Team MONEY Makers

Team MONEY Makers TEAM MONEY MAKERS ni kikundi cha vijana wenye mtazamo sawa wa kupiga vita umasikini pamoja na kusaidiana.

13/07/2016

LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MTADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi k**a unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.
Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.
- paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
-mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
- layer's consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.
TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake
Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500
-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga
Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe k**a mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. K**a ni sehemu za mjini litakugharimu k**a Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.
Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe. Nikiwa na maana k**a kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.
Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.

12/12/2015

TEAM MONEY MAKERS

Uongozi wa team money makers unapenda kukumbusha mwanachama/mwanakikundi kuwa tumebakiwa na siku 8 kufanya shughuli yetu ya uzinduzi wa TMM's.
Unaombwa kununua T - shirt ya kikundi, kabla ya siku ya uzinduzi pamoja na kutoa pesa yako ya uzinduzi au kumalizia kabisa ilikufanikisha shughuli yetu.

KIJANA PIGA VITA UMASIKINI CHANGIA MAENDELEO YAKO NA YAMWENZAKO.

Ahsanteni sana.

29/11/2015

TEAM MONEY MAKERS

Mpendwa Mwakikundi.
Leo ni tarehe 29/11/2015 ni siku ya jumapili.
Tutakuwa na kikao chetu cha Nne cha wanakikundi ambacho kitaanza kufanyika saa 10 kamili Alhasili.
Mahala ni pale pale tulipokutana katika kikao cha pili na cha tatu mtaarifu na mwenzio.

Kuwai ni muhimu sana katika kufikia madhumuni ya kikao.
Ahsanteni !!

KIKAO CHA TATU CHA  WANAKIKUNDI.AGENDA ZA KIKAO(1)Utafutaji wa masoko kwa ajili ya kikundi(2) Uchambuaji wa vipengele vy...
26/11/2015

KIKAO CHA TATU CHA WANAKIKUNDI.

AGENDA ZA KIKAO
(1)Utafutaji wa masoko kwa ajili ya kikundi
(2) Uchambuaji wa vipengele vya Rasmu ya katiba ya kikundi
N.K

PICHA YA WANAKIKUNDI WA KIWA KATIKA VIKAO VYA KILA MWISHO WA JUMAA.majadiliano yaliyokuwa ya kihusu RASMU pendekezwa ya ...
26/11/2015

PICHA YA WANAKIKUNDI WA KIWA KATIKA VIKAO VYA KILA MWISHO WA JUMAA.

majadiliano yaliyokuwa ya kihusu RASMU pendekezwa ya katiba ya kikundi cha TEAM MONEY MAKRRS

T-SHIRT ambazo ni mradi wa kikundi bei yake ni Tsh 15000.KWA MAITAJI TUMIA SIMU: Mwenyekiti- 0653727102Afisa Masoko- 065...
26/11/2015

T-SHIRT ambazo ni mradi wa kikundi bei yake ni Tsh 15000.
KWA MAITAJI TUMIA SIMU:
Mwenyekiti- 0653727102
Afisa Masoko- 0656708252

25/11/2015

TEAM MONEY MAKERS ni kikundi cha vijana wenye mtazamo sawa wa kupiga vita umasikini pamoja na kusaidiana.
WALENGWA: Ni vijana wote wa kitanzania mwenye umri wa miaka 15 na kuebdelea mwenye mtazamo sawa na dhamira yetu kuu ya kikundi ya kupiga vita umasikini pamoja na kusaidiana.
NJIA YETU kubwa ya kutupatia kipato k**a kundi ni biashara kunafaida nyingi kwa mwanakikundi. Karibu ujumuike na sisi.
Tunapatikana MWANANYAMALA HOSPITAL - karibu na kituo cha Angaza (AMREF).

Kwa Mawasiliano:
SAID IBRAHIM MBULU- Mwenye kiti
[email protected]
0653727102
Au
SALUM KHAMIS- Katibu wa kikundi
[email protected]
0773145075

KIJANA PIGA VITA UMASIKINI CHANGIA MAENDELEO YAKO NA YAMWENZAKO

25/11/2015

Team Money MakersInajiusisha
(1) Kumsaidia kijana kupiga vita umasikini pamoja na kusaidiana.
SHUGHULI ZA KIKUNDI
(a) Kubuni na kutengeneza T-SHIRT
(b) Kuingiza-kusambaza na kuuza bidhaa za kilimo-uvuvi na ufugaji kutoka mikoani
(c) Kusaidia jamii inayotuzunguka katika maswala ya usafi na majanga

Address

MWANANYAMALA/HOSPITAL (AMREF) Email: Teammoneymakers7@gmail. Com PHONE: 0653727102
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Team MONEY Makers posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share