25/03/2023
Mama Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania Hayati John Magufuli ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Kimataifa toleo la 3, inayotolewa na Taasisi ya Martha Tshisekedi Kasalu kwa kutambua mchango wake kwa Taifa la Tanzania na kwa Hayati Magufuli akiwa Rais wakati akitekeleza majukumu yake Kitaifa na Kimataifa.
Tuzo hizi za M. T. Kasalu ambazo hutolewa kwa Wenza wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Watu Maarufu Duniani kwa kutambua michango yao kwa Wenza wao, Jamii na Taifa husika, zimetolewa jana Ijumaa March 24, 2023 katika Hoteli ya Pullman Jijini Kinshasa ambapo Waandaaji wa Tuzo ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakishirikiana na Taasisi ya Lizadeel.
Kwa mwaka huu waliopokea Tuzo hizo ni Mama Janeth Magufuli, Mama Suzanne Mukay, Mke wa Daktari maarufu nchini DRC, wa magonjwa ya kina Mama na kansa, Mama Vivianne Dalo, Mke wa Mchungaji Maarufu na anayeheshimika DRC, Pastor Roland Dalo.
Wengne ni Mama Colette SENGHOR, Mke wa Rais wa kwanza wa Senegal, Leopold Senghor ambaye aliisaidia Senegal kupata Uhuru. A Mama Coretta KING Mke wa Martin Luther King ambaye Mumewe alisaidia mengi ikiwemo kupinga ubaguzi wa rangi USA.
Darasa La mapenzi