis, ambao huletekeza dalili za UTI ni moja ya matatizo yanayosababisha maumivu ya nyonga.

🕳️Matatizo ya figo
Matatizo k**a maambukizi kwenye figo au mawe kwenye figo husababisha maumivu ya nyonga. Tatizo la mawe kwenye figo husababisha maumivu ya chini ya mgongo ambayo husambaa mpaka kwenye eneo la nyonga.

🕳️Hernia au ngiri
Hernia/ngiri hutokana na kutofunga kwa eneo la chini ya tumbo na kupelekea kukua kwa tishu kukua kuelekea eneo la uzazi. Ngiri husababisha maumivu makali ya nyonga.

MAUMIVU YA NYONGA KWA MWANAMKE
Maumivu ya nyonga kwa wanawake yanaweza na shida kwenye uzazi. Matatizo haya yanaweza kutokea kwenye viungo k**a uke, shingo ya kizazi, kuziba mirija ya uzazi, mifuko ya mayai au mfuko wa mimba. Inawezekana pia kupata maumivu kutokana na sababu zaidi ya moja, sababu hizi zinaweza kuwa:

1. Endometriosis
Endometriosis ni kitendo cha kukua kwa ukuta wa ndani(endometrium) wa mfuko wa mimba kuelekea nje ya mfuko wa mimba. Pale tishu zinapokua na kuwa nene husababisha dalili k**a maumivu ya nyonga, maumivu kipindi cha hedhi, tumbo kujaa gesi na maumivu ya chini ya mgongo.

2. Fibroids
Fibroids ni uvimbe usio saratani unaotokea ndani ya kuta za mfuko wa mimba. Tafiti zinasema kwamba karibu asilimia 40 mapaka 80 ya wanawake hupata shida ya fibroids katika uzazi kwenye maisha yao.

3. PID
Pid ni maambukizi kwenye njia ya uzazi ambayo kwa kiasi kikubwa husababishwa na magonjwa ya ngono k**a chlamydia au gonorrhea. Dalili kubwa ni maumivu ya nyonga, maumivu wa wa tendo ndoa, maumivu wakati wa kukojoa, na kutokwa na uchafu ukeni kusiko kawaida.

4. Ovarian cysts
Ovarian cysts ni mkusanyiko kwa vimbe ndogo ndogo zilizojaa maji kwenye mifuko ya mayai ya mwanamke. Kwa wanawake wengi vimbe hizi hazileti shida na huweza kupotea baada ya muda. Lakini kwa baadhi ya wanawake vimbe zinapokuwa kubwa huleta maumivu ya nyonga na kuvurugika kwa hedhi.

5. Kutoa mimba
Dalili kubwa zinazotokea baada ya kutoa mimba ni k**a kutokwa na uchafu ukeni usio kawaida, maumivu ya chini ya tumbo, maumivu ya nyonga, kuharisha na wakati mwingine kuzirahi kutokana na kutokwa na damu nyingi.

6. Maumivu kipindi cha hedhi
Baadhi ya wanawake hupata maumivu ya nyonga wakati wa hedhi, maumivu haya huitwa dysmenorrhea kwa kitaalamu. Maumivu kipindi cha hedhi ni kutokana na kutanuka kwa misuli ya mfuko wa mimba.

MAUMIVU YA NYONGA KWA MWANAUME
Ukiacha wanawake, wanaume pia hupata tatizo hili la maumivu ya nyonga, hasa wenye tatizo la tezi dume. Kuvimba kwa tezi dume ama maambukizi kwenye tezi dume husababisha maumivu ya nyonga, eneo la haja kubwa, kwenye tumbo la chini na pia maumivu kwenye kibofu.

Dalili zingine zinazoonesha kuna shida kwenye tezi dume ni kupata maumivu wakati wa kukojoa ama kupata mkojo kidogo sana . Unapoona dalili hizi wahi hospitali mapema ili kupata vipimo na tiba haraka.

11/11/2021

TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE/VAGINAL ITCHING:
Kwa kawaida kuwashwa sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi au maambukizi mengine ya bacteria katika sehemu husika.Wakati mwingine mzio(allergy) pia inaweza kusababisha muwasho katika sehemu za siri.
-Muwasho maeneo ya ndani ya uke au kwenye mashavu ya uke husababishwa na mambo mengi. Muwasho ndani ya uke (va**na) unaweza kutokana na;
1.Matumizi ya kemikali au sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria ( detergents or medicated soaps),
2.Kwa kuosha ndani ya uke kwa sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu tunasema va**nal douching) na kitendo hiki hupelekea kuua bakteria wanaoishi kwenye uke (normal flora) kwa ajili ya kuulinda,
3.Kwa kutumia cream au manukato kwenye uke,
4.Kwa kutumia sabuni za bafuni(bath products)kwa kunawia maeneo hayo nyeti.
5. Wanawake ambao wameacha kuingia kwenye hedhi wanaweza kupata mwasho kutokana na kubadilika kwa kiwango cha homoni ya Oestrogen. Kwa kipindi hiki kuta za uke huwa nyembamba na kukauka na hivyo kupelekea kupata miwasho.

