17/04/2026
"KIDUCHU" - Fresh Tunasonga
Mkurugenzi Mtendaji wa , Bw. Edwin Urasa, ameshiriki katika uzinduzi wa kampeni ya “Kiduchu” yenye kaulimbiu “Fresh, Tunasonga!” ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inayolenga kusisitiza umuhimu wa urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu unaozingatia uwezo wa kila mnufaika hususan katika sekta isiyo rasmi ili kuhakikisha uendelevu wa mfuko kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Edwin Urasa, amesema kampeni hiyo imekuja wakati muafaka kwani wadaiwa wengi wanatoka katika sekta isiyo rasmi, hivyo utaratibu wa kulipa kidogo kidogo utawawezesha kurejesha mikopo kwa urahisi zaidi.
Uzinduzi huo umefanyika leo, (Aprili 17, 2026), katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Kanda ya Mashariki, jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir.
Kampeni hii inalenga kuwahamasisha wanufaika kuanza kurejesha mikopo yao kwa kiasi kidogo walichonacho, kwa kuanzia TZS 5,000. Kampeni ya “Kiduchu”, imelenga kuwafikia wanufaika 135,186 wanaodaiwa jumla ya TZS 920 bilioni.
Creditinfo Tanzania ni taasisi inayopokea na kuchakata taarifa za mikopo, ikitoa huduma muhimu za kusaidia benki na taasisi za kifedha kufanya maamuzi bora ya mikopo na huduma za kifedha.