Elimu ya Fedha

Elimu ya Fedha Consultations in all business and community related issues.

Credit advisory services, business consultations, Investment management advice, School management best practice, entrepreneurship Trainings, Financial education trainings etc.

24/10/2022

TAJIRIKA MAPEMA.

Nakusalimu.
Mimi ni KUMBUAEL KAAYA 0769160382

Naomba usome kuhusu kutajirika mapema.
Biashara za mtandaoni za tajirika mapema zimekua nyingi sana katika zama hizi za utandawazi. Wengi wanaathirika na huu uvumi kwa sababu ya tamaa ya kua Tajiri. Napenda kua Tajiri hata mimi ieleweke hivyo.

Tajirika mapema ni nini? Ni mpango unaoahidi kumfanya mtu kuwa tajiri sana kwa muda mfupi. Ipo mifano mingi sana ambayo hata wewe utakua unafahamu. Swali, je ulishawahi kusikia hao wanaotangaza hiyo mifumo ya kutajirika mapema wakisema wanafanya biashara gani mpaka wapate hizo faida?

Embu fikiri pamoja na mimi mtu anakwambia ukiweka laki moja unapata faida ya elfu 30 kwa wiki, ni biashara gani unafanya upate faida kwa wiki ambayo unatoa gharama zako zote na bado unatoa gawio la elfu 30 kwa wiki kwa mtaji wa laki moja. Taasisi ndogo za fedha zinakukopesha uwalipe riba ya asilimia 3 kwa mwezi, wakufuatilie, kukudai na maform mengi unajaza je hujawahi kujiuliza kwanini hawa matapeli k**a inalipa wasiende kukopa benki warudishe marejesho maana wakopeshaji wanataka riba ndogo tu asilimia 3 sio kubwa?

Nakushauri ukitaka kuwekeza pesa yako mahali hakikisha unapafahamu vizuri. Inakuaje mtu anakueleza habari za namna utapata faida unakubali kirahisi tu unaweka pesa bila hata kua na taarifa za kutosha.

Unachukua mtaji wote unawapa watu wakati mtu aliepewa Hekima nyingi sana na Mungu mfalme Suleimani kwenye Kitabu cha Mhubiri 11:2 Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane; Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi ameshakwambia usiweke mahali pamoja hujui baa gani litakuwepo hata k**a unapafahamu, wewe unampa mtu usiemjua tena pesa zote.

Watu wengi wanalia sana sasa hivi kila mahali wametapeliwa pesa zao, mara mtu anaenda kuchukua mkopo Benki ili awekeze inaliwa pesa unalipa mkopo miaka 10 utakua na afya ya akili kweli wewe? Tunasingizia michango mingi kanisani kumbe ni kwa sababu tumeshaibiwa huko na matapeli.

Katika elimu za muhimu sana nakusahuri uwe nazo ni elimu ya fedha na naomba ukiona pesa zako zinapotea kwa mwendo kasi kuliko zilivyokuja ujue tayari shida mahali.

Kabla ya kuwekeza tafuta elimu au kujua huo uwekezaji unafanyaje kazi. Kua makini na pesa zako. Ukiona unaingia kwenye uwekezaji ambao wewe binafsi hauna utaalamu wake tafuta ushauri na umuombe Mungu usizitegemee akili zako mwenyewe! Nitafute

Karibu.

Mfululizo wa Masomo ya Elimu ya FedhaSomo la PiliMatumizi ya lazima na yasiyo ya lazima.Baada ya kusoma makala ya kwanza...
08/04/2022

Mfululizo wa Masomo ya Elimu ya Fedha
Somo la Pili

Matumizi ya lazima na yasiyo ya lazima.

Baada ya kusoma makala ya kwanza nilipata swali kutoka Kwa watu wawili Moja Kwa maandishi na lingine Kwa njia screenshot yote yalilenga kujua *K**a kipato hakitoshelezi matumizi Yako, unatengaje Akiba?*

Jibu ni hili hapa kwenye somo la Pili,

Katika uandaaji wa bajeti Yako angalia mahitaji yapi ni lazima na yapi sio ya lazima. Hitaji la lazima ni Lile ambalo huwezi kuishi au utaishi Kwa shida usipolipata mfano ni chakula au maji hitaji lisilo la lazima ni vitu k**a pombe au kuhonga.

