12/08/2025
Wiki iliyopita tulipata fursa ya kukutana na kuungana na wakulima, wachakataji wa mazao, na washirika kutoka sehemu mbalimbali Nchini
Katika kipindi hicho chote:
Tulifanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakulima ili kuelewa mahitaji na changamoto zao vyema zaidi.
Tulionesha suluhisho k**a pampu zetu za maji za sola na mashine za kuchakata mazao zinazosaidia kuongeza tija na maendelo kwenye secta ya kilimo.
Tulipata nafasi ya kujenga na kuimarisha ushirikiano na wadau muhimu katika mnyororo wa thamani wa kilimo.
Maonyesho haya yameimarisha dhamira yetu ya kutoa suluhisho sahihi, bora ,na zinazowawezesha wakulima na jamii za vijijini.
Kwa washirika wetu na wakulima wote waliotembelea mabanda yetu ,tunawashukuru sana kwa ushiriki wenu.
Tumedhamiria kuendeleza ari hii na kuleta mabadiliko makubwa zaidi pamoja.
Bank Plc Pass Leasing Rikolto - Vredeseilanden