NAMNA GANI TUNAWEZA KUZUIA MWASHO SEHEMU ZA SIRI?
Wanawake wanatakiwa kuchukua hatua zifuatazo kuzuia mwasho sehemu za siri:
1.Namna ya kujitawaza baada ya haja ndogo au kubwa: Wanawake wanashauriwa kujitawaza kutokea mbele kuelekea nyuma ili kuzuia bakteria wa kwenye njia ya haja kubwa(anus) kuingia kwenye uke (va**na)
2.Kuzuia matumizi ya kemikali au sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria (detergents or soaps), kuosha ndani ya uke kwa sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu va**nal douching), kutumia cream kwenye uke, karatasi za chooni (toilet papers) na sabuni za bafuni (bath products)
3.Kuhakikisha sehemu za siri ni kavu baada ya kujisaidia au kuoga.
4.Kutokuvaa nguo za ndani ambazo hazibani sana (Wear loose natural fiber underwear and clothing)
5.Hakikisha sehemu za siri ni safi na kavu wakati wote,
6.Zuia kukaa na nguo zenye unyevunyevu kwa muda mrefu, 7.Jiepushe kufanya ngono zembe.
8.Tumia pedi bora zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu(anion chip technology) ili kujikinga na kujiepusha na miwasho na michubuko sehemu za siri pamoja na UTI.(Machukizo mbalimbali wakati wa hedhi)

0710705676

Chunusi Zinasababishwa Na Nini?Chunusi ni ugonjwa gani?Chunusi ni tatizo la ngozi linalotokea wakati vinyweleo vinapozib...
10/11/2021

Chunusi Zinasababishwa Na Nini?
Chunusi ni ugonjwa gani?
Chunusi ni tatizo la ngozi linalotokea wakati vinyweleo vinapozibwa na mafuta pamoja na seli za ngozi zilizokufa.

Kwa kawaida chunusi hutokea usoni, kifuani, mabegani na mgongoni.

Chunusi hutokea zaidi kwenye umri wa kubalehe, ingawa inaathiri watu wa rika lolote.

Chunusi huwaathiri takribani asilimia 80% ya watu wenye umri kati ya miaka 11-30.

Kuna aina mbalimbali za matibabu ya chunusi, aina mbalimbali za dawa ya chunusi na njia mbalimbali za jinsi ya kuondoa chunusi.

Kulingana na ukubwa wa tatizo, chunusi inaweza kusababisha kutokujiamini na kuleta msongo wa mawazo.

Chunusi zisipotibiwa mapema zinaweza kusababisha madoa na makovu ya chunusi.

Chunusi husababishwa na nini?
Kuna sababu kuu nne zinazosababisha chunusi kutokea:

1. Kuzalishwa mafuta kwa wingi
2. Vinywelea kuzibwa na mafuta na ngozi iliyokufa
3. Bakteria
4. Kuzidi kwa homoni k**a vile Androgen

Chunusi kwa kawaida hutokea usoni, kifuani, mgongoni na kwenye mabega, na hii ni kwa sababu katika sehemu hizi ngozi ina mafuta mengi.

Mafuta haya, pamoja na seli za ngozi zilizokufa huziba vijitundu vya vinyweleo, na kusababisha mafuta kujirundika ndani ya ngozi.

Na hapo ndipo bacteria nao huingia hapo na kutengeneza aina ya usaha unaotoka kwenye chunusi.