Hitaji la lazima na lisilo la lazima pia linategemea na kipato Cha mtu, nafasi yake katika jamii au shughuli anazofanya. Mfano kuna mtu kulingana na kazi zake kununua gari ni hitaji la lazima lakini mwingine sio hitaji la lazima kwake hivyo usiangalie Kwa mwenzako ukasema nawe ni hitaji la lazima Ishi maisha Yako.

Ukifika hatua hii ya kuchambua hitaji la lazima na lisilo la lazima (needs and wants) utagundua kuna mianya mingi ya upotevu wa pesa ambayo ukiidhibiti vema unapata pesa nyingi Kwa ajili ya akiba na Uwekezaji.

Mfano Kwa wale tunaofanya kazi mjini Unaweza kuja kugundua hauna sababu ya msingi ya Kila siku kula chakula Cha 6000 na soda 🥤, chai ya 2000 na bado kuna nauli au mafuta ya chombo.

Mahitaji ya lazima na yasiyo ya lazima yanakupa uwanja mpana wa kupunguza mianya ya upotevu wa mapato au sehemu ambazo Unaweza kubana ukapata Akiba.

Kuna wale wa tumia pesa ikuzoee, nakushauri Hakikisha matumizi Yako hayazidi mapato Yako la sivyo utaingia kwenye mikopo isiyo na tija.

K**a unatengeneza laki Kwa mwezi na unakula yote ujue unakula mbegu na hauna bima hata ya wiki. Usisahau kuna likizo, kuumwa na wakati ambao utashindwa kuzalisha utaishije?

Tito 3:14
[14]Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, *kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.*

Mwisho, Andika matumizi Yako yote Kwa ukweli alafu ainisha lipi la lazima na lipi sio lazima au wapi Unaweza kupunguza kidogo na ukapata Akiba.

Asante

Kwa masomo Zaidi Tuwasiliane

Kumbuael Yesaya Kaaya| 0769160382

07/10/2021

AKIBA: MFUKO WA DHARURA

Akiba Ni kiasi cha fedha au kitu kinachowekwa kwa ajili ya matumizi ya baadae. Matumizi haya ya baadae ni muhimu yawe na malengo ambayo mtu anahitaji kuyafikia baada ya muda fulani.

Katika kuweka akiba kuna sababu kuu tatu za kuweka akiba nazo ni Manunuzi au matumizi ya baadae, uwekezaji na dharura.

Katika Makala hii nitaangazia sababu ya kuweka akiba ambayo ni dharura na nataka tuangazie namna ya kuanza kuweka akiba kwa ajili ya dharura;-

Jambo la kwanza: Badili tabia na mfumo wa maisha. Kwenye hili tutazame mifano kadhaa;

Mfano wa kwanza, Usafiri. Angalia k**a ulikua unapendelea kutumia tax kwenda mahali pa kazi au kupanda bodaboda kila umbali kidogo tu jizoeze sasa kutumia usafiri wa umma ili kupunguza gharama za usafiri uziweke kwenye akiba yako.

Mfano wa Pili, Badili mfumo wa kula, kuna wale watu wanaokula Zaidi ya 5,000 kwa mlo mmoja wa asubuhi na hapo hana akiba yoyote. Sisemi usile ila hakikisha unakula na mfuko wako wa akiba unapata kitu, msemo wa mtaani.. usifanyie tumbo tu.

Mfano wa Tatu, Fanya kazi ya ziada. K**a kazi uliyonayo kwa sasa haitoshi jitahidi upate na kazi ya ziada au jambo lingine litakalo kuingizia pesa ili uweze kumudu matumizi yako na kuweka akiba.

Jambo la Pili: Ondoa dhana potofu juu ya umiliki wa pesa na mali. Najua utakua umesikia mtu akipata pesa kidogo tu mara ni Freemason, katoa kafara, mchawi, anapenda pesa na mengine mengi. Hiyo ni dhana potofu juu ya fedha, fanya kazi acha kukaa kijiweni wengine wakipata pesa uwaseme.

