26/08/2026
Tarehe 22 Agosti 2026, Car & General Tanzania iliunga mkono Tamasha la Madereva wa Pikipiki na Tuk Tuk lililoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Madereva wa Pikipiki na Tuk Tuk Msasani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, lenye kauli mbiu: βKwa Pamoja Tunafurahi, Karibu AFCON Msasani.β
Tamasha hilo lililenga kuikaribisha AFCON Msasani huku likikuza umoja, mshikamano na ushirikiano kati ya madereva na Jeshi la Polisi, pamoja na kuchangia katika kuimarisha sekta ya usafirishaji na usalama katika jamii.
Washiriki walifurahia michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mbio za magunia, kukimbiza kuku na michezo mingine ya burudani.
Akizungumza wakati wa tamasha hilo, Mgeni Rasmi, Diwani wa Kata ya Msasani, Mh. Yusuph Hamisi Yusuph, aliwahamasisha viongozi wa Shirikisho kuendelea kuandaa matukio ya aina hii, akisisitiza kuwa michezo ni chachu ya kujenga jamii yenye umoja, mshikamano na usalama.
Car & General Tanzania-Tunaamini katika maendeleo ya jamii.