Dattieko Investment

Dattieko Investment Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Dattieko Investment, Arusha.

   with .repost・・・Wanawake Nane kutoka sekta mbalimbali wametunukiwa Tuzo za Malkia wa Nguvu Kanda ya Kaskazini katika h...
02/06/2026

with .repost
・・・
Wanawake Nane kutoka sekta mbalimbali wametunukiwa Tuzo za Malkia wa Nguvu Kanda ya Kaskazini katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya Jukwaa la Malkia wa Nguvu.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, Mkurugenzi wa Utalii Tanzania, Thereza Mugobi amesema jukwaa hilo limeendelea kuwa chachu ya uwezeshaji wa Wanawake kwa kuwapa fursa ya kuonesha uwezo wao na kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia sekta mbalimbali.

Amesema Mwanamke anapopewa nafasi huleta mabadiliko makubwa si kwa maisha yake binafsi pekee, bali pia kwa familia na Jamii kwa ujumla.

Washindi wa tuzo hizo ni Leah Pantaleo Asenga (Huduma na Chakula), Dativa Koyanga (Kilimo Biashara), MWEDO – Maasai Women Development Organization (Afya na Ustawi wa Jamii), Mariam Chuma Kobelo (Utumishi Bora Sekta ya Umma), Miriam Oscar Kaaya (Elimu, Malezi na Ulinzi wa Mtoto), Christine Mwakatobe (Diplomasia ya Uchumi na Utalii), Carolyn Kandusi (Mapinduzi ya Kidigitali na Maendeleo ya Jamii) pamoja na Mary Msonsa (Biashara, Uvumbuzi na Ajira).


Humbled 🙏🏽

01/06/2026

Malkia Wa Nguvu

Tunaanza Jumatatu kwa furaha na shangwe.
Tunaanza mwezi wa Sita kwa furaha na shangwe Celebrating our wins!








🌱 Wiki ya Mazingira Duniani 2026 🌱Dattieko Investment Limited tunajivunia kuwa sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Mazingir...
01/06/2026

🌱 Wiki ya Mazingira Duniani 2026 🌱

Dattieko Investment Limited tunajivunia kuwa sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani 2026.

Kupitia suluhisho zetu za greenhouse, irrigation systems na dam liners, tunaendelea kuhamasisha matumizi bora ya maji, uhifadhi wa mazingira na kilimo endelevu kwa maendeleo ya sasa na vizazi vijavyo.

📅 01 – 06 Juni 2026
📍 Jakaya Kikwete Convention Center

“Kilimo Bora, Kesho Iliyobora.”

Karibu ujifunze, ujionee teknolojia za kisasa za kilimo na tushirikiane kujenga mazingira endelevu.

IrrigationSystems DamLiner SustainableAgriculture 🌍🌿

   with .repost・・・DATIVA KOYANGA Chozi lililobadilika ladhaMiaka sita aliishi ndani ya ndoa iliyompa chozi lenye ladha y...
31/05/2026

with .repost

・・・
DATIVA KOYANGA Chozi lililobadilika ladha
Miaka sita aliishi ndani ya ndoa iliyompa chozi lenye ladha ya sukari. Kwa nje alionekana mwanamke mwenye furaha, mwenye juhudi na mwenye ndoto kubwa, lakini ndani ya moyo wake alikuwa akibeba maumivu makubwa yasiyoelezeka.

Alivyotoka kwenye ndoa wengi walizani ndiyo mwisho wake ila ulikuwa mwanzo wa kuzaliwa DATTIEKO COMPANY LTD, kampuni ya teknolojia ya kilimo (Agritech) iliyopo Arusha, Tanzania akitoa suluhisho za kisasa za kilimo k**a greenhouse technology, mifumo ya umwagiliaji wa matone (dripline), rain pipes, dam liners pamoja na vifaa vya ufugaji nyuki na samaki.

hadi sasa Zaidi ya wakulima 360 tayari wamehitimu mafunzo hayo, huku zaidi ya 90 kwa mwaka wakipata nafasi ya kuendelea kujifunza na kujiendeleza.

30/05/2026



・・・
DATIVA KOYANGA
Chozi lililobadilika ladha
Miaka sita aliishi ndani ya ndoa iliyompa chozi lenye ladha ya sukari. Kwa nje alionekana mwanamke mwenye furaha, mwenye juhudi na mwenye ndoto kubwa, lakini ndani ya moyo wake alikuwa akibeba maumivu makubwa yasiyoelezeka.
Alivyotoka kwenye ndoa wengi walizani ndiyo mwisho wake ila ulikuwa mwanzo wa kuzaliwa DATTIEKO COMPANY LTD, kampuni ya teknolojia ya kilimo (Agritech) iliyopo Arusha, Tanzania akitoa suluhisho za kisasa za kilimo k**a greenhouse technology, mifumo ya umwagiliaji wa matone (dripline), rain pipes, dam liners pamoja na vifaa vya ufugaji nyuki na samaki.

hadi sasa Zaidi ya wakulima 360 tayari wamehitimu mafunzo hayo, huku zaidi ya 90 kwa mwaka wakipata nafasi ya kuendelea kujifunza na kujiendeleza.

29/05/2026

MABADILIKO YA TABIANCHI..

Katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabianchi, usimamizi bora wa maji si chaguo tena bali ni hitaji.
Kufunga mifumo bora ya umwagiliaji kunasaidia kutumia maji kwa ufanisi, kupunguza upotevu, kuongeza uzalishaji wa mazao na kuhakikisha kilimo kinaendelea hata wakati wa ukame.

Kila tone la maji lina thamani. Tuchague teknolojia sahihi za umwagiliaji ili kulinda rasilimali zetu za maji na kujenga kilimo chenye tija na himilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Sisi tunafunga mifumo bora ya umwagiliaji na vifaa vyetu ni bora na imara.
Wataalamu waliobobea wapo kukuhufumia.

Karibuni sana wakulima wetu.

28/05/2026

Hifadhi Maji, Linda Mustakabali wa Kilimo Chako! 🌱
Mifumo yetu ya Dam Liner huwasaidia wakulima kuhifadhi maji kwa ufanisi kwa ajili ya umwagiliaji, mifugo, na kilimo endelevu.
✔ Imara na ya Ubora wa Juu
✔ Suluhisho la Uhifadhi wa Maji
✔ Inafaa kwa Kilimo cha Kisasa
Ubunifu katika Kilimo, Ukuaji Endelevu

Address

Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dattieko Investment posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share