AIM Globale géré l'homme et la femme a être responsable de sa famille et de soit mm.

17/08/2020

*Mwenye shahada* asiye na ajira kuna wakati huwa anaona bora angeishia kidato cha nne na angefanya shughuli nyingine...

Na aliyeishia darasa la saba kutokana na hali ngumu ya maisha aliyonayo kuna wakati anaona alipaswa kufika chuo kikuu ili awe na maisha mazuri...HAYO NDIO MAAJABU YA MAISHA...

Cha kushangaza ni kwamba maisha huwa hayana formula maalum...aliyesoma maskini, wakati asiyesoma ni tajiri, na kuna asiyesoma maskini wakati aliyesoma ni tajiri...

Mwenye pesa anaumizwa na mapenzi mpaka anatamani kuwa Single wakati asiye na pesa anatamba na mapenzi mubashara ya kula ugali na miguu ya kuku

Unawaza kuacha shule ili ufanye biashara kwa sababu watu wengi wanafanikiwa na muda huo huo kuna mwenzako anawaza kuacha biashara kwa sababu biashara hailipi ili arudi shule akimaliza akaajiriwe...

Ingelikuwa maisha yana jibu moja wala tusingeona maajabu yake...

HUAMINI...? wakati wewe unaumiza kichwa ufanye nini ili ufanikiwe kuna mwenzako anatamani angefikia walau hata robo tu ya maisha yako...

Ishi kwa amani...ishi kwa upendo, ishi kwa furaha...maisha ndiyo haya haya...hakuna formula zaidi ya kuishi maisha yako...

Hard work pays...lakini wakati mwingine kwenye maisha kufanikiwa huwa ni bahati, ila ni kwa wale tu ambao wanazielekeza bahati kuja upande wao...

Kuna anayejituma sana lakini miaka nenda rudi hafanikiwi na yupo mvivu na uvivu wake anatusua...kuna anayeweka bidii kubwa kwenye kazi/biashara na bado hafikii malengo...(maajabu ya Maisha)

Usiumize sana kichwa kuishi maisha ya wengine kwenye maisha yako....bali unatakiwa kutumia muda wako mwingi kuishi maisha yako kwenye maisha yako...

Dunia inakuruhusu kupanga na kubonyeza kitufe unachoona ni sahihi na huku ikiwa imeficha "button" ya matokeo...kazi yako kubwa ni kuumiza kichwa kipi ni kitufe sahihi unachopaswa kubonyeza ili kikuonyeshe "button" ya matokeo unayoyahitaji...

Kujua Zaidi pakua KIPAJI APP 📲 na angalia Filamu ya MATUSI..

Adresse

Goma

Heures d'ouverture

Lundi 09:00 - 17:00
Vendredi 09:00 - 17:00

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque AIM Globale publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Partager

Type