Achieve Finance

Achieve Finance At Achieve Finance Ltd, we strive to help people ACHIEVE their goals – whatever those maybe, through management of their Money. Achieve Finance Ltd.

Following our page means you become part of our VISION: Creating a financial literate Society; where we achieve our lifetime financial goal and create a positive future not just for ourselves, but for the families, society and the Nation, in a sustainable fashion. Together we help you live your life abundantly as you design the tomorrow of your desire with our products that offer actionable and up

-to-date financial tips on budgeting, saving, investment, retirement planning, side hustling to complement your main incomes, investment management services and dialogues with other experts in Personal Finance. As our slogan has it; Personal finance is a lifestyle and we promise to ensure you learn and implement the knowledge in your life. Some changes have to be accomplished but the outcome is worth it. Join us in this noble journey by follow us on all our social media handles. Instagram: https://www.instagram.com/achievefinancetz/
Facebook: https://www.facebook.com/achievefinancetz
YouTube: https://linktw.in/fJXves

Welcome!

02/09/2026

Kula bata inaruhusiwa kabisa as long as iko ndani ya bajeti yako.

Shida inaanza pale unapochukua pesa ya kodi ukalipie bili ya kiwanja au unanunua simu mpya ili uonekane, huku huna akiba yoyote.

Ili ufurahie maisha bila stress, fanya hivi:
1️⃣ Tengeneza Sinking Fund: Hii ni kwa ajili ya yale matumizi makubwa yanayokuja (k**a kodi, ada, au service ya gari). Usisubiri yakushtukize.
2️⃣ Tengeneza Lifestyle Fund: Hii ni bajeti yako ya vitu vidogo vidogo na kujipa raha. Ukitaka kutoka weekend, unatumia hii. Ikiisha, bata inaishia hapo hadi mwezi ujao!

Jifunze kutofautisha kati ya "I WANT IT" (Natamani) na "I CAN AFFORD IT" (Nina uwezo wa kuinunua bila kuathiri maisha yangu ya kesho).

Wewe unawezaje kubalance kati ya kusave na kufurahia maisha?

Tupe mbinu zako hapo chini! 👇🏾

02/09/2026

Dear Achiever.

Tulikuwa na wakati mzuri sana na warembo kutoka TEWS Tanzania

Tulizungumza kuhusu usimamizi na nidhamu ya fedha, uwekezaji na njia bora ya kuwa mwanamke makini, mdadisi na mwenye kutumia akili na utashi wake kujiongezea thamani ili kuvutia wateja wanaolipa, washirika katika mambo ya uchumi na biashara na kupata masoko.

Nilienda kufundisha lakini nilitoka nikiwa nimefundishwa pia na Aunt Sadaka pamoja na warembo kutoka TEWS Tanzania

Maswali yao, experience zao na hadhithi zao kwa ujumla zimenipa ufahamu mpya (always a student of life).

kwa huduma ya mafunzo kwa vikundi tupigie au tuma whatsApp 0753820744.

02/09/2026

Dear Achievers.

Batch 3 tunaanza leo.

Karibu kwa usajili.
WhatsApp 0753820744

Unataka kuwa na Uwezo wa Kutengeneza Tsh 1,000,000 na zaidi ndani ya Mwaka?Zingatia hizi tabia 10
02/09/2026

Unataka kuwa na Uwezo wa Kutengeneza Tsh 1,000,000 na zaidi ndani ya Mwaka?

Zingatia hizi tabia 10

kuweka ...

02/09/2026

Unapambana kila siku, unafanya kazi kwa bidii, lakini ikifika katikati ya mwezi huna hata elfu kumi ya dharura. Usimlaumu bosi wako mara nyingi tatizo linaanzia kwenye "Tabia".

Utajiri hauji kwa mshahara mkubwa tu; unakuja kwa kujenga nidhamu ya pesa. Ikiwa unataka kujua jinsi ya kudhibiti matumizi yako, kuanza kuweka akiba, na kuwekeza (k**a kwenye Faida Fund na Hatifungani), nimekuwekea darasa kamili!

