31/01/2026
KWA NINI IRANI INAPIGWA VITA DHIDI YA MATAIFA YA MAGHARIBI NA NCHI ZA KIARABU?
Jibu lipo hapa...
Turudi nyuma kidogo mpaka mwaka 1979, kipindi hiki ndio Iran ilifanya mapinduzi na kuwa taifa la kufuata itikadi za Kishia.
Wakati mapinduzi yanafanyika Iran Gen Saddam Hussein Al Tikrit alikuwa makamu wa rais wa Iraq na wakati huo Kiongozi wa Iraq alikuwa Gen Al Bakr, Saddam alimpindua Al Bakr 1979.
Mwaka mmoja nyuma...
Mwaka 1978 wanafunzi wa vyuo vikuu vya Teheran waliandamana hali iliyomfanya Mfalme au Shah Muhammed Reza Khan Pahlav kuikimbia nchi na kwenda kuishi Misri ambako Rais wa nchi hiyo Colonel Annuar Al Sadat alimpa hifadhi kwakuwa mke wa Shah alikuwa ni bint mfalme wa mfalme Farouk wa Misri ambaye alipinduliwa na Jeshi chini ya Umoja wa vuguvugu la Free Officers Corps ukiongozwa na Maj Gen Muhammad Negouib na Col Gamal Abdul Nasser.
Shah alipoondoka alikabidhi serikali yake kwa Wazir Mkuu wake Duktoora Shapur Bakhtiar, serikali hii ilikumbana na vikwazo vingi ikiwemo maandamano na migomo hadi pale Ayatollah Khomein aliporudi toka Ufaransa na siku hiyo hiyo kutangaza kuundwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Serikali hizi yani ya Duktoora Shapur Bakhtiar na ya Ayatollah Rohallah Khomein zilipingana hadi pale jeshi la nchi hiyo Pasdaran walipoamua kumuunga mkono Ayatollah Khomein.
Asubuhi yake Wanafunzi kutoka Qum na Teheran waliuvamia ubalozi wa Marekani na kuwashikilia mateka wanadiplomasia wote.
Hichi ndicho kilichomkosesha kura Rais Jimmy Carter wa Marekani na kusababisha kuchakuguliwa kwa Rais Ronald Regan.
Jaribio lililofanywa na Marekani kuwakomboa mateka hao lilishindwa baada ya helicopter mbili zilizobeba makomando wa Marekani kugongana na kuwaka moto katika anga ya Iran.
Baada ya hapo Iran iliwatawanya mateka hao mmoja mmoja katika nchi nzima na kufanya jaribio la kuwaokoa kuwa gumu.
Tujirejeshe Iran Sasa...
Mpaka miaka ya 60 Iran ilikuwa inaitwa Persia au kwa kiswahili Uajemi, Na hii ilitokana na Quraan kuwa Allah SW ameumba makabila mawili tu, Waarabu na wasiokuwa waarabu(au al ajemi).
Waajemi ndio watu waliohamia Ulaya baadae, hata lugha ya kiirani haifanani na kiarabu ingawa inaandikwa kwa alfabeti za kiaarabu, na imo katika orodha ya lugha zinazoitwa indo aryans language.
Kwahiyo...
kwakutambua hili Ilipofika miaka hio baada ya mapinduzi Iran ilibadilisha jina lake kutoka Persia(yani Uajemi) na kuitwa Iran au nchi ya wa Aryans.
Utakumbuka pia Hi**er alisema Ujerumani si wayahudi bali ni wa Aryans akichukulia maandiko ya Biblia kuwa baada ya Cain kumuua Abel alikimbia akaenda katika nchi nyengine na kule akatwaa mke, kwahiyo hao watu aliowakuta hata kutwaa mke ndio wa Aryans.
Katika vita ya Iran dhidi ya Iraq (Gulf war) ambapo nchi hizi mbili zilipigana kutokana na mgogoro wa muda mrefu wa Shat al Arab, Iraq ikiongozwa na Gen Saddam Hussein al Tikrit wakati huo ndio kwanza amechukuwa madaraka akauchukulia uundwaji wa Jamhuri ya kiislamu k**a udhaifu, akaivamia Iran na kuzikalia sehemu zote zenye waarabu za Iran akitaraji kuungwa mkono nao (Iran ina mikoa miwili na visiwa vingi kwenye ghuba ya uajemi ambavyo vinaishi waarabu).
Wakati huo Saddam aliungwa mkono na nchi zote za kiarabu, Israel, Ufaransa na Uingereza ambao hawakupata chochote kutokana utawala mpya wa kiislamu.
Saddam na Saud Arabia ambao wana idadi kubwa ya waislamu wa shia walihofia yaliyotokea Iran kwa mfalme kupinduliwa yasije yakawakuta na wao hivyo wakaona waipige vita Serikali mpya ya Iran ili kuzuia mapinduzi na kwao yasitokee, hapa ndio uadui wa pili kati ya Iran na nchi za kiarabu ulipoanza.
Rise
Call now to connect with business.