Mwanga Community Bank

Mwanga Community Bank To empower the community via financial intermediation by providing valuable and efficient financial services to support and strengthen their development

A regional Community bank offering all banking services, The light for your development

Follow my pages: To keep in touch on professional matters and enjoy my company offers.
11/07/2024

Follow my pages: To keep in touch on professional matters and enjoy my company offers.

View Anitha Micah Pallangyo’s profile on LinkedIn, the world’s largest professional community. Anitha Micah has 6 jobs listed on their profile. See the complete profile on LinkedIn and discover Anitha Micah’s connections and jobs at similar companies.

Nini maana ya ujasiriamali, toa maoni yako...
27/02/2018

Nini maana ya ujasiriamali, toa maoni yako...

Je wajua?Kiwanda pekee kinachotengeneza spirit Tanzania ambayo ndio malighafi inayotumika kutengeneza dawa hospitalini, ...
11/02/2018

Je wajua?
Kiwanda pekee kinachotengeneza spirit Tanzania ambayo ndio malighafi inayotumika kutengeneza dawa hospitalini, perfume, pombekali n.k kinapatikana wilaya ya mwanga mkoani Kilimanjaro, kinaitwa Biochem Ltd kipo maeneo ya kifaru karibu na Kifaru oil investment company ya kituo cha mafuta. Biochem ambao pia ni moja kati ya wateja wakubwa na wakongwe wa Mwanga Community Bank.

11/02/2018

Kila mwana Kilimanjaro akijitolea kununua hisa kwa tsh10,000 tu, ataiwezesha benki ya wananchi mwanga kuongeza mtaji hivyo kuboresha huduma na kuweza kuwafikia wanakilimanjaro Tanzania nzima!!! Kwa Maelezo zaidi piga 0759601196

10/02/2018

FUNGUA AKAUNTI, WEKA AKIBA, VUNA FAIDA NZURI YA AKIBA ULIOWEKA MWANGA COMMUNITY BANK.
NYARAKA MUHIMU KUFUNGULIA AKAUNTI:
1. PICHA 3 ZA PASSIPOTISAIZ ZA RANGI
2. KITAMBULISHO NAKALA NA ORIJINO (KURA/LESENI YA UDEREVA/UTAIFA/PASSI YA KUSAFIRIA)
3. BARUA YA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MTENDAJI WA SERIKALI ZA MTAA UNAPOISHI
4. KIASI KISICHOPUNGUA 15,000/=

KARIBUNI SANA!!!!

10/02/2018

TUNAKOPESHA!!!!

WAFANYABIASHARA, WAAJIRIWA, WASTAAFU, WAKULIMA, WANAVIKUNDI K**A VILE VICOBA,SACCOs, VSLA N.K
K**A UPO NDANI YA MKOA WA KILIMANJARO WASILIANA NASI KUPITIA NAMBA 0759601196

Wanakikundi kinachojulikana k**a Tumaini Group, waliopo Mandaka mnono Old moshi magharibi, walipokutana katika kikundi c...
10/02/2018

Wanakikundi kinachojulikana k**a Tumaini Group, waliopo Mandaka mnono Old moshi magharibi, walipokutana katika kikundi chao k**a ilivyo ada kuwa kila wiki wanakutana kukusanya hisa na mchango wa jamii, kufanya marejesho ya mkopo pamoja na kujua maendeleo ya kikundi chao.
Kikundi cha Tumaini chini ya uongozi wa mwenyekiti wao Eliaichi Jacob Mrema, ni moja kati ya vikundi kongwe vilivyojiunga na benki ya wananchi. Kikundi hiki kina wananchama 30 na wengi wao wanajishughulisha na kilimo cha mpunga.
Benki hutoa huduma kwa wanavikundi hasa vya kina mama na mchanganyiko na kina baba, kwa kuwafungulia akaunti zisizokua na makato ya kila mwezi, wanajipatia faida kila mwaka, afisa huwatembelea na kuwapa elimu ya ujasiriamali na nidhamu ya fedha kabla hawajapata mkopo.

Wilaya ya Mwanga yajivunia kuanzishwa kwa kiwanda cha maji safi ya kunywa kinachojulikana kwa jina la Mwanga Pure Drinki...
10/02/2018

