03/08/2023
🔴😁 Mabibi na Bwana, amerudi tena Burundi, kwa mara yake ya pili.
===============
Muigizaji huyo wa kitanzania, aliwasili hapa nchini, juzi, ijuma nne. Alikuwa ametokea nchini Congo, alipokuwa akishiriki kwenye kazi zake mbalimbali za .
Kesho tarehe 4 Agosti 2023, Kicheche atakuwa na sherehe yake aliyoiita “ UPENDO party” pale uzuri beach , mjini Bujumbura, kwa ajili ya kuwafurahisha na kuwashukuru warundi kwa Upendo walio muonyesha, kipindi alipofika Burundi kwa mara yake ya kwanza. Hayo na mengine aliyazungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, leo tarehe 03/8/2023.
🔹 "Nimerudi kwa mara yangu ya pili Burundi kwa ajili ya kuwashuru wapenzi wa kazi zangu. Siwezi nikarudi Tanzania bila kupita hapa na Kufanya nyingine shoo. Hii ni party ya kuwashukuru mashabiki zangu kwa upendo walio nionyesha".
🔹Kiingilio itakua ni elfu kumi, sehemu ya kawaida na elfu ishirini, VIP . Hii ni kwa wote wanaopenda kucheka!!
Je,Utakuepo?