Sababu zinazochochea chunusi kutokea au kuongezeka
1. Homoni. Androgen ni homoni zinazoongezeka kwa wavulana na wasichana wakati wa kubalehe kupelekea vijifuko vya kuzalisha mafuta kukua na kuongezeka, na hivyo kuzalisha mafuta mengi kwenye ngozi. Pia mabadiliko ya homoni hutokea wakati wa ujauzito na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango na hivyo kusababisha chunusi
2. Dawa. Dawa k**a steroids, testosterone
3. Vyakula. Tafiti zinaonyesha kuwa vyakula vya wanga k**a mkate, chips, pia chokoleti huongeza makali ya chunusi
4. Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo huchochea tatizo la chunusi kutokea au kuongezeka
5. Mazingira yenye mafuta. Mazingira k**a ya jikoni yanaweza kuchochea tatizo la chunusi kuongezeka
6. Vipodozi. Vipodozi vyenye mafuta mengi vinaweza kusababisha chunusi kutokea
7. Historia katika familia. K**a wazazi wana tatizo la chunusi, kuna uwezekano mkubwa wa mtoto pia kupata

Jinsi ya kuondoa Chunusi
Zifuatazo ni njia zinazosaidia kuondoa tatizo la chunusi
1. Osha uso wako mara mbili kwa siku ili kuondoa uchafu na mafuta kutoka kwenye ngozi
2. Usifanye “harsh scrub”, itasababisha ngozi kuwa “irritated” na kufanya tatizo la chunusi kuwa kubwa zaidi
3. Tunza nywele zako katika hali ya usafi, maana mafuta ya nywele yakifika usoni yanaweza kusababisha chunusi
4. Jihadhari na kutumbua chunusi, hii inasababisha uvimbe na makovu
5. Tumia dawa k**a unavyoshauriwa na wataalam
6. Pata ushauri wa Daktari kuhusu kutumia antibiotic inapobidi ili kuzuia kupambana na bacteria wanaochochea chunusi
7. Punguza kula vyakula vinavyohusishwa na chunusi. Vyakula hivyo ni k**a vya wanga, vilivyowekwa sukari, chokoleti, vya mafuta, n.k. Ongeza kula matunda na mboga za majani
8. Tumia “sunscreen” unapokuwa juani, kupigwa na jua kunachangia kuongeza mafuta kwenye ngozi
9. Tafuta huduma ya kitaalam kwenye “aesthetic clinic”. Huduma k**a vile Facial, LED light, Salicylic Acid, Laser, Microneedling, Derma roller, n.k
10. Usitumie vipodozi vyenye mafuta, vinaweza kusababisha kuziba kwa vitundu vya ngozi
11. Usitumie vipodozi vyenye mafuta, vinaweza kusababisha kuziba kwa vitundu vya ngozi
12. Punguza msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi, kufanya vitu unavyopendelea,
kutembelea maeneo ya kuvutia, kuongea na watu uwapendao, n.k
13. Tunza vifaa unavyotumia kusafisha uso katika hali ya usafi wakati wote

0710705676 kwa ushaur na namna ya kupata matibabu

FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST )Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (o***y) hutokana na mkus...
01/11/2021

FAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (OVARIAN CYST )

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (o***y) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana k**a ovarian cyst.
Uvimbe huu unaweza kumtokea mwanamke wa umri wowote ingawa mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito.

MAYAI YA MWANAMKE
Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus).
Mayai haya huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana k**a o**m ambapo mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (o***y) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.
Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, saa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya Luteinizing Hormone kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa katika kila ovari na hii ndio hujulikana k**a ovulation au upevukaji mayai. Mayai haya ya uzazi huishi kwa saa chache hadi saa 24 ikiwa hayatorutubishwa na mbegu za kiume.
Mabaki ya mfuko wa mayai ya uzazi yanayojulikana k**a follicle ndani ya ovari, hugeuka na kuwa corpus luteum ambao huhusika na utoaji wa kichocheo au homoni aina ya progesterone kwa wingi.
Homoni hii ya progesterone ndio inayosababisha mfuko wa uzazi kujiandaa kwa kujikita yai (implantation) lililorutubishwa kwa mbegu ya kiume ndani ya mfuko wa uzazi kwa kuongeza unene kwenye kuta zake. Yai hili husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ambako hukua na kuwa mtoto. K**a upachikwaji wa yai liliorutubishwa hautafanyika, basi ndani ya wiki mbili, corpus luteum huanza kusinyaa na kupotea na kusababisha kushuka kwa kiwango cha homoni aina ya progesterone na estrogen.
Kushuka kwa kiwango cha vichocheo hivi ndio husababisha mfuko wa uzazi kuanza kutoa mabaki ya kuta zake pamoja na yai la uzazi na ndipo pale mwanamke anapoanza kuona siku zake za hedhi(kutokwa na damu ukeni).

UVIMBE KWENYE MAYAI.
Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke ila aina hizi saba ndio huonekana sana kwa wanawake wengi.

