20/01/2025
*📃 SUJUDU YA KUSHUKURU*
السـ❓ـؤال
*⚠️naam ..je inafaa kusujudu kwa kumshukuru Allah juu ya jambo flan ulilotekelezewa na Allah ?*
الجـ✅ـواب
*🎙️Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz*
*✅ Sujudu ina sujudu iliowekwa katika Shari´ah. Akibashiriwa kitu chenye kumfurahisha, mambo ya waislamu kufunguka, waislamu kushinda dhidi ya maadui wao au chenginecho cha kumfurahisha, basi atamsujudia Allaah hali ya kumshukuru. K**a mfano wa sujudu ya swalah. Atasema:*
*سبحان ربي الأعلى*
*“Ametakasika Allaah, Aliye juu, kutokamana na mapungufu.”*
*✅ Na ataomba du´aa ndani ya sujudu yake, kumhimidi Allaah, kumsifu kwa kheri aliyopata. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimsujudia Allaah hali ya kumshukuru anapojiwa na kitu cha kumfurahisha.*
*✅ Wakati [Abu Bakr] as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) alipobashiriwa juu ya kuuawa kwa Musaylamah alimsujudia Allaah kumshukuru. Wakati ´Aliy (Radhiya Allaah ´anh) alipompata mwombozi katika wauliwaji wa Khawaarij alimsujudia Allaah akimshukuru.*
*📚 Majmuu´-ul-Fataawaa (11/424)*