Kupenda pesa ni chanzo cha mabaya yote… wengi wanasema pesa ni chanzo cha mabaya na hivyo kunukuu huo mstari vibaya au wengine wanasema ukiwa tajiri uendi mbinguni ni uvivu wa kufanya kazi ndio unafanya uwe na mawazo ya namna hiyo.

Tunafahamu kwa uhakika linapokuja jambo la ghafla au dharura linahitaji mbinu za dharura kulitatua, baada ya kuangazia mbinu ya kutengeneza akiba tuangalie vitu ambavyo vinaweza kuja kwenye maisha yako na vikabadili kabisa matumizi yako ya pesa.

Likitokea janga k**a hili la CORONA ambalo hakuna mtu alikua analifahamu limesababisha vyanzo vingi vya mapato vimehathirika na kupotea kabisa hivyo imekua dharura kubwa kwa mtu binafsi, taasisi, nchi hata dunia. Ukiwa na dharura unaitumia kwenye nyakati k**a hizi na inakusaidia.

Hakikisha dharura inatumika wakati wa dharura sio dharura unaifanya tena mfuko wa matumizi wa kawaida utakua haujafikia lengo la kua na mfuko wa dharura. Kuhusu dharura iwe kiasi gani pangilia mwenyewe. Kwa maoni nitafute.

Elimu ya Fedha--BimaKatika uandaaji wa bajeti yako ya kila mwezi au mwaka kumbuka BIMA.Bima ni mkataba kati ya mtu au ka...
28/09/2021

Elimu ya Fedha--Bima

Katika uandaaji wa bajeti yako ya kila mwezi au mwaka kumbuka BIMA.

Bima ni mkataba kati ya mtu au kampuni na kampuni ya Bima ambao mtu au shirika hupokea ulinzi wa kifedha au kulipwa dhidi ya hasara itakayotokea dhidi ya kile ulichokikatia Bima.

Bima itakusaidia mambo kadhaa ambayo bila bima ungetumia fedha nyingi sana kuyatatua.

Kuna aina nyingi za bima kulingana na kile kilicholindwa lakini hapa nitaje tatu;-

i. Bima ya afya. Hii bima ambayo mtu ananunua ili kupata huduma ya matibabu atakapoumwa kwa kutumia bima.

ii. Bima ya dhidi ya hatari za moto, mafuriko, upepo na majanga yote dhidi ya Jengo. Hii ni kwa ajili ya majengo ukipata janga bima inakufidia kulingana na mkataba wenu.

iii. Bima ya vyombo vya moto. Hii ni kwa ajili ya magari, pikipiki na vifaa vyote vya moto. Birika la kahawa sio chombo cha moto. Hii unafidia kifaa au mtu atakae pata tatizo akiwa na kile kifaa.

Bima itasaidia pale unapopatwa na janga lolote iwe kuumwa, ajali na madhara mengine bima watafidia hasara ya kifedha ambayo ungeingia kwa kulipa keshi k**a hauna bima. Bima itakusaidia kudhibiti matumizi yako ya pesa kwenye majanga k**a hayo.

Pakua Kisomo App https://kisomo.co.tz/download ujifunze zaidi

Elimu ya Fedha - Wanunuzi jihadharini (Makala ya Pili)Habari za leo,Karibu tena kwenye mfululizo wa masomo ya elimu ya f...
27/09/2021

Elimu ya Fedha - Wanunuzi jihadharini (Makala ya Pili)

Habari za leo,

Karibu tena kwenye mfululizo wa masomo ya elimu ya fedha, leo tuangalie mambo gani mnunuzi anahitajika kuyafanya kabla hajafanya manunuzi kwa lengo la kuzingatia mpango wake wa fedha k**a umeenda sahihi kwa kununua vitu vilivyoko kwenye mpango, k**a hazipo kwenye mpango viwe vinahitajika na ni manufaa kuvinunua. Kumbuka manunuzi yanaathiri Kipato chako.

