Mwalimu Vicoba Endelevu

Mwalimu Vicoba Endelevu Fahamu vizuri kuhusu mfumo wa vicoba endelevu

Leo nikiwa katika kutembelea vijana wenzangu na kuzungumza nao  Mbagala kuu-dar
30/10/2019

Leo nikiwa katika kutembelea vijana wenzangu na kuzungumza nao
Mbagala kuu-dar

30/10/2019

UMADHUTI WA VICOBA

1. Uanzishaji wa kikundi cha vicoba hauhitaji mtaji

2: Mikopo ya vicoba haina mashart mengi k**a fedha zipo

3: Kupitia mfumo wa vicoba wanakikundi hupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ,
Mf: biashara, ufugaji, sheria, jinsia, kilimo n.k

4: Mfumo wa utunzaji kumbukumbu ni rahisi ambao unawezesha wananchi kusimamia kumbukumbu zao za fedha bila kuhitaji elimu ya juu ya utunzaji wa fedha.

5: Ziada ya mkopo inayopatikana hutolewa mgao kwa wanakikundi wote

29/10/2019

MADHUMUNI YA KUANZISHWA KWA MFUMO WA VICOBA ENDELEVU

1: kuwajengea uwezo na desturi ya kuweka akiba wsnanchi

2: kujipatia mikopo isiyokuwa na masharti mengi lakini kwa urahisi

,3: kuweka urahisi wa utoaji mafunzo ya kujitambua,ujasiliamali na fedha kwa wananchi

4: kuwajengea uwezo wananchi kuwa na miradi ya pamoja

5: kuwajengea wananchi uwezo wa kukopesheka kwenye miradi mikubwa

6: kutatua matatizo ya dharura ya wananchi

Wanachama cha kikundi wanawake wa kiismalu wakipata elimu juu ya mfumo WA kujiwekea akiba vicoba endelevuWakiwa makao ma...
29/10/2019

Wanachama cha kikundi wanawake wa kiismalu wakipata elimu juu ya mfumo WA kujiwekea akiba vicoba endelevu
Wakiwa makao makuu dar sinza whiteinn
Tunawashukuru sana hakika mlipata kitu hamkuondoka bure

29/10/2019

TUNAMALIZIA FAIDA ZA VICOBA ENDELEVU

D:KUWEZA KUKOPESHEKA KWENYE MIKOPO MIKUBWA
Unapokuwa katika kikundi chochote kile cha kikoba endelevu unapata dhaamana ya kukopa mikopo mikubwa
Mf:bank ya kuna benki za hapa nchini kwetu wanatoa viwanja wanapata nafasi sana wanachama waliokua katka kikundi kilichosajiliwa na kinatambulika kisheria na kwa bei nafuu sanaa
Vilevile kikundi endelevu hupata sifa kwakua ni endelevu hivyo baadhi ya mabank hutoa mikopo ya miaka 3 ya viwanja, magari au mitaji mikubwa ya biashara .

F:KUTOA URAHISI KWA WANACHAMA KUPATA MIKOPO HATA K**A KIKUNDI KIMEFIKIA KATIKATI YA MWAKA

Vicoba endelevu oyeeeeee
29/10/2019

Vicoba endelevu oyeeeeee

Ni kikundi cha kikoba endelevu wanachama wakimkabidhi mwanakikundi mmoja wapo mkopo wa piikipiki hii inapendeza Vicoba e...
29/10/2019

Ni kikundi cha kikoba endelevu wanachama wakimkabidhi mwanakikundi mmoja wapo mkopo wa piikipiki hii inapendeza
Vicoba endelevu oyeeeeee
Hii ni jana baada yakumaliza kikao Makao makuu ya YEMCO sinza whiteinn

28/10/2019

Haijalishi unapitia hali gani ngumu usikate tamaa songa mbele. Changamoto kazini, nyumbani, katka shughuli zozote zile usikate tamaa hakika siku ipo Mungu atakuona na kukushika mkono na kukuinua

08/08/2019

VICOBA ENDELEVU
Hivi ni vikundi vya vicoba ambavyo kila inapofika mwisho wa mwaka wanagawana jamii na faida halafu hisa zinabaki na kuendelea Kwenye kila mwaka

FAIDA ZA VICOBA ENDELEVU
@. Kufanya biashara endelevu
Mfumo wa vicoba endelevu humpa nafasi mwanachama wa kikundi husika au kikundi chenyewe kuwa na biashara endelevu

B) kuongezeka kwa kiwango cha mikopo
Kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha hisa kila mwaka
MF; mwanachama kwa mwaka Ana hisa za sh200,000 tena akawa ananunua hisa 200,000 mwaka wa pili atakuwa na jumla ya hisa400,000 hivyo anaweza kukopa mkopo wa sh1,200,000 anaendelea na kukuza. Biashara yake

C) kuwa na malengo makubwa na endelevu

08/08/2019

Tunamalizia changamoto za vicoba vunjavunja zipo nyingi ila tumeorodhesha baadhi.

4: Kutokukopesheka Kwenye mikopo mikubwa.
Vikundi ambavyo vinavunja kila mwaka vinapoteza sifa za kukopesheka Kwenye mikopo mikubwa ya taasisi zingine za kifedha.
MF, benki inafursa ya kutoa mkopo wa miaka mitatu Kwenye vikundi vya vicoba, vicoba vunjavunja huenda kikakosa fursa hii kwasababu wao huvunja kila baada ya mwaka mmoja na tukumbuke kuna baadhi wataendelea na wengine hawataendelea tena na kikundi

5:kutokutimiza malengo makubwa

6:kutokuwapa nafasi wanachama ya kuchukua mikopo mwisho wa mwaka

Bado vipo vitabu kufaham vzur mfumo wa vicoba endelevu
07/08/2019

Bado vipo vitabu kufaham vzur mfumo wa vicoba endelevu

07/08/2019

Tunaendelea changamoto za vicoba vunjavunja

2;kutokuwa na miradi na biashara endelevu
K**a kikundi kinavunja kila baada ya mwaka mmoja hii husababisha kikundi kutokuwa na miradi endelevu kwasababu inatakiwa kila mwaka waweze kugawana fedha wanachama

3:kutokukuwa kwa mikopo

Kwasababu kila mwaka wanavunja hii inamaana kwamba k**a mtu kiwange chake cha kununua hisa ni laki1 ataishia kukopa mikopo ya shlaki3 kila mwaka hawezi kupanda apo kwasababu kila mwaka anarudishiwa hisa zake zote

Address

Dar Es Salaam
15112

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
18:00 - 19:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Telephone

0715283578

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwalimu Vicoba Endelevu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share