1~ Aina ya kwanza ni Follicular cyst ambayo uvimbe hutokea wakati ovulation isipotokea au baada ya corpus luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi.
Uvimbe huu unakuwa na wastani wa inchi 2.3 kwa upana. Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya ovulation.
Kwa kawaida uvimbe huu hauna dalili zozote na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa.

2~Aina ya pili ni Corpus Luteum cyst- ambao ni uvimbe unaosababishwa na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi. Kwa kawaida corpus luteum husinyaa na kupotea yenyewe, au wakati mwengine inaweza ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe.
Uvimbe huu huonekana kwenye upande mmoja (kushoto au kulia) wa mwanamke na hauna dalili zozote zile.

3~Uvimbe wa tatu ni Hemorrhagic cyst- Uvimbe huu hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa aina yoyote ule ambao umeshajitengeneza tayari. Huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu wa mwanamke.

4~Uvimbe mwingine ni Dermoid cyst- ambao sio saratani na pia hujulikana k**a mature cystic teratoma, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika mimba na huweza kukua na kufikia inchi 6 kwa upana na ndani huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mfupa, mafuta na cartilage.
Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa zaidi au kujizungusha na hivyo kuathiri usambazaji wa damu kwenda kwenye uvimbe huu na hivyo kusababisha maumivu makali sana maeneo ya tumboni.

5~Aina nyingine ni Polycysitic appearing cyst- ambao unakuwa mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijivimbe vingine vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni.

6~Aina ya sita ya uvimbe ni Cystedenoma-Ni aina ya uvimbe unaotokana kwenye tishu za ovari na hujazwa na majimaji yenye kuvutika. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa sana hata kufikia inchi 12 au zaidi kwa upana.
7~Aina ya mwisho ya uvimbe unaowapata wanawake ni Endometriomas /Endometrial.

SABABU ZA UVIMBE.
Vihatarishi vya tatizo la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke nipamoja na
historia ya awali ya ovarian cyst. Kwa wanawake ambao wazazi wao au watu wao wa karibu wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kuna uwezekano mkubwa nao wakapatwa na tatizo hilo.
Sababu nyingine inayoweza kusababisha uvimbe katika mayai ya mwanamke ni kuwa na mzunguko wa hedhi usiokuwa na mpangilio maalum. Kihatarishi kingine ni kuwa na mafuta mengi kwenye sehemu ya juu ya mwili na hii ni kwa wale wanawake wanene.
Ugumba na kuvunja ungo mapema ni sababu nyingine ambapo mtoto wa k**e hasa anayevunja ungo akiwa na miaka 11 au chini ya hapo huweza kupatwa na uvimbe katika mayai yake.

DALILI;
Maumivu makali, ambayo hayana mwanzo maalum na yanayochoma, ambapo maumivu hayo yanaweza yakawa yanakuja na kupotea au yakawepo moja kwa moja.
Kuhisi tumbo kuwa zito, kujaa au kuvimba, maumivu kwenye matiti na hedhi isiyokuwa na mpangilio maalum, maumivu ya muda mrefu kwenye nyonga wakati wa hedhi na ambayo huweza kuhisiwa sehemu ya chini mgongoni. Maumivu haya yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi.
Maumivu ya nyonga baada ya kufanya kazi ngumu, mazoezi au baada ya kukutana kimwili, kuhisi kichefuchefu, kutapika na kutokwa na matone ya damu ukeni. Dalili nyingine ni ugumba na kuhisi uchovu, mabadiliko ya haja ndogo yaani kukojoa mara kwa mara, kujikojolea au kushindwa kutoa mkojo wote kutoka kwenye kibofu cha mkojo wakati wa kupata haja ndogo.

VIPIMO
Mgonjwa kufanyiwa Endova**nal Ultrasound ambayo hufanywa kwa kuingiza mpira maalum kupitia ukeni na kuangalia mfuko wa uzazi na mayai ya mwanamke. Kwa kutumia kipimo hiki, ni rahisi kwa daktari kugundua k**a uvimbe kwenye mayai ni wa aina gani na kujua k**a ni maji tu (fluid filled sac), au ni maji pamoja na mchanganyiko wa vitu vigumu kwa maana ya complex, au ni vitu vigumu pekee ambapo huitwa completely solid