Mambo matano ya kuyazingatia ni miongoni mwa haya;-

i. Jipe Muda wa kutafakari. Usilazimike kununua kwa haraka bila kufikiri kwani hiyo bidhaa itakuwepo tu sokoni hata kesho na siku nyingine. Kaa tafakari angalia bei unayolipa kulingana na umuhimu na je k**a kuna muuzaji mbadala mwenye bei nzuri zaidi.

ii. Fikiria sababu za kununua. Angalia k**a hilo ni hitaji la lazima ua sio lazima, usinunue kuwafurahisha watu wengine wakuone nawe wa maana huku unapigika hapana. Hiyo bidhaa haimaanishi ndio chanzo cha furaha yako.

iii. Usinunue kitu usichokielewa. Mfano mzuri ni zile dawa za kwenye magari zinatibu magonjwa yote, unaelezewa mpaka hukumbuki alipo anzia, usinunue kitu k**a huelewi. Mfano mwingine kwa watu wa maofisi usinunue vifaa vya kazi ambazo uwezo wake ni mkubwa sana kulingana na mahitaji ya kazi kwa sababu tu vimesifiwa mfano mimi unanikuta na laptop sawa na inayotumika na watu wa sayansi ya anga si utanishangaa ya nini hiyo.

iv. Fikiria gharama. Hapa nazungumzia pesa unayolipa lakini pia nazungumzia ile ukinunua kitu cha laki moja je hiyo laki moja ingeweza kununua nini kingine chenye thamani zaidi au unachokihitaji, gharama ya kukikosa hicho kwa sababu umenunua hiki inaitwa opportunit cost kwa kimeru.

v. Ongea na mwenzako. K**a umeoa au kuolewa kabla hujafanya manunuzi hususani makubwa ambayo yanaathiri mpango wenu, mshirikishe mwenzako kujua maoni yake na je k**a yeye anajua mbadala mzuri zaidi. K**a hujaoa wala kuolewa najua utakua na rafiki yako ambae mnashirikiana mambo flani flani, mshirikishe huyo kujua maoni yake pia na akushauri k**a ni kitu chafaa au kuna mbadala.

Sizuii watu kununua kwa sababu kutumia pesa ndio sababu hasa ya kuzitafuta ili ukiwa una uhitaji utumie nnachotaka hapa ni uende kwa umakini na kwa kutumia mpango. Kila kitu unachokitaka kiweke kwenye mpango usiseme hiki siweki kwa sababu hii na hii, weka ili ujue namna kitaathiri mpango wako na namna bajeti yako itafanana ukikiweka.

Fanya manunuzi yako kwa weledi kwani yanaathiri kipato chako. Najua ulishasikia au hata wewe imekutokea unapata pesa lakini hujui hua zinaenda wapi, sehemu mojawapo ukiachana na kuibiwa ambayo sio asilimia kubwa ni kwamba unafanya MANUNUZI HOLELA bila MPANGO. Kila muuza bidhaa akikufikia unanunua kwa kumuonea huruma lakini huionei huruma pesa yako uliyoipata kwa jasho.

(Leo ni birthday ya mke wangu Ishengoma ambae tunashauriana kuhusu manunuzi)

Nilikuita Rafiki, sasa ni Mke ambae ni Rafiki Yangu, Mimi na wewe ni kitu Kimoja kwa hiyo leo ni Birthday Yetu. Happy Bi...
27/09/2021

Nilikuita Rafiki, sasa ni Mke ambae ni Rafiki Yangu, Mimi na wewe ni kitu Kimoja kwa hiyo leo ni Birthday Yetu. Happy Birthday My Lovely Wife. Hapiness Ishengoma

24/09/2021

Elimu ya Fedha - Wanunuzi jihadharini (Makala ya kwanza)

Habari za leo,

Karibu tena kwenye mfululizo wa masomo ya elimu ya fedha, leo tuangalie jinsi gani mnunuzi anahitaji kujiadhari wakati wa kufanya maamuzi ya kununua ili kuhakikisha anafanya manunuzi kulingana na mpango wake wa fedha yaani bajeti.

