Private Agricultural Sector Support - PASS Trust

Private Agricultural Sector Support - PASS Trust Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo iliyoanzishwa mwaka 2000 ili kuchochea uwekezaji na kukuza PASS Trust ni nini? HUDUMA ZIPI ZINAZOTOLEWA NA PASS Trust?

PASS Trust ni Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo iliyoanzishwa mwaka 2000 ili kuchochea uwekezaji na kukuza kilimo cha biashara na sekta zinazohusika. Ilisajiliwa mwaka 2007 k**a asasi isiyokuwa ya serikali kwa mujibu wa sheria ya ushirikishaji wadhamini ya mwaka 2002. DIRA
Kuwa asasi inayoongoza katika utoaji wa huduma za fedha na maendeleo ya biashara katika sekta ya kilimo. DHAMIRA
PASS

TRUST/Asasi ya PASS inawajibika katika utoaji wa huduma za maendeleo ya kilimo cha biashara na fedha kwa wafanyabiashara wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kuwaunganisha katika tasisi za fedha. MALENGO
Malengo ya PASS ni kuchochea uwekezaji na kuhimiza ukuaji wa kilimo nchini Tanzania. Huduma zinatotolewa na PASS ni:
1. Huduma za maendeleo ya Biashara.
2. Huduma za fedha. HUDUMA ZA MAENDELEO YA BIASHARA ZA PASS
PASS inatoa huduma nyingi za maendeleo ya biashara kwa wateja kwa kuchangia gharama. Huduma hizo ni pamoja na;
- Upembuzi yakinifu.
- Kuandaa mipango ya biashara.
- Kujenga uwezo-mfano katika maeneo maalumu ya kitaalamu. Kuwaunganisha wakulima katika vikundi ambavyo vinaweza kutumika k**a vikundi maalumu kwa ajili ya kilimo cha mkataba, kusambaza pembejeo kwamkopo, kufanya mazungumzo ya bei na kutoa ushauri.
- Utafutaji na uunganishaji masoko. HUDUMA YA FEDHA
PASS itawasaidia watu na makampuni yanayostahili kupata mkopo kwa ajili ya uwekezaji wenye faida kupitia Tathmini ya maandiko ya kuombea mkopo kulingana na masharti ya benki husika na kulionganishwa na benki hizo: CRDB, NMB, EXIM,TIB,FBME,KCBL,BOA,ABC, AKIBA COMMERCIAL BANK, n.k. Dhamana ya mkopo ambayo inatolewa kwa benki zenye mikataba ya kushirikiana na PASS ili kujazia upungufu wa dhamana ya mteja. NANI ANAYEWEZA KUOMBA HUDUMA ZA PASS? Mtu binafsi yeyote, Vikundi, Chama au kampuni inaweza kutumia huduma za PASS haswa:
- Wajasiriamali binafsi - ambao ni watu binafsi, vyama au kampuni zinazoshughulika na sekta ya kilimo.
- Wajasiriamali binafsi - ambao wana dira na wanafanya biashara katika hali ya ufanisi na kibiashiara.
- Wajasiriamali binafsi - watakaoshirikiana na PASS na Benki washirika na kuwakilisha nyaraka zinazotakiwa na ambao wanaweza kufikia angalau vigezo vya msingi kwa ajili ya ukopaji. Kipaumbele kitatolewa kwa wateja wenye motekeo makubwa katika mwendelezo wa mnyororo wa thamani wa bidha za kilimo hususani katika mazao ya chakula, biashara na mazao ya kusafirishwa nje ya nchi.

26/08/2026

For 63 years, Sweden and Tanzania have shared a development partnership built on cooperation, trust and a common commitment to creating lasting impact.

This 25-minute documentary looks at the journey of Swedish development cooperation in Tanzania highlighting the achievements, experiences and stories of different organisations and partners who have been part of this longstanding relationship.

PASS Trust is proud to be among the organizations featured in this broader story, with our Managing Director sharing insights from PASS Trust’s experience and contribution to Tanzania’s development journey.

Watch the full documentary link in Bio

Video Credit Swedish Embassy - Tanzania

Heri ya siku ya Maulid
25/08/2026

Heri ya siku ya Maulid

PASS Trust Managing Director, Mr. Yohane Kaduma, met with the new Enabel Country Director, Ms. Virginie Hallet, during t...
17/08/2026

PASS Trust Managing Director, Mr. Yohane Kaduma, met with the new Enabel Country Director, Ms. Virginie Hallet, during the Nanenane Exhibitions in Dodoma.

The introductory meeting explored opportunities to build on the longstanding PASS-Enabel partnership, particularly in expanding credit guarantees and business development support for SMEs and MSMEs across agriculture, fisheries, forestry and livestock value chains.

The discussion also explored opportunities to strengthen trade and investment linkages, connecting enterprises supported through PASS’s financing ecosystem and PASS itself with markets, investors and new commercial opportunities.