Kumbuka uvimbe huu sio kansa hivyo ondoa hofu. Mbali na donazole ambayo ni ya gharama na haishauliwi itumiwe kwa mda mrefu ina sababisha mwanamke anakua na sifa za kiume.UKIFANYIWA OPERATION USIDHANI UVIMBE UMEISHA UNAOTA PEMBENI HADI UTAKAPOWEKA VICHOCHEO SAWA.
Sasa suluhisho lako lipo tuna dawa ambao imetengenezwa kitalamu katika mfumo wa vidonge na vimetengenezwa kwa mimea baada ya utafiti na majaribio ya kutosha na viwanda vya madawa vikubwa hapa duniani.
Utapata suluhisho lako bila madhara kwani ni mimea 100%.
Hii dawa inapunguza uvimbe wa fibroid bila madhara k**a donazol. K**a una ndugu au rafiki mwambie suluhisho lipo na mshirikishe kuokoa afya yake.
Kwa maoni na ushauri na tiba tuandikie kwa namba
0710705676

CHANGO LA UZAZI NA TIBA YAKE.  la uzazi ni matatizo yaliyopo katika viungo vya uzazi kwa mke au mume. Huu ni ugonjwa amb...
27/10/2021

CHANGO LA UZAZI NA TIBA YAKE.

la uzazi ni matatizo yaliyopo katika viungo vya uzazi kwa mke au mume. Huu ni ugonjwa ambao humpata mtu katika umri mdogo utotoni.

Kwa mfano :- *mume, hupata maumivu ya tumbo mara kwa kunzia anapokuwa mdogo.

Kwa upande wa *mwanamke hupata maumivu ya tumbo anapoanza kuvunja ungo.*

hayo hupelekea mtu (mume/mwanamke) kupata madhara katika viungo vyake vya uzazi.

ZA CHANGO LA UZAZA KWA MWANAUME

🌱Kuwahi kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa
🌱Kushindwa kurudia tendo la ndoa
🌱Dhakari kuwa legelege na kushindwa kusimama vizuri

YA CHANGO LA UZAZI KWA MWANAMUME.

🍁Kuwa na mbegu ambazo haziwezi kutunga mimba
🍁Kiwango kinachozalishwa cha mbegu ni kidogo mno
🍁Kukosa hamu ya tendo la ndoa
🍁Manii kuwa mepesi

ZA MWANAMKE MWENYE CHANGO LA UZAZI.

🌹Kupata maumivu makali wakati anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi
🌹Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa
🌹Kuvurugika siku zake za hedhi
🌹Kujisikia homa kali anapokaribia siku zake za dhedhi
🌹Kupatwa hasirakali/ jazba anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi
🌹Kujisikia uchovu mkubwa anapokaribia siku zake za hedhi.
🌹Kuchukia kushiriki tendo la ndoa
🌹Kupata uvimbe kwenye kizazi
🌹Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi

YA CHANGO LA UZAZI KWA MWANAMKE.

🍂Vigumu kupata mimba
🍂Anaweza kuwa tasa kabisa
🍂Kuingia na kutoka kwa mimba
🍂Kuwa na hamu ya tendo la ndoa lakini hafikii kileleni
🍂Kuwa na uke mdogo sana na mkavu
🍂Homoni kutowiyana

18/10/2021

*NINI CHANZO CHA UKE KUWA MKAVU?*

Uke mkavu; ni tatizo ambalo husababishwa na upungufu wa homoni au kutokua na uwiano wa homoni ya estrogen ambayo hupelekea misuli ya uke kusinyaa na kukosa *vilainishi.*

Kwa kawaida uke unatakiwa kuwa na Ute wa wastani ambao hufanya uke kubana kuleta joto na Raha ya tendo.
Ute huo ukizidi Sana au kua pungufu Sana nalo ni tatizo.

*VISABABISHI VYA UKE MKAVU.*
👉🏿Utumiaji mafuta yenye kemikali (cosmetics)
👉🏿Magonjwa ya zinaa na fangasi.
👉🏿Matumizi ya sabuni za antibiotics kwa kuoshea uke.
👉🏿Upungufu wa homoni.
👉🏿Uoga na wasiwasi

*DALILI ZA UKE MKAVU*
👉🏿Maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉🏿Kupungua hamu ya tendo la ndoa
👉🏿Kua na ngozi kavu
👉🏿Maumivu ya mifupa na viungo
👉🏿Msongo wa mawazo
👉🏿Mzunguko wa hedhi Kubadilika badilika
👉🏿Kutokufurahia tendo la ndoa kutokana na Maumivu.
*MATIBABU YA UKE MKAVU*
Kuna lishe ambazo zimetengenezwa kwa kuzingatia tiba lishe na Ni Bora Zaidi kwa afya

0710705676
WhatsApp na sms za kawaida

Address

Kihonda
Morogoro

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Health Insurance posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share