Kabla ya kuangalia vitu vya kujiadhari navyo niweke mambo mawili mbele yako ambayo unahitaji kuyajua kabla ya kufanya manunuzi;-

Matangazo ya bidhaa ni mengi sana wakati huu kuliko wakati mwingine wowote. Kwa siku mtu anakutana na matangazo zaidi ya 100 ya bidhaa mbali mbali kuanzia redioni, TV, facebook, Insta, Twitter, simu, vipaza sauti mijini na mabango barabarani. Yote hayo yanafanyika na kila mmoja ni vita ya kuipata hiyo pesa yako. (watu wa marketing tulieni nafanya kazi yangu)

Mawakala wa mauzo ni wengi sana siku hizi. Wakati unamsikiliza wakala usisahau lengo lake ni kuuza na sio kukupa wewe maelezo na elimu. K**a inafaa kua na wakala wako wa manunuzi pia k**a wauzaji walivyo na mawakala. (nitafafanua cha kufanya kwenye makala ya pili).

Mbinu nne za wauzaji unahitaji kujiadhari nazo.

Ukikutana ana kwa ana na muuzaji (pesonal selling). Najua umeshakutana na watu wa mauzo/sales hivyo siongei sana unajua ilivyo ngumu kuchomoka bila kununua k**a hauna mpangilio wa mambo yako. Umeshawahi kukutana na watu network marketing wewe? Forever living, Qnet na mengine ukachomoka?

Mikopo ya bidhaa (Ofa, punguzo, nunua sasa lipa baadae, dunduliza). Sababu kubwa ya ofa, punguzo na nunua sasa lipa baadae ni ili usiulizie bei ya kitu maana wameshakuwai kua ni ofa na kumbuka mara nyingi wewe hujui bei halisi ya hiyo bidhaa. Kabla ya kukubali hizi ofa za mauzo chunguza kwanza k**a watu wa BEROYA ambao huchunguza maandiko kabla hawajakubali (matendo ya mitume 17:11). Unavyodunduliza anaendelea kufanyia pesa yako kazi na bado umenunua ghali.

Matangazo kwa njia ya vyombo vya habari. Hii inatengeneza jina la bidhaa fulani kichwani mwako inaitwa brand ili ukiliona usianze kuuliza sana kwani tayari una taarifa. Mtu akikusikia mara kwa mara kuna uwezekano mkubwa kua atakukumbuka. Najua hata wewe unajua misemo mingi sana ya makampuni... Pesa ni Mpesa, yajayo yanafurahisha.... ile misemo inakaa kichwani kiasi kwamba inakunong’oneza wakati mwingine kwenda kununua hata k**a ulikua hutaki.

Mpangilio wa bidhaa maeneno ya kununua (product positioning). Picha zinazooneshwa na sifa zitolewazo za bidhaa husika. Ukienda madukani au sokoni angalia walivyopanga vitu hususani supermaket havijapangwa hivyo bahati mbaya bali wamefanya utafiti juu ya tabia za wanunuzi hivyo kua makini na mpango wako wa matumizi ya fedha

Kila mtu anawajibika kwa manunuzi yake. Kumbuka ukishanunua na ukijikuta umetumia nje ya mpango wako wa manunuzi na umezama kwenye madeni anaewajibika ni wewe na sio muuzaji, hivyo katika mfululizo wa elimu ya fedha fikiria pia namna unavyofanya manunuzi na sio bajeti peke yake itakusaidia. Bajeti ni nyenzo tu lakini mtekelezaji ni wewe na unatakiwa usimamie kwa uangalifu

Kumbuka: sikuambii usinunue hapana, ila nakuambia fanya manunuzi kulingana na mpango wako wa matumizi

Usikose makala ya Pili ambayo itakuletea miongozo mitano ambayo ikizingatiwa inakuhakikishia maamuzi sahihi ya manunuzi

SABABU KUU TATU ZA KUWEKA AKIBA Dharura. Tunaweka akiba kwa sababu tunajua kuna dharura itatokea na utahitajika kuwa na...
22/09/2021

SABABU KUU TATU ZA KUWEKA AKIBA

 Dharura. Tunaweka akiba kwa sababu tunajua kuna dharura itatokea na utahitajika kuwa na akiba, dharura sio kwamba hazijulikani hapana, usichojua ni itakuja lini na kwa kiwango gani. Kuna watu wakipata dharura na wana akiba awaitumii eti kwa sababu ni akiba, ujue hujui sababu ya kuweka akiba.