Wilaya ya Mwanga yajivunia kuanzishwa kwa kiwanda cha maji safi ya kunywa kinachojulikana kwa jina la Mwanga Pure Drinking water kilichopo Lambo kata ya Shighatini wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro. Kiwanda kinafanya mchakato wote wa uzalishaji, ikiwemo kutengeneza chupa, kujaza maji, kuweka nembo na kupaki kwenye katoni maalumu kulingana na ujazo ambapo wanatengeneza maji ya ujazo wa nusu lita, lita moja hadi lita moja na nusu.
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Bwana Kassim Msemo amesema, "Kiwanda kilianza kujengwa kuanzia 2016 baada ya wazo hilo kutoka mwaka 2015 na hatimaye kupitia ushirikiano walioupata kutoka Benki ya wananchi mwanga kiwanda hicho kilikamilika ujenzi mwaka 2017 na kufunguliwa rasmi mwaka 2017 septrember na kiongozi wa mbio za mwenge kwenye mbio za mwenge mkoani kilimanjaro."
Pamoja na fursa ya kuwapatia wananchi wa eneo hilo maji safi na salama kwa bei nafuu sana, pia wameweza kutoa ajira kwa wananchi wa kijiji cha lambo.
Maji hayo kwa sasa yameanza kuuzwa maeneo ya mwanga na wanatarajia kupeleka Rombo, Arusha, Tanga na sehemu nyingine mbalimbali za Tanzania, wateja wao wakubwa ni wauzaji wa jumla na rejareja na wanaonunua kwa matumizi ya nyumbani.
Aliongeza, "Benki imetupa mchango mkubwa ikiwa ni mikopo ya hadi milioni 400 ambayo imesaidia kuongeza machine za uzalishaji na jenereta linalofanya kazi mara tu umeme unapokatika."

Dada Veronica Manyanga, mmiliki wa saluni ya Cleopatra Excellent beauty iliopo mjini Moshi town, anafurahia uanachama wa...
10/02/2018

Dada Veronica Manyanga, mmiliki wa saluni ya Cleopatra Excellent beauty iliopo mjini Moshi town, anafurahia uanachama wake ndani ya benki ya wananchi. Anahamasisha wadada wenzake na wanawake kwa ujumla wanaopenda maendeleo wanaomiliki biashara ndogondogo ambao wanakutana na changamoto k**a ukosefu wa mitaji ya kutosha, kukosa mikopo ya kujiendeleza kwa sababu ya kutokua na dhamana zinazotakiwa kwenye benki nyingine, wajiunge na benki ya wananchi ili wafurahie tofauti kwenye biashara zao.

"Nilishangaa nimejiunga na benki ndani ya muda mfupi tu nimeweza kupata mkopo ulioniwezesha kuongeza vifaa vya saluni na sasa kwenye saluni yangu natoa huduma zote ikiwemo na kupamba maharusi." Amesema dada Vero. Hivyo amehamasisha wakinamama na vijana kufungua akaunti benki ya wananchi mwanga ili wafurahie huduma kwani mikopo ni rahisi, riba nafuu, upatikanaji wa haraka.

Moja kati ya wafanyabiashara wakubwa mjini Moshi, Bwana Miraji Ali Kidundi almaarufu k**a CHAKITO, mmiliki wa mabasi mak...
09/02/2018

Moja kati ya wafanyabiashara wakubwa mjini Moshi, Bwana Miraji Ali Kidundi almaarufu k**a CHAKITO, mmiliki wa mabasi makubwa ya kusafiria yanaoenda Dar , Arusha pamoja na vituo vya mafuto petroli, dizeli na mafuta ya taa, vinavyopatikana maeneo ya Moshi, Same na Lushoto akielezea uzuri wa Mwanga Community Bank na jinsi ilivyomtoa kutoka mfanyabiashara wa kawaida na mpaka sasa amekua moja kati ya wafanyabiashara wakubwa mjini humo, anaemiliki mabasi ya kusafiria, vituo vya mafuta, kumbi za sherehe pamoja na vituo vya utalii.
"Nimeanza kutumia benki yetu ya wananchi kwa muda mrefu sasa nina zaidi ya miaka kumi na nimeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa tangu nimeanza kufanya hizi biashara.Nilianza kukopa kuanzia milioni 4 za kitanzania na sasa ninaweza kukopa zaidi ya milioni 100. Mkopo wa sasa unafika hadi 400 milioni ambao ndio namalizia kuurejesha.Naipenda Benki yetu kwa sababu haina ubabaishaji kwenye utoaji wa mikopo, pia urahisi wa kufanya malipo ninapotaka kuagioza mzigo pesa zinatumwa kwa wakati kwenda kwa wasambazaji, makao makuu yapo kilimanjaro hvyo ni rahisi kufanya maamuzi. watu wasiangalie jina waangalie ni vitu gani, uaminifu na uwezo gani benki ilionao katika kihudumia wateja wake."
Pia aliongeza kwa kuwaasa wafanyabiashara wakubwa kuwekeza kwenye beni hii na kufurahia matunda mazuri ambayo na yeye yameweza kumfikisha alipo sasa.

Our working cubicle has turned into a monotonous one, asha was always a great co worker ,her sudden death is a great sho...
03/01/2018

Our working cubicle has turned into a monotonous one, asha was always a great co worker ,her sudden death is a great shock to all of us, I'd like to express my deepest sympathies to her family and the whole MCB team 😢

Address

Mwanga New Town
Arusha
255

Opening Hours

Monday 08:30 - 15:30
Tuesday 08:30 - 15:30
Wednesday 08:30 - 15:30
Thursday 09:00 - 15:30
Friday 08:30 - 15:30
Saturday 09:00 - 12:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwanga Community Bank posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category