With a shared focus on women and youth, PASS and Enabel have successfully worked together to strengthen enterprises and improve access to finance. The next chapter presents an opportunity to scale this impact by unlocking more capital, investment and market opportunities for businesses, jobs and inclusive economic growth.
Enabel in Tanzania

AccessToFinance Agribusiness Youth WomenEntrepreneurs SMEs Tanzania

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Badria Atai Masoud, ametembelea banda la P...
10/08/2026

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Badria Atai Masoud, ametembelea banda la PASS Trust katika Maonyesho ya NaneNane yanayofanyika Dole Kizimbani, Zanzibar.

Ziara hiyo imekuwa fursa ya kubadilishana uzoefu kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano na kuwezesha wakulima na wafanyabiashara wa kilimo kupata huduma za kifedha, teknolojia na fursa za kukuza biashara zao

PASS Trust inawatakia Watanzania wote, hususan wakulima, wafugaji, wajasiriamali na wadau wa sekta ya kilimo, NaneNane y...
08/08/2026

PASS Trust inawatakia Watanzania wote, hususan wakulima, wafugaji, wajasiriamali na wadau wa sekta ya kilimo, NaneNane yenye mafanikio na matumaini mapya

PASS Trust inaendelea kushiriki Maonesho ya Nane Nane Zanzibar kwa kuwaleta pamoja wakulima, wajasiriamali wa kilimo na ...
07/08/2026

PASS Trust inaendelea kushiriki Maonesho ya Nane Nane Zanzibar kwa kuwaleta pamoja wakulima, wajasiriamali wa kilimo na wadau mbalimbali kujifunza kuhusu huduma zetu na ushirikiano unaochochea ukuaji wa sekta ya kilimo.

Tembelea banda letu ujifunze jinsi tunavyowezesha upatikanaji wa huduma za kifedha, kukuza biashara za kilimo na kujenga sekta yenye tija na ushindani kwa maendeleo ya Taifa.

05/08/2026

Kupitia programu zetu za uwezeshaji wa kilimo, PASS Trust imewezesha zaidi ya wanufaika milioni 4.9 na kuwezesha mikopo yenye thamani ya TSh trilioni 3.29 kwa ajili ya kukuza uzalishaji na biashara za kilimo nchini.

Akizungumza katika Maonesho ya Nane Nane, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa PASS Trust, Bw. Adam Kamanda, amesisitiza dhamira ya PASS Trust katika kuimarisha upatikanaji wa fedha, kuongeza tija na kuwawezesha wakulima kufikia masoko, sambamba na kaulimbiu ya mwaka huu: “Tambua Soko, Ongeza Tija kwa Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Ushirikiano wa kimkakati ni msingi wa kuleta matokeo katika kilimo.Wadau mbalimbali wanaendelea kutembelea banda la PASS...
05/08/2026

Ushirikiano wa kimkakati ni msingi wa kuleta matokeo katika kilimo.

Wadau mbalimbali wanaendelea kutembelea banda la PASS Trust katika Maonesho ya Nane Nane 2026 kujifunza zaidi kuhusu huduma zetu za kifedha na suluhisho tunazotoa kwa ajili ya kuwawezesha wakulima, wafanyabiashara na wadau wa mnyororo wa thamani wa kilimo.

Karibu PASS Trust, tuungane kukuza fursa na maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa PASS Trust Bw. Adam Kamanda ametembelea banda la Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) ka...
04/08/2026

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa PASS Trust Bw. Adam Kamanda ametembelea banda la Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) katika Maonesho ya Nane Nane, ambapo PASS Trust imefanya majadiliano kuhusu fursa za kuimarisha sekta ya kahawa kupitia ushirikiano wa kimkakati.

Kupitia ushirikiano na wadau mbalimbali, PASS Trust inaendelea kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha na suluhisho bunifu zinazowawezesha wakulima na wadau wa mnyororo wa thamani wa kahawa kuongeza tija, ubora wa uzalishaji na ushindani wa kahawa ya Tanzania katika masoko ya ndani na kimataifa.

Tanzania Coffee Board

Tunafurahia kupata fursa ya kuzungumza na wakulima, wajasiriamali, taasisi na wadau wengine kuhusu namna tunavyoendelea ...
03/08/2026

Tunafurahia kupata fursa ya kuzungumza na wakulima, wajasiriamali, taasisi na wadau wengine kuhusu namna tunavyoendelea kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha na kujenga sekta ya kilimo yenye tija na endelevu

Tupo katika maenesho ya NaneNane hapa Dodoma. Karibu utembelee Banda letu linalopatikana kwenye hema la Taasisi za Fedha na ujionee fursa zinazotolewa na PASS Trust.

Address

P. O. Box 9490, PSSSF Commercial Complex, 5th Floor – Wing B, House No. 24, Sam Nujoma Road
Dar Es Salaam
16102

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Private Agricultural Sector Support - PASS Trust posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Private Agricultural Sector Support - PASS Trust:

Share