 Manunuzi/malipo. Tunaweka akiba kwa ajili ya kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali na malipo ikiwepo ada za shule, vifaa vya nyumbani, ardhi na vitu vngine vingi.

 Kukuza utajiri/kipato. Hapa ni pale unapoweka vitu akiba lakini katika hali ya kuzalisha. Unanunua shamba au nyumba ambayo baadae itapanda bei au utakua unapata kodi na kukuza kipato chako. Unaweka pesa benki kwa riba au unanunua hisa za makampuni ili upate faida baada ya kipindi Fulani cha muda.

Hizi ndizo sababu kuu tatu za kuweka akiba, ongezea za kwako

Vitu  vikuu vinne ambavyo unahitaji kujifunza Kuhusu Fedha.i. Kazi. Lazima ujifunze na kuwafundisha wengine kua njia pek...
22/09/2021

Vitu vikuu vinne ambavyo unahitaji kujifunza Kuhusu Fedha.

i. Kazi. Lazima ujifunze na kuwafundisha wengine kua njia pekee ya kupata pesa na sahihi ni kufanya kazi na sio kupewa pesa na watu au kusubiria misaada, serikali au mchezo ya bahati nasibu. Wafundishe watoto kufanya kazi usiwadekeze kiasi cha wewe kuwawekea wafanyakazi wa kuwasaidia kila kitu katika maisha yao, unawasaidia kila kitu bure. Utadhani unawajenga lakini unawaharibu.

ii. Akiba. Wafundishe watoto au hata vijana au wewe binafsi umuhimu wa kuweka akiba na mbinu nzuri za uwekeaji akiba ikiwa ni pamoja na kuweka malengo ya kuweka akiba kila siku au mwezi au wakati wowote kulingana na upatikanaji wa kipato chako. Akiba ni Muhimu.

iii. Matumizi. Lazima ujifunze namna ya kufanya matumizi ya pesa zako. Lazima ujue ilivyo vizuri kununua vitu kwa pesa yako mwenyewe sio unaweka akiba tu alafu hutaki kutumia hiyo pesa, utakua hauna faida na uwekaji wako wa akiba. Jifunze kutumia pesa kwa mpango maalum

iv. Kutoa. Lazima ujifunze kutoa pesa, zawadi na vitu kwa wengine. Unapokua na pesa ni fahari sana kuwapa watu k**a ambavyo ni vizuri kupokea pesa kutoka kwa watu wengine ikiwepo serikali, wafadhili na mashirika kadhaa. Fikiria ilivyo vizuri kupokea je si Zaidi sana kwa yule anaetoa? Ukitoa inakupatia Baraka lakini pia inakuongezea morali na motisha ya kutafuta pesa Zaidi kwa ajili ya mahitaji yako na ya watu wengine.

Katika kujifunza kuhusu pesa ni lazima tujifunze haya mambo yanayohusiana na pesa.

Think about how beautiful its discovering the hidden potential or asset that is at your disposal and can be used right a...
02/09/2021

Think about how beautiful its discovering the hidden potential or asset that is at your disposal and can be used right away to increase your income!

Challenge yourself of the time you have per week and how many hours are real used for income generation.

Example, If your are employed formally that is 8 Hours a day, which totals to 40 hours in five days or 45 hours in six days.
The week has 168 hours, you are using only 24-27% of the time in income generating activities and the remaining time is spending time.

The question is, How can 27% of your time generate the income sufficient to cover 100% of the time? I know 20/80 rule but does that apply to you?

