09/10/2023
・・・
Kampuni ya Southern Sichuan Port Industrial Invest Group (SPSI) inayomilikiwa na Serikali kutoka jimbo la Sichuan imeingia mkataba wa kununua mazao ya kilimo kutoka Tanzania kupitia kampuni ya TCCI ya Guangzhou.
Mkataba huo umetiwa saini na Bw. Hangyong Yang, Mwenyekiti wa Kampuni ya Southern Sichuan Port Industrial Invest Group (SPSI) na Bw. John Rwehumbiza, Mkurugenzi Mtendaji kwa upande wa kampuni ya TCCI. Sherehe za utiaji saini zikifanyika katika Ofisi za Konseli Kuu jijini Guangzhou .
Mwezi Agosti 2023, Kampuni ya TCCI ilitembelea Tanzania na kufanikiwa kutia saini Mkataba wa Makubaliano na Bodi ya Mazao Mchanganyiko ya Tanzania (CPB) ili kampuni ya TCCI iwe na uwezo wa kupata mazao hayo kwa kiwango inachohitaji kwa soko la China.
Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa kampuni ya SPSI Bw Yang amemueleza Konseli Mkuu Bw kuwa kampuni yake pia ina nia ya kuwekeza katika sekta ya madini pindi biashara ya ununuzi wa mazao itakapokuwa imeshamiri.