AJ Recoveries limited

AJ Recoveries limited Loan recoveries /management of NPL and auctioneering

25/12/2023

Amezaliwa

Hatua benki inatakiwa kuchukua kabla ya kuuza dhamana ya nyumba ya mdaiwa,1.Kutoa notisi za kukumbusha malipo ya marejes...
26/01/2023

Hatua benki inatakiwa kuchukua kabla ya kuuza dhamana ya nyumba ya mdaiwa,
1.Kutoa notisi za kukumbusha malipo ya marejesho kwa ucheleweshaji kuanzia siku 7 hadi 30.
2.kutoa onyo na notisi ya mwisho(final demand notice) kwa mdaiwa aliyechelewesha ndani ya marejesho mawili yaani chini ya siku sitini.
3.Mteja anaposhindwa kulipa,pamoja na kupewa onyo na notisi basi benki itaamua kuanza utaratibu wa kuuza dhamana(Nyumba)iliyowekwa kwa mkopo ili kufuta deni.
4.Kwa mujibu wa sheria ya ardhi benki inatakiwa kutoa notisi ya siku sitini kwa mdaiwa kulipa deni lote kwa maana benki haina nia ya kuendelea na mkataba wa mkopo wako kwa sababu imeonekana biashara yako na wewe mdaiwa hamna uwezo wa kulipa deni tena.ikumbukwe hapa mdaiwa unatakiwa ulipe mkopo wako wote hata k**a muda wa mkataba haujaisha.
5.baada ya siku sitini kuisha k**a umeshindwa kufuta deni lako basi benki itateua dalali kuendelea na utaratibu ili kuuza dhamana kwa njia ya mnada.benki hairuhusiwi kuuza dhamana yenyewe inatakiwa kukabidhi kwa dalali.
6.Dalali anatakiwa kutoa kwanza notisi ya siku 14 kwa mdaiwa vinginevyo utaratibu wa kuuza dhamana kwa mnada unaendelea.
7.Baada ya siku 14 kuisha ni lazima mnada utangazwe katika gazeti.inapendekezwa liwe gazeti linalotoka kila siku au la serikali. Ni muhimu dalali kutoa taarifa ya tangazo la gazeti kwenye serikali ya mtaa ilipo dhamana ikiwezekana tangazo la gazeti liwekwe kwenye mbao za matangazo ofisi serikali ya mtaa.
Utaratibu huu usipofuatwa uuzaji wa dhamana unakuwa batili na mdaiwa anayo nafasi kubwa kushinda kesi k**a akifungua.
Nakumbusha mabenki vitu viwili muhimu sana,
1.Notisi ya siku 60 kwa mdaiwa inapohusisha uuzaji wa dhamana ya nyumba.
2.Tangazo la mnada kwenye gazeti ni lazima.
Asanteni sana tutaendelea kupeana elimu.

13/11/2020

Address

PO BOX1056, DAR ES SALAAM
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 13:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AJ Recoveries limited posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category