Huduma za Bima Tanzania

Huduma za Bima Tanzania Bima aina zote

Kwa huduma za Bima tutafute
11/03/2024

Kwa huduma za Bima tutafute

Kata Bima Kwa Ulinzi dhidi ya Majanga uwapo barabaraniWasiliana nasi kwa ushauri kuhusu masuala yote ya Bima
21/02/2024

Kata Bima Kwa Ulinzi dhidi ya Majanga uwapo barabarani

Wasiliana nasi kwa ushauri kuhusu masuala yote ya Bima

Ume Bima Njoo jipatie Bima Aina zote
21/02/2024

Ume Bima
Njoo jipatie Bima Aina zote

Bima ya moto ni muhimu katikabiasharaNyumbaKila mtu anaweza kukata bima kwa ushauri
16/01/2023

Bima ya moto ni muhimu katika
biashara
Nyumba
Kila mtu anaweza kukata bima kwa ushauri

🧶JE, WAJUA WAJIBU WA MTOA HUDUMA YA BIMA AU KAMPUNI YA BIMA WAKATI UTAKAPOWASILISHA MADAI YAKO??🧶👉Wakati mteja au mkatab...
14/01/2023

🧶JE, WAJUA WAJIBU WA MTOA HUDUMA YA BIMA AU KAMPUNI YA BIMA WAKATI UTAKAPOWASILISHA MADAI YAKO??🧶

👉Wakati mteja au mkatabima utakapowasilisha madai kwa kampuni ya bima, basi kampuni ya bima itatekeleza yafuatayo:

1.Itajiridhisha kwa kukagua na kuhakiki juu ya mkataba wako wa bima k**a ulikuwa hai(nikimaanisha ulikuwa endelevu au haujafikia kikomo wakati tukio la ajali au majanga yalipotokea)

2.Kuhakiki k**a mleta madai (mteja au mkatabima) ndiye yule aliyetajwa kwenye mkataba wa bima.

3.Kuhakiki na kujiridhisha kuwa janga, tatizo au hasara iliyotokea ni sawa na majanga yaliyotajwa kwenye mkataba wa bima wakati wa kukata bima.

4.Kukagua na kujiridhisha kuwa mteja kwa wakati wote amekuwa akifuata, kuzingatia au kutekeleza vigezo na masharti vilivyotajwa kwenye mkataba wa bima.Vigezo na masharti vipo kwenye makundi mawili ambayo ni:

*policy condition precedent-vigezo vyote ambavyo mteja inabidi atimize kabla ya kuingia kwenye mkataba wa bima au kabla mkataba wa bima kuanza rasmi.

*policy condition subsequent-vigezo vyote ambavyo mteja inabidi afuate wakati wote anapokuwa ndani ya mkataba wa bima (nikimaanisha vigezo vyote ambavyo inabidi mkatabima afuate kipindi chote cha mkataba wa bima)

5.Mtoa huduma ya bima atakuagiza kuleta vielelezo vya ajali,hasara au majanga yaliyotokea ili kuthibitisha uhalali wa madai uliyoyaleta.

Vielelezo vya kuthibitisha madai-nitavielezea kwa somo litakalofuata

Je, wajua wajibu wako k**a mkatabima?
Wajibu wako k**a mkata bima upo wa aina mbili ambao ni:-

(i) implied duties or condition- majukumu ambayo hayajaandikwa kwenye mkataba wako wa bima lakini inabidi uyatimize.Nayo ni k**a yafuatayo

-loss minimization principle (ni wajibu wa mteja kufanya k**a hauna bima na kuchukua hatua zozote zinazowezekana kupunguza hasara au kusababisha majanga au matatizo kuongezeka) Mfano :k**a una bima ya nyumba na moto umetokea unaunguza nyumba lazima uchukue hatua za kuzima moto na si kuacha nyumba nzima iteketee kwa moto kwa kigezo cha kuwa na bima.

-ni wajibu wa mteja (mkatabima) kuwasiliana na mamlaka husika za Kiserikali wakati wa majanga.Mfano, kutoa taarifa za janga la moto kwa Jeshi la zimamoto, kutoa taarifa za ajali kwa askari wa usalama wa barabarani au kituo chochote cha polisi kilichopo karibu na eneo la tukio la ajali

-Kutomzuia mtoa huduma ya bima au kampuni ya bima kufanya uchunguzi ili kujiridhisha na uhalali wa madai yako.

(Ii) expressed duties or condition-haya majukumu yapo mengi na ni majukumu yanayoandikwa kwenye mkataba wako wa bima na wewe k**a mteja inabidi uyazingatie na kuyatimiza. Mfano

-prompt notification (kutoa taarifa za ajali,hasara au tatizo kwa kampuni ya bima papohapo au kwa uharaka bila kupoteza muda).Usipotoa taarifa utakuwa umekiuka kigezo kimojawapo cha mkataba wa bima kwani hupaswi kukaa kimya unapopatwa na majanga au matatizo.

👉Kwanini unapaswa kutoa taarifa za haraka juu ya ajali, hasara au tatizo lililojitokeza?

>Kuruhusu kampuni ya bima kuchukua hatua za kupunguza hasara mfano k**a una bima ya moto na ikatokea nyumba inaungua kampuni ya bima itaomba usaidizi kutoka jeshi la zimamoto

>Kuruhusu kampuni ya bima kuchukua vielelezo vya ushahidi kwaajili ya kukusanya taarifa za ushahidi ili kufahamu ukweli. Hii hatua ni jambo linalohitaji umakini na haraka bila kupoteza muda.

>Kutoa nafasi kwa kampuni ya bima kuandaa utaratibu wa malipo ya fidia

>Kutoa nafasi kwa kampuni ya bima kutimiza na kutekeleza haki yake (the right of subrogation and salvage)
*yaani kampuni kukulipa fidia baada ya hasara na kupeleka gharama ilizotumia kwa kampuni nyingine iliyokuwa na wajibu wa kulipa hasara iliyotokea (subrogation)

*(Subrogation) Mfano kwenye bima ya gari baada ya ajali iliyosababisha uharibifu wa gari kampuni inaweza kumlipa mteja wake hasara zilizotokea na baada ya malipo ikapeleka gharama zilizotumika kukulipa fidia kwa aliyesababisha ajali na hapa (aliyemkatia bima anawajibika kulipa fidia hiyo).

*(Salvage) -kampuni ya bima baada ya kukulipa madai yanayohusu kitu kilichoharibika inayo haki ya kuchukua mabaki au sehemu zinazounda kitu kilichoharibika (mfano kwenye ajali ya gari baada ya kampuni kukulipa kwa kufanya matengenezo au kupewa gari jipya mabaki ya sehemu ya gari lililoharibika ni mali ya kampuni) hii ni salvage

AHSANTE SANA🙏

0621199717

Una ushauri kuhusu Bima Unahitaji bima yoyote k**a vile Bima ya magariBima ya moto Bima ya miradi ya ujenzi Bima ya Afya...
24/09/2022

Una ushauri kuhusu Bima
Unahitaji bima yoyote k**a vile
Bima ya magari
Bima ya moto
Bima ya miradi ya ujenzi
Bima ya Afya
Bima ya maisha
Bima ya pikipiki & bajaji nk
Wasiliana nasi 0756752545 /0736752545
Au njoo wasap 0756752545

Address

Ubungo
Dar Es Salaam
DARESLAAM

Telephone

+255756752545

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Huduma za Bima Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share