11/05/2026
π βUSIWEKE MAYAI YAKO YOTE KWENYE KAPU MOJAβ
Huu ni msemo maarufu unaohusishwa na Aesop (Aesopβs Fables), ukiwa na maana ya kutogawa hatari zako zote sehemu moja.
π Katika biashara ya forex, mtaji ni kitu kisichoepukika, lakini muhimu zaidi ni jinsi unavyoutumia.
Tunashauriwa kuwekeza pesa ambayo tuko tayari kuipoteza bila kuathiri maisha yetu ya kila siku.
π Ukweli ni kwamba, mwanadamu ana emotional attachment kubwa sana na pesa.
Na tofauti ya forex na kazi nyingine ni hii:
π Kwenye kazi ya kawaida, siku mbaya maana yake hujauza au hujapata wateja
π Lakini kwenye forex, siku mbaya maana yake ni hasara ya moja kwa moja ya pesa
Hii ndiyo sababu risk management ni muhimu sana.
π Kabla hujaingia sokoni:
- Hakikisha una emergency fund ya angalau miezi 6
- Usiguse pesa ya basic needs (chakula, kodi, maji, umeme)
- Usitumie pesa ya majukumu muhimu ya maisha
π Na muhimu zaidi, βPay yourself firstβ β concept hii imeelezwa sana kwenye kitabu *The Richest Man in Babylon* cha George S. Clason.
π Pia kwa elimu zaidi ya maamuzi ya kifedha, unaweza kujifunza kitabu *Money Formula* kilichoandikwa na Joel Arthur Nanauka
π
π Kabla ya kuingia kwenye biashara ya forex, hakikisha umejipanga kifedha na umeelewa hatari zake vizuri.
# SMFU # TRADE SMARTER NOT HARDER