11/12/2025
`USIFANYE KOSA HILI`
_____________________
✓✓Usitoe matumaini kwa mtu k**a hauna
uwezo kwa wakati huo/hauko tayari kumpa pesa yako
(Respond Promptly, Be clear).
✓✓Kuna watu wengi wameingia kwenye mtego wa kutoa
pesa hata pale ambapo wanakuwa wamebakiwa
nazo kidogo kwa sababu ya huruma.
✓✓Kumbuka kuwa, unaweza kuwa na huruma, ila k**a
hauna uwezo wa kuihudumia huruma kipesa,
usijilazimishe.
✓✓Mtu anapokuomba pesa, huwa anatarajia unaweza
kusema NDIO au HAPANA.
✓✓ Ukijijua kuwa uko kwenye
changamoto za kipesa, usimpe mtu matumaini ya
kuwa unaweza kupata na kumpatia baadaye.
Achana na majibu k**a “Ngoja niangalie kwanza”
,
“Tuombe Mungu nitakuchek baadaye”
“Kuna hela
naisubiria, nikipata nitakupatia”.
✓✓Kwa tafiti zangu ndogo ni kuwa, mtu ukishampa jibu
lolote la matumaini, kwanza anaacha kutafuta
kwingine kote na pili anatarajia kuwa lazima utampa,
hii ndio maana lazima atakusumbua tu.
> Ushawahi fanya hili kosa k**a Mimi 🙆??