Nimeandaa video mpya kule YouTube nikiangazia "TABIA 10 NZURI ZA KIFEDHA" ambazo ukianza kuziishi kuanzia leo, maisha yako ya kiuchumi lazima yabadilike.

🔴 Tazama Video Kamili YouTube Hapa: https://youtu.be/_4KL7BxB_JU

Kabla hujaenda kuitazama, niambie hapa kwenye comments: Ni tabia gani ya matumizi inakusumbua sana na unatamani kuiacha mwezi huu?

01/09/2026

Januari ulisema, "Mwaka huu ni wa kutafuta pesa na kuwekeza." Sasa hivi tuko katikati ya mwaka, ukiangalia akiba yako... inasoma sifuri.

Kwanini hatufikii malengo yetu ya kifedha? Si kwa sababu hatupati pesa, bali ni kwa sababu matamanio siyo mipango.

Kusema "Nataka kununua hisa" au "Nataka kuweka pesa Faida Fund" ni nzuri, lakini k**a huna mpango thabiti wa asilimia ngapi ya mshahara wako inaenda huko kila mwisho wa mwezi kabla hujagusa matumizi mengine, unajidanganya. Mipango thabiti inahitaji bajeti inayoandikwa na nidhamu ya kuifuata.

Wewe unakwamia wapi linapokuja suala la kupanga bajeti yako?

Tuambiane ukweli hapa chini

31/08/2026

Tuseme ukweli...

Wakati unaanza kazi na mshahara wa Laki 5, ulikuwa unapanda daladala kwa amani, unakula kwa mama ntilie, na bado mwisho wa mwezi unaweka akiba ya elfu 50.

Leo umepata promotion, unalipwa Milioni 2. Ghafla, daladala ina "joto", sasa hivi ni Uber/Bolt tu. Chakula cha ofisini hakifai tena, unaagiza kutoka kwenye migahawa ya bei mbaya. Umehama chumba kimoja, sasa umepanga ghorofa nzima Mbezi Beach—ambayo unalala huko masaa 6 tu.

Huu ugonjwa unaitwa "Lifestyle Inflation" (au Lifestyle Creep). Ni tabia ya kupandisha matumizi yako kila kipato chako kinapoongezeka. Matokeo yake? Unakuwa 'Masikini anayelipwa mshahara mkubwa'.

Utajiri sio kiasi gani unaingiza, ni kiasi gani unabakiza na kuwekeza.

👉🏾 Je, ni kitu gani kimoja ambacho ukipata hela nyingi huwa unashindwa kujizuia kukibadilisha? Ni simu, mtaa unaoishi, au marafiki? Tupeane uzoefu kwenye comments! 👇🏾

30/08/2026

Dear Achiever.

Karibu kwa huduma ya “Finance & Investment Talk” kwa vikundi. Yani, ni muhimu sana financial talk isikose kwenye agenda za mkutano wenu unaofuata.

Achieve Finance 🇹🇿 tuko tayari.

30/08/2026

Tufunguke leo. Umemkopesha mtu hela yako (bila hata riba), kwa nia nzuri kabisa ya kumsaidia. Siku ya kulipa ikifika:

A. Inabidi wewe ndio ujitilishe huruma.
B. Inabidi utunge stori (umwambie unaumwa ndio akulipe).
C. Unaanza kutishiwa wewe uliyekopesha!

Kwanini Watanzania wengi kwenye suala la "Personal Loans" hawana financial discipline? Shida ni nini? Ni kwamba hawana hela, au wanajua huwezi kuwapeleka polisi kwa sababu ni "watu wa karibu"?

Tupeane uzoefu hapa mbinu gani uliwahi kutumia kudai hela yako ikafanya kazi?

30/08/2026

Dear Achiever.

Vipande kamwe havizuii mchakato wa kuomba mkopo kuendelea k**a kawaida kulingana na taratibu za bank ama Taasisi ya kifedha.

Sikiliza video utaelewa.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Achieve Finance posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share