25/08/2026
Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Kaimu Mkeyenge mewaongoza watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Bi. Esther James Nyembera aliyekuwa Mwandishi Mwendesha Ofisi Mwandamizi, Idara ya Bima za Maisha aliyefariki dunia tarehe 22 Agosti, 2026 katika Hospitali ya Kairuki alipokua akipatiwa matibabu.
Akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu Dar es Salaam (Kimara, S**a) Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Nasemaba Mgonja amewapa pole familia huku akieleza namna NIC ilivyopoteza mtumishi mchapakazi ambaye wakati wote amekuwa akishirikiana na watumishi kwa upendo mkubwa.
Marehemu Esther James Nyembera amesafirishwa kwenda Kahama kwa mazishi yatakayofanyika Jumatano tarehe 26 Agosti 2026.
Shirika la Bima la Taifa (NIC) tunaendelea kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.