Think about your time management priorities!
............................................................................
Learn and Unlearn Financial Education on by George Akilimali Kisomo App

Uhuru Wa kifedhaMakala ya TanoKuna vitu utagundua havizalishi kwako wala havina tena kazi kwako ila vinakuingiza Gharama...
27/08/2021

Uhuru Wa kifedha

Makala ya Tano

Kuna vitu utagundua havizalishi kwako wala havina tena kazi kwako ila vinakuingiza Gharama ya kuhodhi nafasi

mfano, una store ya kuweka vitu chakavu na imejaa na hukitumii tena, piga Hesabu za hiyo nafasi ungeifanyia nini visingekuepo?

Funga macho Wape watu wengine, jifunze kutoa misaada, hata mwanao akiwa na midoli 3 mfundishe kugawa mingine kwa wale wasio nayo.

Usijenge stoo ya bati 8 imejaa vitu chakavu tu wakati ungeigeza banda LA Kuku wangekaa Kuku mia (100). Ukiwatunza vizuri ukauza kwa bei za pale kijijini kwetu Nasholi Kikatiti 10,000 una Laki, kumbuka utapata mayai, Nyama n.k

Kua mbunifu, umeacha eneo LA nusu ela LA kuchungia mbuzi na unao wawili na punda mmoja, ni matumizi mabaya ya rasilimali. Ungelitumia vizuri hilo eneo kwa kuongeza mifugo au kulimega ukaweka hata matuta ya viazi.

Sizuii Uhuru wako ila nakupa posibo k**a walimu wanavyotoaga wakati Wa mitihani.

Uhuru Wa kifedha (Financial Freedom)Makala ya NNE.Baada ya kuona maana ya Uhuru Wa kifedha, tukaangalia bajeti, namna ya...
26/08/2021

Uhuru Wa kifedha (Financial Freedom)

Makala ya NNE.

Baada ya kuona maana ya Uhuru Wa kifedha, tukaangalia bajeti, namna ya kupata Uhuru kwa kutafuta utofauti kati ya mahitaji yako na kipato chako,

Moja ya njia tulisema ni kuangalia Mali uliyonayo na haizalishi kwa sasa.

Mali ambayo Nataka tuiangalie kwa ufupi sana Leo ni kipaji chako

Kila MTU ana kipaji, kila MTU ana Uwezo Wa kutumia hicho kipaji kujipatia kipato cha ziada.

Angalia ni kipaji gani unacho na ona namna ya kukifanya kua Pesa, kizalishe pesa. Kumbuka hakitaanza kuzalisha mpaka ujitangaze.

Kila MTU anayo Talanta alaiyopewa labda tu ya kwako umeifukia chini ndo maana hujui k**a unayo lkn kila MTU anayo.

Ukigundua una kipaji ambacho hukitumii kuingiza Pesa kwa sasa Anza kukitumia.

Usiwe k**a wale watu walisoma Biblia kua usitumikie mabwana wawili basi toka hapo anakomaa na kikazi chake kimoja hata k**a hakilipi, Fanya kazi nyingi kadri unavyoweza.

Tumia vipaji vyako vyote.

Kila MTU atadaiwa kulingana na alivyopewa, k**a umepewa vingi vitahitajika vingi kutoka kwako. Usishangae mahitaji yako yapo juu sana, umepewa vingi Ndio maana vinahitajika vingi pia.

Tumia Uwezo wako wote vizuri, usibanie Uwezo kusema huu nitatumia wakati Mwingine Hapana, wakati uliokubalika ni sasa.

Kadri unavyokitumia kipaji chako ndivyo unakua bora zaidi k**a misuli unavyofanya mazoezi mengi ndivyo unakua bora zaidi.

Tumia kipaji chako upate Uhuru Wa kifedha, usikubali kukaa na rasilimali ambayo haizalishi na wewe huna Uhuru Wa kifedha.

Utukutane wakati Mwingine.....

Address

Arusha

Opening Hours

Monday 08:00 - 18:00
Tuesday 08:00 - 18:00
Wednesday 08:00 - 18:00
Thursday 08:00 - 18:00
Friday 08:00 - 18:00
Saturday 08:00 - 19:00

Telephone

+255769160382

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elimu ya Fedha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Elimu ya Fedha:

Share