20/07/2024
SENTENSI 8 ZITAKAZOKUZA UWEZO WAKO WA MAHUSIANO YA KIJAMII:
1. "Kutatua jambo haraka, kuwa muungwana kwa mtu anayehusika na mkali kwa tatizo lenyewe"
Unapokumbana na changamoto au migongano, chukua mtazamo unaojali hisia na maoni ya wengine na kuwa muelewa. Unapoteza nguvu kwa kumwia mkali mtu aliyekosea wakati jambo la msingi ni kutatua tatizo.
2. "Dhania kuwa kila mtu alitumwa kukufundisha kitu."
Tazama kila fursa ya kujadiliana jambo na wengine k**a fursa ya kukua na kujitambua zaidi. Mchukulie kila mtu unayekutana naye k**a mwalimu, ukitambua kuwa kila mtu ana mambo ya kukufundisha na mtizamo wa kutoa. Kuwa tayari kukubali kutokuelewana na wengine. Kuwa mdadisi.
3. "Kuwa na Vituo Unapoongea + Tazama Machoni = kujiamini."
Jenga tabia ya kuwa na vituo(pozi) kabla ya kuzungumza, hii itakupa muda wa kupanga mawazo yako na kuwa na uwasilishaji mahiri. Kutazama machoni hukuwezesha kuonesha kujiamini na kuwa mkweli.
4. "Jifunze Jinsi ya Kuwafanya Watu Wajisikie Kuwa Muhimu."
Wafanye watu wajisikie kuonekana kwa kuwapa usikivu wa kweli na uwepo wako. Hakikisha wanajisikia kuwa wamesikilizwa kwa kuwasikiliza na kuuliza maswali ya kutaka kuelewa zaidi. Kuwa na bidii ya kukumbuka taarifa za muhimu za maisha yao, mambo wanayopenda na uzoefu wao.
5. "Sauti Bora Kabisa kwa Mtu ni Ile ya Jina Lake, Hivyo Likumbuke."
Kukumbuka na kutumia jina la mtu huashiria heshima, utambuzi, na uthibitisho ambao hutengeneza hali ya kuheshimiana na kuthaminiana.
6. "Kuwa na nia njema/chanya kabla ya kutoa mrejesho."
Kabla ya kutoa mrejesho chanya wenye manufaa, ni muhimu kuhakikisha kuwa watu wengine wanajisikia kuwa unawajali na unajali mafanikio yao ya muda mrefu. Hii husaidia kuonesha nia chanya.
7. "Sifia Hadharani. Kosoa faragha."
Kutambua hadharani hujenga utamaduni wa kuthamini na kuwatambua wengine. Lakini kwa kutoa mrejesho chanya unaojenga kwa faragha, kwa heshima huunda mazingira yaliyo salama kwaajili ya majadiliano na kukua bila kuhofia kuhukumiwa na kudhalilishwa.
8. "Mategemeo ambayo hayajaelezwa ni shina/chanzo cha chuki."
Jitahidi kuelezea matarajio yako kwa namna inayoeleweka na kwa heshima la sivyo tegemea kutoelewana, chuki, na mfarakano kwenye mahusiano.
Asante kwa kusoma na kushea 🙏🙏🙏