Jubilee Group Tanzania

Jubilee Group Tanzania Jubilee Insurance is the number one insurer in East Africa.

25/08/2026

Tunakutakia Sikukuu njema ya Maulid kwako na familia yako.

Timu ya Jubilee Group katika picha ya pamoja na timu ya CRDB International Marathon baada ya kushiriki CRDB Internationa...
17/08/2026

Timu ya Jubilee Group katika picha ya pamoja na timu ya CRDB International Marathon baada ya kushiriki CRDB International Marathon iliyofanyika jana, tarehe 16 Agosti 2026.

Katika picha, kutoka kushoto: Pendason Philemon – Director of Procurement; Ms. Helena Mzena – CEO, Jubilee Life; Boma Raballa – Chief Commercial Officer (CCO); Dereck Rwezaura – Chief Distribution Officer; na Douglas Mpangile – Head of Business Development, Jubilee Group.

Leo, timu ya Jubilee Group tumeshiriki CRDB International Marathon! Tukiwa na nguvu, umoja na moyo wa kujenga jamii yeny...
16/08/2026

Leo, timu ya Jubilee Group tumeshiriki CRDB International Marathon!

Tukiwa na nguvu, umoja na moyo wa kujenga jamii yenye afya.

14/08/2026

Kampuni ndogo na za kati bima za afya za JBiz na FBiz ni mahususi kwenu! Linda wafanyakazi wako na bima za afya za JBiz na FBiz kwa gharama nafuu.

Tupigie simu 0748500877 au tembelea tovuti yetu link ipo kwenye BIO kupata maelezo zaidi.



Leo, tulipata heshima ya kumkaribisha Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware, kwa mazungumzo yenye tija kuhusu ...
12/08/2026

Leo, tulipata heshima ya kumkaribisha Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware, kwa mazungumzo yenye tija kuhusu Dira ya Sekta ya Bima Tanzania 2050.

Mazungumzo yalilenga kuimarisha sekta ya bima, kuchochea ubunifu, kupanua ulinzi wa kifedha na kujenga sekta ya bima yenye ustahimilivu na jumuishi kwa vizazi vijavyo.

Jubilee Group tunaendelea kujitolea kuwa sehemu ya safari hii ya mabadiliko na kuchangia katika kujenga sekta ya bima imara na endelevu zaidi Tanzania.

Kwa pamoja, tunajenga sekta ya bima. 🇹🇿

08/08/2026

Jubilee Group inawatambua wakulima k**a nguzo muhimu ya uchumi wa Tanzania. Kupitia juhudi na kujituma kwenu kila siku, mnaweka chakula mezani, mnachangia ukuaji wa uchumi na kujenga Tanzania yenye maendeleo na ustawi zaidi.

Tunapoadhimisha Nane Nane, tunakukumbusha kuwa afya na maisha yako ni muhimu. Jubilee Group tupo hapa kuwa mshirika wako wa kuaminika katika kukulinda wewe na familia yako.

Heri ya Nane Nane kwa wakulima wote na wadau wa sekta ya kilimo!

Leo, Ijumaa tarehe 7 Agosti 2026, Jubilee Group Tanzania imezindua rasmi ukuta uliojengwa kuzunguka Shule ya Msingi Made...
07/08/2026

Leo, Ijumaa tarehe 7 Agosti 2026, Jubilee Group Tanzania imezindua rasmi ukuta uliojengwa kuzunguka Shule ya Msingi Madenge iliyopo Temeke, Dar es Salaam.

Mradi huu umetekelezwa ili kuimarisha usalama wa wanafunzi na walimu pamoja na kutatua changamoto ya usumbufu uliokuwa ukisababishwa na wapita njia, hali iliyokuwa ikiathiri mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.

Tunaamini kuwa ukuta huu utachangia kuimarisha mazingira salama na tulivu ya elimu, hivyo kuwapa walimu nafasi bora ya kufundisha na wanafunzi mazingira mazuri ya kujifunza na kufanya vizuri kitaaluma.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Maafisa Watendaji Wakuu wa Jubilee Life Insurance na Jubilee Health Insurance, Bi. Helena Mzena na Dkt. Harold Adamson, pamoja na viongozi wa serikali za mitaa, uongozi wa shule na wafanyakazi wa Jubilee Group Tanzania.

Jubilee Group Tanzania itaendelea kutekeleza shughuli za uwajibikaji kwa jamii (CSR) kwa lengo la kuleta mchango chanya katika elimu, afya na ustawi wa jamii, kwa kuamini kwamba jamii yenye maendeleo ndiyo msingi wa maendeleo endelevu ya taifa.

Nanenane Kaskazini kumepambazuka! 🌾🎉Karibu Kijiji cha Bima na upate huduma bora kutoka Jubilee Health Insurance.Tunakule...
06/08/2026

Nanenane Kaskazini kumepambazuka! 🌾🎉

Karibu Kijiji cha Bima na upate huduma bora kutoka Jubilee Health Insurance.

Tunakuletea suluhisho za bima ya afya kwa watu binafsi, familia, SMEs na taasisi, ili uwe na amani ya moyo kila siku.

Pia tulifurahi kupokea ugeni kutoka Ofisi ya RAS Mkoa wa Manyara uliotutembelea katika banda letu, tukipata fursa ya kushirikiana na kubadilishana mawazo kuhusu umuhimu wa bima ya afya kwa jamii.

Tembelea banda letu, zungumza na wataalamu wetu, na ujifunze jinsi Jubilee Health inavyoweza kukulinda wewe na wapendwa wako.

Jubilee Health Insurance – Afya Yako, Kipaumbele Chetu.

NanenaneKaskazini

28/07/2026

Hata k**a kampuni yako ni ndogo, mnastahili ulinzi wa afya zenu. Bima ya afya ya FBiz ipo kuwalinda kikamilifu.

Kwa msaada zaidi kuhusu kujiunga na Bima ya Afya ya FBiz, tupigie simu kupitia 0748500877.

21/07/2026

Bado haujachelewa jiunge na Mpango Binafsi wa Pensheni uanze kujiweka akiba kwa ajili ya kesho yako.

Kwa maelezo na msaada, tupigie simu
BURE kupitia 0800783030.

Address

Faykat Tower, 7th Floor, Ali Hassan Mwinyi
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255222110176

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jubilee Group Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Jubilee Group Tanzania:

Shortcuts

Share