12/08/2026
Leo tumefikisha Kasi Isambazayo Tabasamu hadi Benki Kuu ya Tanzania.
Tumemkabidhi Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba, jezi na vifaa rasmi vya CRDB Bank Marathon 2026, ikiwa ni mwaliko wa kuungana nasi katika mbio hizi kwa lengo la kusambaza tabasamu kwa wenye uhitaji katika jamii.
Makabidhiano hayo yamefanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa.
Gavana yupo tayari kwa ajili ya kusambaza tabasamu tarehe 16 Agosti 2026.