25/06/2026
Sifa Muhimu za Hatari Zinazoweza Kukatiwa Bima.
Bima imejengwa juu ya kanuni muhimu za kiufundi ambazo huamua k**a hatari inaweza kukatiwa Bima au la.
Sifa nne kuu za hatari zinazoweza kukatiwa Bima, ambazo ni:
1. Sheria ya Idadi Kubwa (Law of Large Numbers)
2. Hasara za Bahati Mbaya (Fortuitous Losses)
3. Maslahi Yanayoweza Kukatiwa Bima (Insurable Interest)
4. Hatari Zisizo za Maafa Makubwa (Non-Catastrophic Exposures)
Kanuni hizi ndizo msingi wa:
1. Uandishi wa Bima (Underwriting)
2. Tathmini ya Hatari (Risk Assessment)
3. Upangaji wa Bei za Bima (Pricing)
4.Uendeshaji Endelevu wa Biashara ya Bima
ndani ya sekta ya kimataifa ya bima na bima ya kurejesha hatari (Reinsurance).
Kwa ujumla, kanuni hizi hutoa msingi imara unaowezesha kampuni za bima kutathmini hatari kwa usahihi, kupanga viwango vinavyofaa vya malipo, na kuhakikisha uendelevu wa shughuli za bima kwa muda mrefu.