06/02/2025
Anatuandikia wakala: Alikuja jamaa mmoja smart hivi, muonekano wa kiboss. Aka-pack IST yake mbele ya ofisi na kuja kupata huduma ya kutoa pesa kiasi cha TZS.500,000/=
Alinichangamkia na kunifanya rafiki ndani ya muda mfupi. “Vipi naweza kutoa 500k mrembo?” Nikamjibu ndiyo. Akaanza kusifia ofisi yangu kuwa ni nzuri sana, nikamjibu Ahsante.
Kweli akatoa ile 500,000/= nikamhesabia nikampa. Punde akaja mtu mwingine nae akasema anatoa 200,000/=. Hisia zinaniambia walikuwa pamoja. Alikuja kuchukua attention yangu.
Huyu wa 200k akani-keep busy kidogo, wakati naendelea nae, huyu mwingine akaniambia naomba simu yako nikuandikie namba yangu ya simu uje umuulize Boss wako kuhusu fundi aliyetengeneza hapa nina shida nae.
Ak**aliza akaondoka. Huyu mwingine nae akaondoka. Baada ya k**a dakika 20 hivi nikaona sms Boss wangu(Muajiri wangu) akinipa maelekezo ya kutuma pesa kwenye namba fulani. Nikasema sawa, nikatuma.
Mara ya kwanza nilipewa maelekezo ya kutuma TZS400,000/=. Dakika moja tena akasema nitumie TZS600,000/= jumla iwe milion moja -Nikatuma. Akaniuliza kwenye mtandao mwingine kuna kiasi gani? Nikamwambia akasema tuma. Zoezi zima linaisha nilikuwa nimeshatuma TZS3,000,000/=.
Nilipokuja kushtuka ni pale aliponiuliza Bank fulani ina shilingi ngapi? Ndipo nikashangaa inamaana boss hajui kuwa hatuna hii huduma? Kuangalia Namba ya simu sio yake. Kumbe tapeli aliandika namba yake akafuta ya Boss muda ule nipo busy na mteja wa 200,000.
MBINU ALIYOTUMIA TAPELI:
1. Kujenga urafiki na mazoea
2. Alitoa hela halisi ili kumtoa hofu
3. Aliangalia sehemu ya SMS na kujua jina la Boss wake.
3. Ali-fake conversations za mwisho za Mfanyakazi na Boss wake.
USHAURI:
•SMS sio lugha ya kibiashara, Piga simu boss wako atoe maelekezo kwa mdomo na ujiridhishe pasi na shakakuwa hayupo sehemu hatarishi akiwa na akili timamu (Beyond reasonable doubt, with sound mind).
•Usimpe mtu ashike simu yako, namba mwambie akutajie uandike.
•Mambo ni mawili: asubiri/awe mpole uhudumie wateja au aondoke kwa amani.
Graphics: jordan Mallya
Caption: Hemedy, Esq.
06 February, 2025. Dar es salaam.